Kutafakari kuhusu Lk
9, 28b-36
Tukio la kugeuka sura kwa Yesu kulitokea baada
ya siku sita ya ufunuo kuhusu mateso, kufa na kufufuka kwake na mwaliko wake
kwa wanafunzi wa kumfuata kulingana na njia yake mwenyewe, yaani “Kujikana
mwenyewe, kuuchukua msalaba wake na kumfuata Yesu.” Habari ya kugeuka sura kwa
Yesu tena inafuatwa na tangazo la pili kuhusu kifo na ufufuko wake. Kwa uzoefu
huu Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo na Yohana. Kwa nini
wafuasi hawa? Labda kwa sababu aliwapendelea kuliko wengine. Injili haiongei
maana ya habari hii. Yesu aligeuka mbele ya wafuasi wake na ishara kuu zilikuwa
nguo na mwili wake. Yesu aliwaonyesha kidogo utukufu wake na hali ya wakati ujao
kuhusu mwili wa yeyote anayemfuata kwa uaminifu. Yesu anashiriki utukufu wake
na wanafunzi wake kwa maana inampendeza kufanya hivyo ili wawe na furaha moja ya
vile Mwalimu wao alivyo.
Kama illivyotokea kuhusu jangwa, Mlima pia ni mahali
muhimu katika uhusiano wa Watu wa Israeli na Mungu; katika mwendo huu, Musa na
Eliya wana ushiriki maalum. Katika Agano la Kale milima iliyojulikana sana ni Mlima
Sinai na Horebu. Ilikuwa katika Mlima Sinai ambapo Mungu alikutana na Musa na kuwawekea
Waisraeli mkataba/agano. Ilikuwa katika Mlima Horebu ambapo Eliya alijiandaa
kwa muda mrefu akutane na Mungu. Katika Agano Jipya Yesu alitumia sana mahali
huko mlima kama rejeo ya uhusiano wake na Baba na kama eneo kwa matukio muhimu
katika kazi yake. Kulingana na utamaduni mmoja wa zamani, tukio la injili ya
siku ya leo lilitokea juu ya milima Tabor.
Uwepo wa
Musa na Eliya unaongea kuhusu rejea ya ufunuo katika Agano la Kale. Waliongea na
Yesu wakionyesha kwamba hakuna mpasuko/mshipa kati ya mafundisho yao na mafundisho
ya Yesu, bali uhusiano na mwendelezo. Lakini kulingana na sauti iliyosikika
kutoka kwenye wingu, mwendelezo huu, ambao ni Yesu, lazima kuwa kipaumbele
katika maisha ya wanafunzi kwa sababu ni Yesu peke yake kwa mamlaka aliyoyapokea
kutoka kwa Baba ili kufundisha na kutafsiri kamili lile lililosemwa na mababu wa
zamani. Kusikiliza katika Biblia ni
kitenzi chenye nguvu sana. Hii ni tabia ya myahudi mbele ya Neno la Mungu,
akiweka vitendoni au kufanya mazoezi/vitendo kuhusu yale aliyosikia. Kusikiliza
kuna uhusiano na kushika au kutenda. Baba anashuhudia kuhusu Mwana wake,
anamweka kama rejeo cha maisha yetu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni”.
Huu ni pia mwaliko ili tufananishe maisha yetu kulingana na Neno la Yesu. Neno
la Yesu ni kipimo ili mtu awe pia mwana mpendwa wa Mungu kama Yeye. Tunashiriki
katika kugeuka sura kwa Yesu kupitia kusikiliza makini kwa Neno lake.
Kuhusu
mambo hayo Mtakatifu Yohana Calabria alisema: sisi ni makini sana kwa maneno ya
binadamu na kuhusu hiyo ni sawa. Lakini tunapaswa kuwa na uangalifu zaidi kwa
Neno la Mungu ambalo ni – consecratory – huweka wakfu, ni kwamba, linalifanya
lile linalosema.” Mtakatifu Yohane Calabria ilikuwa
anasema hasa kuhusu injili ambayo ni sheria kwetu Poor Servants of Divine
Providence. Katika sehemu nyingine ya maandiko yake alisema: “Ikiwa sisi
huamini katika maneno ya kuapishwa kwa – consecration – katika misa, yaani “twaeni
mle wote, twaeni mnywe wote”, tunapaswa kuamini pia wakati Yesu asema: “Msiwe
na wasiwasi” au “Baba yeno wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo
vyote” au “mtafuteni kwanza ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote
mtapewa kwa ziada.” katika maneno mengine, kutokana na Maneno ya Yesu tunaalikwa
kuwa “Injili hai.” Hiki ni kipimo kwetu ili tuweze kumtambua uso uliogeukwa wa
Yesu katika nyuso zenye mateso za ndugu wengi miongoni mwetu. Neema ya Mungu itusaidie kulisikiliza Neno lake kwa uangalifu na kutangaza habari
njema ya siri ya Mwanae kama njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário