domingo, 28 de fevereiro de 2016

MUNGU ANATUPA NAFASI MOJA ZAIDI TUWEZE KUZAA MATUNDA MAZURI

Kutafakari kuhusu Ex 3, 1-8a. 13-15; 1Kor 10,1-6.10-12; Lk 13,1-9

      Somo la kwanza linaongea kwamba huko mlimani Horebu Mungu anatokea kwa Musa na kuudhihirisha utambulisho wake kama Mungu aliye yupo katika historia ya ubinadamu daima. Yeye ana unyeti mbele ya hali ya mateso ya watu wake na kuamua kuwaokoa kutokana na utumwa wa Misri, kuwaongoza kwa nchi njema, yaani nafasi ya kuishi maisha mapya. Katika mwendo huu Mungu anatumia Musa kama chombo cha huruma yake na Musa anakubali kuiacha mipango yake ya maisha na kuchukua mpango wa Mungu ili ukombozi wa Mungu ufikie Watu wake kubadilisha hali ya mauti kuwa hali ya uzima. Katika somo la pili, Mt Paulo anawakumbusha Wakristo wa Korinto kwamba miongoni mwa wale waliopitia huruma na ukarimu wa Mungu wengi waliangamizwa jangwani kwa sababu maisha yao hayakumpendeza Mungu. Hili ni onyo kwa sisi sote ya kuishi kulingana na zawadi za kiroho tumepokea kwa sababu yule ambaye anatoa zawadi hizi antarajia mabadiliko ya maisha yetu kama matokeo ya tendo lake la ukarimu.  
        Katika injili, baadhi ya watu alimwendea Yesu na kumpasha habari kuhusu ukatili wa Pilato kwa ajili ya Wagalilaya. Kama ilivyotokea mara zingine, hii ni nafasi zaidi aliyotumia Yesu awafundishe na kuwaalika kwa toba. Kwanza kabisa alipaswa kusahihisha mawazo fulani yapo miongoni mwao kwamba watu ambao wanateseka ni kwa sababu ya dhambi walizotenda. Kulingana na mawazo haya, mateso yote yalionekana kama matokeo ya dhambi. Kama hii ilikuwa hali ya wagonjwa wote katika mazingira ya Yesu. Kwa hivyo, kabla ya kufanya muujiza wowote alimwambia mgonjwa, “Nakuondolea dhambi zako”. Alisema hivyo kama ushuhuda kwa jamii nzima ambayo pia ilipaswa kupona na hali ya ubaguzi kuhusu wagonjwa. Kulingana na Yesu njia hii ya kufikiri ni hatari kwa sababu inaweza kuwa kikwazo kwa watu kukataa kuwasaidia wale walio katika mateso. Kutokuwa na ahadi kwa ajili yao na kutofautiana kunayaongeza zaidi mateso yao.
        Kwake Yesu, mateso hayatokani na Mungu, bali yanaweza kuwa ni nafasi kwa mtu kumrudia Mungu kwa moyo wote na kumtukuza. Inawezekana pia kuwa ni nafasi ya jumuiya nzima kujifunza juu ya huruma waipokeayo kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kuwaongoza waonyeshe upendo na huruma hasa kwa wale wanaoteseka. Sisi ni kama wagonjwa kwa sababu ya uzoefu wa dhambi. Wakati Yesu aliposimulia mfano kuhusu mti bila rutuba, alitaka kuongea kuhusu uvumilivu na huruma ya Mungu kwa ajili ya wanadamu wote. Kama ilivyotokea na mti ule, Mungu anataka kutupa nafasi moja zaidi ili tuweze kuzaa matunda anayotarajia. Mungu hutupa muda ya kukomaa na kuishi maisha bora. Subira ya Mungu ni nafasi kwetu ya kupata wokovu kwa njia ya toba.

        Kwaresima ni nafasi tupewayo na Mungu ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu kwa uthabiti zaidi. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuacha kuwatenga watu katika makundi tofauti ya walio wema na walio dhambi na kuwaona wote kama walio dhambi wanaohitaji msamaha wa Mungu. Kulingana na Yesu, Mungu anatarajia maisha yetu yaweze kumpendeza kupitia matunda mazuri. Tumepokea nafasi nyingi ili tufikie lengo hili. Katika uzoefu wa watu wa biblia yeye anajifunua kama mkombozi na mwenye uvumilivu mbele ya hali ya udhaifu wa watu. Kwa upande wa Mungu uvumilivu na huruma; kwa upande wetu ushujaa na toba. Kama ilivyotokea na Musa, Mungu anatualika kwa uzoefu tofauti ambao unalenga kutubadilisha kuwa katika vyombo vya huruma yake.          

Fr Ndega 
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: