Kutafakari kuhusu Lk 15, 1-3.11-32
Sura ya kumi na tano ya toleo la Luka ni maarufu
miongoni mwa mifano ya Yesu. Hii inaitwa sura ya Mifano ya huruma. Tuna mifano
mitatu (Kondoo aliyepotea: 4-7; Sarafu iliyopotea: 8-10; Mwana mpotevu: 11-32).
Lakini siku ya leo liturjia inatujulisha moja peke yake, yaani, mfano wa mwana
mpotevu. Mfano huu unaonyesha tabia ya huruma ya Mungu kuhusu wenye dhambi na
furaha ya kukutana tena na yule ambaye alipotea. Kwa kufahamu nia ya Yesu kwa
uhusiano na mifano hii tunahitaji kutafakari kwanza kuhusu mazingira ambayo
Yesu aliishi. Katika muktadha huo, baadhi ya watu
walijiona wanastahili upendo wa Mungu zaidi kwa ajili ya uaminifu wao kwa
Sheria. Walichukua mamlaka ya kuwatenganisha watu, wakiwapanga kama wema au
wabaya. Mamlaka haya hayatoki kwa Mungu kwa sababu kipimo ni ubaguzi. Walisahau
kwamba mbele ya Mungu watu wote ni sawa. Mungu habagui katika upendo wake. Kwa
upande wake watoza ushuru na wenye dhambi ni watoto wake sawa na Mafarisayo na
Waandishi wa Sheria. Ikiwa hao wanaweza kuzaa ndugu, tena wanaweza kuishi
katika ushirika na Mungu, anayekaribisha kila mtu ili awaokoe wote.
Ingawa yako
matukio mengi katika Agano la Kale, ambayo yanaonyesha njia maalum ya Mungu ya
kutenda, ni “katika Yesu Kristo kwamba huruma ya Mungu imepata kuwa hai na
yenye kuonekana, na hata ilifikia kilele chake katika Yeye... Yesu ni uso wa
huruma ya Baba. Kila kitu ndani yake
kinaongelea huruma. Hakuna chochote kwake kinachopungukiwa na huruma (Baba Mt
Francisco).” Kama alama ya
huruma ya Mungu, Yesu ana chaguo wazi sana, yaani, “Mwanamume huyu
anawakaribisha wenye dhambi naye hata anakula nao”. Maneno haya yalisemwa na wale
waliompinga Yesu. Kwa kweli, Yesu aliongea kuhusu huruma ya Mungu si kwa maneno
tu, bali “kwa neno lake,
matendo yake na kwa nafsi yake yote.” Yeye alitumia ishara nyingi za makaribisho,
akithibitisha lengo la ujumbe wake na ukweli wa mafundisho yake. Kwa kweli,
watozaushuru wengi, makahaba na wengine waliokataliwa na jamii walijihisi wamekaribishwa
na Yesu na, kwa hivyo, kubadilishwa kwa mkutano na huruma ya Mungu.
Ingawa katika mfano wa mwana mpotevu tunasikia tukio
la kijana mdogo na hisia za kijana mkubwa, lakini ni baba wa vijana hawa wawili
ndiye aliye mhusika mkuu wakati wote. Uhusiano wake wa mapendo kwa vijana wake,
ambao wote ni wapotevu kwa njia tofauti ndio umuhimu wa tukio hili. Kulingana
na Yesu, baba huyo ni kama Mungu ambaye ana watoto tofauti na kushiriki nao
zawadi zake kwa njia sawa. Yeye anawapenda wote na kutaka kwamba watu wote
wajihisi wakiwa katika familia, kushiriki kwa furaha yake kama Baba. Katika
familia hii anautoa utunzaji na ulinzi ili wawe na maana nzuri ili kubaki naye
daima. Wakati yeyote anaamua kutenda kinyume naye na kubaki mbali sana naye,
sio kwa maana mtu huyo hajihisi kupendwa, bali ni kwa sababu anajiona mwenye
uhuru. Kama huu ni uzoefu wa upendo wa Baba: huu ni huria na kuuzaa uhuru. Sisi
pia tunahisi mbali sana na Mungu wakati sisi hutenda kinyume naye, yaani,
tunapomkosea. Yeye anajihisi ameachwa na kusalitiwa, lakini haachi kutupenda. Kama
yule baba, Mungu anashughulika sana na maisha yetu. Anakuja kututafuta ili kutupa
sisi ulinzi na utunzaji wake. Kwa hivyo tunahisi majuto na kivutio ya kuishi
tena uzoefu wa ushirika tumeopoteza. Ingawa mara niyingi tunakataa utambulisho
wetu wa wana, kupitia dhambi zetu, Mungu haukatai utambulisho wake wa Baba kamwe.
Katika mfano huu yuko pia mwana mkubwa ambaye
hajihisi mwana kwa sababu anajiona kuwa ni mfanyakazi wala anajihisi ndugu, kwa
sababu anatojali ndugu yake mdogo. Tabia ya huyo mwana mkubwa inaizuia furaha
kamili ya Baba na ukamilifu wa sikukuu. Kumrudia Mungu ni maana ya furaha kubwa
kwake. Lakini furaha yake haiwezekani kuwa kabisa ikiwa hatushiriki katika
hisia zake kuhusu wengine. Hataki kwamba tuwe wivu kuhusu njia yake ya kupenda;
anataka kwamba tutende kama yeye alivyo. Kwa hivyo Yesu alisema, “Muwe na
huruma kama Baba yenu alivyo.” Upatanisho na wengine ni kipimo ili uhusiano
wetu na Mungu uwe kweli. Hii ni njia ya kweli ya toba
iliyo mwendo wa muda mrefu na huanza mioyoni mwetu. Kupitia Ekaristi
hii, turuhusu kuguswa na huruma ya Mungu ili tuweze kuwa vyombo vya huruma hii
kwa wale wanaohitaji msamaha wetu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário