domingo, 31 de janeiro de 2016

KUONGOKA KWA MTAKATIFU PAULO NI KIPIMO CHA KUONGOKA KWETU


Kutafakari kuhusu Mk 16, 15-18

      Hii ni nafasi maalum ya kuonyesha upendo wetu kwa kazi ya Mungu kama alivyo Mt. Paulo. Mtu huyo alikuwa mcha Mungu na kushughulika sana kwa ajili ya dini yake. Kupitia njia yake ya kuishi sheria kwa uaminifu, aliamini kwamba akawa anampendeza Mungu. Kwa jina la Mungu aliwatesesha watu wengi. Kwa sababu ya matendo ya Sauli, aliye na ushabiki, watu wengi walikufa. Moyo wa ibada na nguvu zake zote zilitumika kwa kutangaza Mungu wa mauti na uwepo wake ulisababisha hofu na mateso kwa watu. Hakika hakuwa akitumikia Mungu wa kweli. Basi ufunuo wa Yesu wakati wa safari ya Sauli ulikuwa maonyesho ya kwamba kujitoa kwake hakumpendeza Mungu. Sauli alipaswa kugundua tena maana ya maisha na kazi yake. Alikuwa aliyetesesha na sasa ndiye aliyeteseka. Kulingana na maneno yake mwenyewe, tunaweza kusema kwamba Sauli alizaliwa tena akiwa mjumbe mkuu wa Yesu kwa mataifa yote. Alipata kufanya kazi zaidi kuliko mitume wengine wote kwa ajili ya Yesu. Huu ni mwendo wa toba ambao sisi sote tunaalikwa kuchukua.   

       Uwezo wa Paulo wa kuongea na kufundisha unatoka kwa Yesu ambaye ana maneno ya neema na nguvu. Ingawa yeye ni yule peke yake kwa mamlaka ya kutangaza wokovu wa Mungu, alishiriki mamlaka hii na Paulo na wanafunzi wengine wake ili watumikie watu, wakidhamini maisha mengi kwa wote. Kulingana na injili ya siku ya leo, kipimo kwa kuishi maisha mengi haya ni imani, ambayo huja kwetu kupitia hali ya ubatizo. Wanafunzi walitumwa kama wajumbe wa habari njema kwa viumbe vyote kwa sababu injili haina mpaka. Maisha mapya ambayo Yesu alileta kupitia ufufuko wake yanafikia uumbaji mzima. Yesu alikuwa amewaahidia kuandamana na safari yao mpaka upeo. Ingawa uwepo wa mwili wa Yesu usionekana tena, Roho wake yupo daima katika safari ya mitume na maisha ya wote waliomwamini umeyafanya maneno yao ufanisi kupitia ishara nyingi na matendo mengi mazuri.

      Utumishi kwa watu ambao ni wa Mungu ni utumishi kwa Mungu. Kwa hivyo ni lazima kuwa macho kuepuka kuyatumia mamlaka kwa njia mbaya. Mbele yao Yesu alitenda kwa mamlaka kinyume na nguvu za maovu ambayo yaliwapooza watu, yakiwazuia kushiriki kikamilifu katika jamii. Aliwadai njia ya unyenyekevu wa maisha kupitia kujinyima na kujitolea hasa kwa ajili ya wagonjwa, kutangaza ukaribu wa ufalme wa Mungu. Ni jukumu lao kutangaza ufalme wa Mungu, lakini ikiwa watu hawalikubali pendekezo lao si jukumu lao tena. Wanafunzi wa Yesu wanapaswa kutenda kama mwalimu wao alivyo, yaani kuheshimu uhuru wa wengine. Ufalme wa Yesu ni ufalme wa uhuru na amani, wa haki na msamaha. Habari ya ufalme huu inatokana na ukarimu wa Mungu. Nayo ni njema maana ni matokeo ya bure, kuusaidia uhuru.
 
     kama wanafunzi wapya wa Yesu sisi pia tunahitaji mkutano wa kuongoka/toba kama ilivyotokea na mt. Paulo. Kwanza kabisa, tunapaswa kuwa macho kwa msukumo wa Mungu na kuzifuata nyayo za Yesu kuchukua njia yake ya maisha, yaani njia ya unyenyekevu. Hatuwezi kufikiri kwa hakika kwamba tunampendeza Mungu wala kwamba hatuhitaji mwendo wa toba. Mwendo huu ni wa muda mrefu sana. Ingawa Paulo alikuwa mtume mkuu aliruhusu kusaidiwa na marafiki wengi, yaani Luka, Marko, Barnabas, Timotheo, Tito na viongozi wengine wa jumuiya ambazo alitengeneza. Kulingana na uzoefu wake mafanikio ya utume wetu yanawezekana ikiwa uzoefu wa kutenda pamoja unapata kushinda uzoefu wa kutenda mtu akiwa peke yake, kusaidiana katika jumuiya na kwa manufaa wa jumuiya. Tunaweza kutangaza halisi ukaribu wa ufalme kupitia utumishi wetu wa ukarimu na bure, kuheshimu wale waliotenda tofauti nasi. Baadhi ya ugumu katika safari yetu tunapaswa kukabili kupitia roho ya sala na toba daima. Ukarimu na utayari wetu uwe vyombo ambavyo Mungu aweze kutumia kuwajalia wote maisha mengi.

Fr Ndega

Mapitio: Sara   

sexta-feira, 29 de janeiro de 2016

MAPENDEKEZO YA YESU YALISABABISHA UMWINGILIO KWA WENZAKE


Kutafakari kuhusu Yer 1, 4-5. 17-19; 1Kor 12,31. 13,1-13; Lk 4, 21-30

Liturjia ya jumapili hii inaongea kuhusu umuhimu na hatari za unabii. Kwa kuchukua kazi hii ngumu ni lazima ujasiri na utayari, hasa katika mazingira magumu kama yale ya Yeremia na Yesu. Somo la kwanza anasimulia wito wa Yeremia kama historia ya upendo. Mungu mwenyewe anamwita ili awe mjumbe wake. Mungu anajua kuhusu ugumu na udhaifu wa Yeremia na, kwa hivyo, anaahidi utunzaji na ulinzi. Wito wa Yeremia ni matokeo ya uzoefu wa Neno la Mungu ambalo linampa uwezo wa kuongea na kushauri kwa jina la Bwana. Nabi wa kweli hasemi katika jina lake mwenyewe, bali asema tu yale ambayo Bwana anamwamuru kusema. Kulingana na somo la pili msingi wa uzoefu wa binadamu ni upendo. Upendo lazima kuwa hamasa ya matendo yetu kwa sababu bila upendo kila kitu tunachofanya ni bila maana. Kama sisi ni manabii tangu ubatizo, wito wetu ni pia historia ya upendo na mafanikio katika safari yetu inawezekana tu kupitia upendo. Upendo ni maana ya utambulisho wetu kama wakristo.    
Kulingana na kutafakari kwetu kuhusu injili ya jumapili iliyopita, Yesu alienda kijijini mwake Nazareti na kutangaza Neno la Mungu kama mpango wake wa maisha. Watu walishangazwa sana kwa sababu ya maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake. Kwa kweli Yesu aliishi kwa furaha na shauku utambulisho wake kama aliyechaguliwa na Mungu ili atangaze mpango wa upendo na wokovu wake. Uzoefu wake miongoni mwa wenzake ungalikuwa mzuri ikiwa Yesu angalisema tu yale ambayo walitaka kusikiliza. Lakini Yesu hana hofu na neno la Mungu halina mipaka. Aliwapendekezea njia mpya ya maisha na mabadiliko ya mawazo. Pendekezo la Yesu si ngumu; yeye anatarajia tabia tofauti tu. Hii ndiyo ni maana ya umwingilio wao/kukasirika kwao. Mara nyingi maneno ya Yesu yalisababisha mabadiliko maishani mwa watu wengi kwa sababu maneno yake yana nguvu yenyewe. Kwa hivyo alipata wafuasi wengi. Ikiwa mabadiliko yaliyotarajiwa hayatokei kwa baadhi ya watu, shida siyo kwa upande wa Yesu.  
Watu wa kijiji cha Yesu walijua kila kitu kumhusu yeye na walitumia hiki kama kipimo cha hukumu au utambuzi. Kujua kwao kwa awali kumhusu Yesu kuliwazuia kumjua nani ndiye. Yesu kama wokovu wa Mungu, ndiye utimizaji wa maandiko, lakini alikataliwa na wale wanajiona waliojua maandiko. Labda walikuwa na mazoea ya kukubali tu yale yaliyokuwa rahisi kwao, wakirekebisha Neno la Mungu kulingana na njia yao ya maisha, bila kuwa tayari ya kuishi kwa mapitio yanayotokana na Neno hili. Walimkataa Yesu kwa sababu walijifunga kwa upya wa Mungu uliodhihirishwa na Mwana wake. Ilikuwa ngumu sana kwao kufahamu kwamba ingawa Yesu alikuwa mwana wa Yosufu ndiye Mungu kweli. Je! Kujua kwetu kuhusu Yesu kumetusaidia kukua katika imani na kuimarisha uhusiano wetu naye?

Wakati Yesu alichukua hali yetu ya binadamu, alijitambulisha na hali hii, lakini akatambua pia kwamba vitu vingi vilipaswa kubadilika. Kwa hivyo alijulisha pendekezo mpya la maisha. Kwa upande wetu, kuishi kwa uhusiano wa kweli na Yesu hautoshi mshangao mbele ya hekima ya maneno yake kama wenzake walivyo, bali tunapaswa kuruhusu kwamba ujumbe wake wa upendo na ahadi uwe hai ndai yetu. Kama watu kutoka Nazareti, mara nyingi sisi pia tumelipinga Neno la Yesu ambalo linauliza maswali kuhusu tabia na matendo yetu ya kila siku. Kushiriki katika utume wa Yesu ni kuchukua pamoja naye hali ya wengine, hasa watu maskini. Hatuwezi kufikiri kwamba habari tumepokea kuhusu Yesu yatosha kwa safari yetu ya wito. Ni muhimu kuruhusu kwamba yeye mwenyewe ajidhihirishe kwetu kwa nguvu yote ya upendo wake siku zote za maisha yetu. Kama ilivyotokea na Yesu, sisi pia tunapaswa kuwa watu ambao wanalenga mapendekezo ya Neno la Mungu. Turuhusu kwamba maneno haya yatuongoze ili tufanye mapenzi ya Mungu. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara

domingo, 24 de janeiro de 2016

THE MESSENGER OF GOOD NEWS FOR THE POOR AND REJECTED ONES


Reflection from Lk 1, 1-4: 4,14-21

The first part of the gospel speaks that the good news of Jesus generated many witnesses. Our faith is result of the experience, that is, experience which we have received from the people who advanced us and the experience of personal searching, personal meeting with the Lord. The life of the ones who advanced us continues witnessing that without experience our faith in Christ is weak, deprived of meaning. The evangelist Luke addresses his gospel to some person called Theofilo, because it was habit in the First century. Theofilo was prominent person in the pagan society whom became a Christian because the preaching of the apostles. Theofilo means “beloved of God”. Like that is the result of our experience of the Word of God, that is, it makes us also beloved of God. The second part of the gospel is about the experience of Jesus in his hometown, place where he was brought up. He went there led by the Holy Spirit and proclaimed the Word of God with enthusiasm as his own project of life to a people whom were waiting for the revelation of the Messiah with fervour/passion.

Jesus chose a liturgical moment to proclaim the priority of his mission. Feels himself anointed and sent by the Holy Spirit to proclaim good news to the poor and liberation to the oppressed; he is able to recover their hope and give them back their joy of living. This reality is reason of identity for Jesus and part of the plan of love and salvation of his Father. The priority of Jesus is the priority of God. So, we can imagine the great joy Jesus felt internally because of this way of God acting. God loves each person and wants to reach all with his love. But there are some ones whom need special care, because they are rejected by the society. God requests  our attention concerning this reality.

In Jesus, it starts a time of grace and salvation. Jesus is the Saviour whom came to set free all human beings who lost their freedom because the sin. The liberation which Jesus proclaims goes beyond the spiritual reality caused by the sin. He wants to reach the whole society which has mentality against the plan of God revealed by Jesus. Like it happens in another passage, this revelation of Jesus is part of the announcement of the Kingdom of God which brings a proposal of changing. All of us together with the society should think better about the direction which we are giving to the life. Jesus wants to build a new humanity and society. He can do it alone but prefers to involve us in order we have the same sensitivity he has and we should have the same priority of his mission. The strength of the Word of Jesus comes from the Holy Spirit. The same Spirit who led Jesus in his mission wants to lead us also in order we may be able to perform new relationship with the poor people and other rejected among us. The revelation of Jesus is motivation for us in order we should make the difference in the life of many people. May his grace help us to be instrument of goodness and special care for those who are in need.


Fr Ndega

MJUMBE WA HABARI NJEMA KWA MASKINI NA WALIOKATALIWA NA JAMII


Kutafakari kuhusu Lk 1, 1-4: 4,14-21

        Liturujia ya jumapili hii inaongea kuhusu umuhimu wa Neno la Mungu ambalo lazima kusikika kwa heshima na kutangazwa kwa shauku. Neno hili ni alama ya upendo na utunzaji wa Mungu kwa watu ambao ni mali yake. Katika somo la kwanza, Ezra aliitangaza Torati ambayo ni Neno la Mungu kwa Waisraeli. Watu walisikiliza kwa uangalifu na kujibu kwa utayari. Neno la Bwana ni faraja na kutia moyo. Hili Neno ni maana ya furaha ambaye inakuja kutoka kwa Bwana na kuitoa nguvu kwa watu wote. Kupitia Neno la Mungu watu wanakumbuka mambo makuu ambayo yaliwapa maana ya utambulisho kama Watu wa Mungu. Ni mwaliko wa kumsifu Mungu kwa sababu ya uaminifu wake na kufanya upya ahadi yao ya waruhusu kuongozwa na Mungu ambaye anaongea kuzionyesha njia za uzima na ukombozi. Kama Watu wa Agano la Kale waliokusanyika kama mtu moja kwa sababu ya Neno la Mungu, vivyo hivyo ni uzoefu wetu kama washiriki wa mwili wa Kristo, yaani ingawa sisi ni wengi, tulibatizwa kuwa mwili mmoja. Karama mbalimbali ambazo tumepokea ni kwa ajili ya manufaa ya mwili mmoja huu.
Sehemu ya kwanza ya injili inaongea kwamba habari njema ya Kristo iliwazaa mashahidi wengi. Imani yetu ni matokeo ya uzoefu, yaani uzoefu ambao tumepokea kutoka kwa waliotutangulia na uzoefu wa kutafuta binafisi. Maisha ya wale waliotutangulia yanaendelea kushuhudia kwamba bila uzoefu imani yetu katika Kristo ni haba. Mwinjilisti Luka analitoa andiko lake kwa heshima ya mtu fulani aliyeitwa Theofilo, kwa sababu katika karne ya kwanza yalikuwa mazoea kufanya hivyo. “Theofilo alikuwa mtu wa maana aliyesifika katika jamii ya Wapagani, aliye kuwa Mkristo kutokana na mahubiri ya mitume.” Maana ya neno Theofilo ni “mpendwa wa Mungu”. Kama haya ni matokeo ya uzoefu wetu wa Neno la Mungu, yaani tunakuwa wapendwa. Sehemu ya pili ni kuhusu uzoefu wa Yesu mjini mwake Nazareti, mahali alipolelewa. Alienda huko akiongozwa na Roho Mtakatifu na kutangaza kwa shauku Neno la Mungu kama mpango wake kwa watu waliotarajia ufunuo wa Masiya kwa hamu sana.
Yesu alichagua wakati wa liturujia kwa kutangaza kipaumbele cha kazi yake. Anajihisi aliyetiwa mafuta na kutumwa na Roho ili atangaze habari njema kwa maskini na ukombozi kwa wanaoonewa; yeye anaweza kuyafufua matumaini yao na kuwarudishia furaha ya maisha yao. Hali hizi ni maana ya utambulisho wa Yesu na sehemu ya mpango wa upendo na wokovu wa Baba yake. Kipaumbele cha Yesu ni kipaumbele cha Mungu. Basi, tunaweza kuwaza furaha kubwa imo ndani ya Yesu kwa sababu ya njia hii ya Mungu ya kutenda. Mungu anapenda kila mtu na kutaka kuwafikia wote kwa upendo wake. Lakini kuna baadhi ya watu ambao wanahitaji utunzaji maalum, kwa sababu wanakataliwa na jamii. Mungu anatudai kuwa macho kwa hali hii. 
Katika Yesu wakati wa neema na wokovu unaanza. Yesu ni mkombozi ambaye alikuja kuwaweka huru wanadamu wote waliopoteza uhuru wao kwa sababu ya dhambi. Ukombozi ambao Yesu anatangaza ni zaidi kuliko hali ya roho iliyosababishwa na dhambi. Anataka kuifikia jamii kabisa, kwa sababu hali hii ina mawazo kinyume na mpango wa Mungu uliodhihirishwa na Yesu. Kama inavyotokea katika kifungu kingine (k.m. Mathayo) hii ni sehemu ya tangazo la Ufalme wa Mungu ambalo linalihusu pendekezo la mabadiliko. Sisi sote pamoja na jamii nzima tunapaswa kufikiri vizuri kuhusu mwelekeo ambao tumechagua kwa maisha yetu. Yesu anataka kuujenga ubinadamu na jamii mpya. Anaweza kufanya hivi peke yake, lakini anapendelea kutuhusisha ili tuwe na unyeti kama yeye alivyo na tuweze kuchukua vipaumbele vya utume wake. Nguvu ya neno la Yesu ilitokana na upako wa Roho Mtakatifu. Roho mmoja aliyemwongoza Yesu katika kazi yake anataka kutuongoza pia ili tuwe na uhusiano mpya na walio maskini na waliokataliwa kati yetu. Ufunuo wa Yesu ni hamasa ili tufanye tofauti maishani mwa watu wengi. Neema yake itusaidie tuwe vyombo vya wema na utunzaji maalum kwa walio na mahitaji mengi.
Fr Ndega

Mapitio: Sara

domingo, 17 de janeiro de 2016

UHUSIANO KATI YA MUNGU NA WATU WAKE UNAFANANA NA NDOA


Kutafakari kuhusu Isa 62: 1-5; 1Kor 12, 4-11; Yoh 2, 1-12

        Maadhimisho ya wakati wa kawaida ni mwaliko wa kuishi kwa hamu fumbo la imani yetu siku zote za maisha yetu. Liturujia siku hii ya leo aliongea kwamba hali ya ukombozi ambayo Waisraeli walihisi baada ya Utumwa wa Babeli ni matokeo ya uaminifu wa Mungu. Tangu Agano la Kale uhusiano kati ya Mungu na Watu wake unafananishwa na ndoa kati ya bwana na bibi arusi kama mwaliko wa uaminifu na ushuhuda. Mambo mengi makuu Mungu anayofanya kwa ajili ya watu wake ni alama ya utukufu wake na mwanga ambao unayalenga mataifa yote. Mfano wa Yerusalemu kama bibi arusi ni ishara ya hali mpya kabisa ambayo imetokea duniani kupitia kazi ya Kristo, aliye Bwana arusi wa watu wapya wa Mungu. Katika fumbo la uhusiano huu kila mtu anawezeshwa na Mungu atumikie wenzake. Kupitia njia tofauti tunamtumikia Bwana mmoja kwa msaada wa Roho wake ambaye anatupa vipaji vingi kwa wema wa wote.
        Katika injili Yesu amealikwa harusi pamoja na wanafunzi wake huko Kana. Mama yake pia yupo na anamwalika Yesu kuwasaidia maharusi wapya. Huu ni mwujiza wa kwanza wa Yesu, kulingana na toleo la Yohane. Katika andiko hili kuna mambo muhimu mengi kwa safari yetu ambayo tunataka kutafakari sasa. Kwanza kabisa, tukio harusi inaongea kuhusu kazi ya Yesu ambaye ni bwana arusi kwa namna ya ajabu. Yeye anafunga ndoa na ubinadamu, kuchukua ahadi ya kuwa mwaminifu milele. Harusi miongoni mwa wayahudi ilichukua muda mrefu wa siku nane. Ufikirie hali ya aibu kwa wanandoa ikiwa divai haitoshi kwa wote! Hakika si mwanzo mzuri kwa wale wawili ambao wana mipango mingi kwa maisha yao. Divai ni ishara ya furaha na sikukuu. Katika andiko hili ni alama ya Maagano mawili. Divai kukuu ni Agano la Kale hasa kuhusu sheria ambayo, Ingawa ilikuwa nzuri haikuwa inasababisha matokeo yaliyotarajiwa na Mungu kuhusu maisha ya watu wake. Divai hii haikutosha kama dhamana ya furaha milele. Walihitaji divai mpya.
     Maji iliyobadilika kuwa divai ni ishara ya kwanza ya nyakati mpya zilizoanzisha ulimwenguni kupitia Yesu. Yeye ni Bwana arusi na divai mpya, maana ya furaha milele kwa wote. Divai kukuu ilikuwa nzuri, divai hii mpya ni bora. Neno la bikira Maria ni msaada mkubwa katika kazi ya Yesu na hamasa katika maisha ya waliotenda kulingana na mapenzi ya Mwanawe. Yesu hatumii jina la mama yake bali alitaja cheo ambacho ni utambulisho kuhusu jukumu la mama yake katika mpango wa Mungu. Yeye alitaka kuonyesha heshima kwa mama yake na kumjulisha kama mfano kwetu. Katika Adamu na Awa, wanandoa wa kwanza wanadamu wote walifanya dhambi. Katika Yesu ubinadamu ni ulioumbwa tena na Maria ni Awa mpya. kama ilivyotokea kwa watumishi ambao walishika neno la Maria na kulitenda neno la Yesu, vivyo hivyo jukumu la mama Maria ni kutuongoza kwa Mwanawe. Yeye ni mfano wa ajabu wa kulishika na kutenda Neno la Mungu. Mariamu anatuambia kwamba kutii kwetu kwa Neno la Mungu kunampendeza. Mungu anafurahisha sana nasi.  

    Familia inampedeza Mungu ambaye, tangu mwanzo, alimpanga binadamu kwa mfano wake. Uumbaji wa wanadamu, wanaume na wanamke, ulikuwa mwaliko kwa kuishi katika familia. Ni mapenzi ya Mungu waweze kuwa wamoja, kupendana na kusaidiana. Mungu yupo katika familia na anatenda kazi kupitia Yesu. Yesu anapenda sana kushiriki katika maisha ya familia. Yeye alizaliwa katika familia moja na kutokana na makao ya Nazareti alibariki familia zote za ulimwengu. Uwepo wake ni ufanisi ili familia  zetu zifikie lengo lao kulingana na utambulisho asili. Kumheshimu Maria, mama yake, kunatusaidia kutambua uwepo na matendo ya Mwanawe katika familia ili ishinde hofu, changamoto, taabu na majaribio mengi, hasa majaribio ya uzinzi na talaka. Uwepo wa Yesu na Maria unaiweka wakfu familia kuifanya takatifu. Katika maneno mengine, familia ni mahali pa kumcha Mungu; basi, ni mahali patakatifu. Baba Mt. Yohane Paulo wa II alisema kwamba ni lazima kuiokoa familia. Nasi tunaweza kufanya hivyo hasa kwa kuziheshimu na kuzisaidia thamani ambazo tunaziishi katika familia na zinatufanya binadamu wa kweli.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

sábado, 9 de janeiro de 2016

“WEWE NI MWANANGU MPENDWA, NIMEPENDEZWA NAWE”


Kutafakari kuhusu Isa. 42:1-4, 6-7; Mdo. 10:34-38; Lk 3: 15-16, 21-22

        Tunasherehekea sikukuu ya ubatizo wa Bwana Wetu Yesu Kristo. Hii ni nafasi maalum ya kuukumbuka ubatizo wetu na kuweka upya ahadi ya kuwa wakristo, kuishi wito wetu wa wana wa Mungu kama Kristo alivyo. Yeye ni mtumishi wa Bwana, katika somo la kwanza, aliyeitwa awe “agano la watu na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.” Kulingana na kitabu cha Matendo, Yesu alifanya kazi njema kwa maisha ya watu kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. Vivyo hivyo ni maisha mapya ya sisi sote tuliobatizwa katika Kristo, yaani tunakuwa Kristo tena, kwendelea utume wake kwa manufaa ya Kanisa lake na wokovu wetu kwa sababu yeye yuko pamoja nasi. Tumshukuru Mungu kwa zawadi ya ubatizo wetu ulio ushiriki katika uhai wake.

       Injili inatusaidia kukumbuka kitu kuhusu Yohana na kazi yake. Ukuu wa Yohane ulikuwa kutambua ukuu wa Bwana, akijifikiria mwenyewe kama sauti tu na asiyestahili kuulegeza ukanda wa viatu vyake. Yesu mwenyewe alitambua ukuu wa Yohane akiweka unyenyekevu wake kama mfano kwa safari yetu. Yohana aliwabatiza watu kwa maji kama kielelezo cha kugeuka kwao. Kupitia ishara hii alitangaza huruma ya Mungu iliyopatikana kwa wote. Basi ishara ya Yohane ilikuwa kielelezo cha kupita kutoka katika dhambi na mauti kwenda katika neema na maisha mapya ya Mungu. Jambo muhimu katika tendo hili la Yohana ni kwamba aliwabatiza wale waliomhitaji Mungu na kutubu dhambi zao. Yohane na watu hao waliamini kwamba ni Mungu anayesamehe dhambi zao. Lakini Yesu hakuwa na dhambi, kwa nini alibatizwa?

      Kwa Yesu ilikuwa nafasi maalum ya kuonyesha mshikamano wake kuhusu kazi ya ajabu ya Yohana, kuthibisha kwamba Mungu anatarajia kwamba watu ambao ni wake warudi kwake. Kama inatokea katika somo la kwanza, kabla ya Yesu kuongea na watu kwa mamlaka aliyoipokea kutoka kwa Baba, Mungu mwenyewe alimjulisha akisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe”. Sauti hii itasikika tena katika tukio la milima. Huko milimani Mungu Baba alionyesha pendo lake kuhusu Mwanawe na kuwaalika wote wamsikilize. Yesu alionyesha pia unyenyekevu akijifananisha na binadamu ambaye ana udhaifu na kuhitaji kuishi katika ushirika na Mungu. Yesu alikuja si kuishi kujitengwa na watu bali aishi kuhusishwa katika safari yao. Kabla ya Yesu maji yalikuwa na nguvu ya kutakasa mwili pekee yake. Kutokana na uzoefu huu Yesu aliyatakasa maji ili yawe na nguvu ya kutakasa pia roho ya watu, yaani maji ya ubatizo.


      Baada ya kupokea ubatizo wa Yohana na kujulishwa kama Mwana mpendwa wa Mungu Yesu aliwezeshwa na Roho Mtakatifu ili aanze kazi yake akipendekeza uzoefu huu kwa wote ambao wanataka kuwa watoto wapendwa wa Mungu. Tunaweza kusema kwamba ubatizo ambao Yesu anapendekeza ni uwezo wa kushiriki katika uzoefu wake wa Mwana wa Mungu. Ubatizo huu ni ishara ya utambulisho wa kikristo, yaani Ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto, kulingana na maneno ya Yohane Mbatizaji. Ubatizo huu una nguvu ya kufanya mabadiliko katika maisha ya mtu yeyote kwa sababu unamfanya kuzaliwa katika familia ya Mungu. Alama yetu kama watoto wa Mungu haiwezi kufutika. Ipo daima! Tunaweza kuishi maisha mapya ambayo ni zawadi ya Kristo mwenyewe na matokeo ya utume wake. Ubatizo wetu, pamoja na maondoleo ya dhambi, unadhamini ushiriki katika uzima wa Mungu mwenyewe. Kupitia alama hii ya nje tunakufa kweli kwa maisha ya dhambi, na pia tunapitia ufufuko wa maisha mapya katika Kristo aliye mshindi dhidi ya dhambi na mauti. Yeye ni mwanga wa kweli ambao unamtia nuru kila mtu. Yeyote akimfuata hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya milele. Kupitia mwendo huu tumekuwa wana wa nuru ili tutembee katika mwanga wa Mungu kila siku ya maisha yetu. Ekaristi hii itusidie kuishi lengo hili la safari yetu ya kikristo, walio wana wapendwa wa Mungu.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

domingo, 3 de janeiro de 2016

YESU ANATAKA KUWA MWANGA WETU DAIMA


Kutafakari kuhusu Mt 2, 1-12

    Kidogo kidogo liturujia inatusaidia kufahamu maana ya kuzaliwa kwa Yesu. Yeye alizaliwa katika Bethelehemu iliyo nchi ya Wayahudi, lakini siyo kwa Wayahudi tu, bali kwa mataifa yote. Maelezo ya kuzaliwa kwake katika matoleo ya Mathayo na Luka yanadhihirisha kwamba tangu mwanzo wa maisha yake ya ubinadamu, alikuwa aliyekataliwa na nchi yake, lakini alitafutwa na kuheshimiwa na wale wasiyo Wayahudi. Hali hii ni uwazi sana pia katika injili ya Yohane (1,11-12), ingawa hakuna maelezo kuhusu utoto wa Yesu kama yapo katika injili zingine mbili. Kulingana na Yohane, Yesu “alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu.” Basi, Yesu alikuja kwa wanadamu wote na akawaangazia wote kupitia mwanga wake. Kuzaliwa kwake kutuhakikishia kwamba wote wanaweza kuwa watoto wa Mungu na kwamba ni mapenzi ya Mungu kuwaokoa wote.

      Habari ya kuzaliwa kwa Yesu ingekuwa njema kwa wote, lakini makaribisho yalikuwa tofauti miongoni mwa watu. Hii ilikuwa habari ya furaha kubwa kwa upande wa walio na mioyo makini kuhusu ishara za ukaribu wa Mungu na walikuwa tayari kumkaribisha daima, kama ilivyotokea na wachungaji. Lakini kwa wenye nguvu hii ilikuwa habari mbaya kwa sababu iliwaalika kutafuta thamani za kweli. walijihisi kufadhaika na kutishiwa kwa sababu hawakutaka kuacha mawazo yao na walikuwa na hofu ya kupoteza msimamo na upendeleo wao. Kwa upande wa Wageni waliotoka Mashariki habari hii iliwaletea maana ya kweli kwa maisha yao; kwa hivyo walimtafuta mfalme mpya kwa hamu sana. Makaribisho haya kwa njia tofauti yalitajwa pia katika utabiri wa Simeoni hekaluni, “Mtoto huyo atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli (Lk 2,34).

     Kulingana na injili Wageni walikuwa mamajusi; basi, si hakika kwamba walikuwa wafalme wala watatu. Lakini tangu wakati wa Wakristo wa kwanza kuna utamaduni mmoja ambao umeufuata utabiri wa nabii Isaya (60,3) ambao unasema, “Mataifa yataujia mwanga wako, wafalme waujia mwanga wa pambazuko lako.” Kuhusu nambari ya mamajusi haya, tunadhani kwamba wangekuwa watatu kwa sababu ya nambari ya zawadi ambazo walimtolea Yesu, yaani, dhahabu na uvumba na manemane.” Lakini Ishara muhimu katika andiko hili ni Nyota. Hii inamaanisha mwanga wa Mungu uliowaangazia watu ili wamtafute yeye kwa hamu. Mwanga huu ni Mwanawe mwenyewe ambaye mtu yeyote akimfuata hatatembea gizani (Yoh 8,12). Mamajusi waliacha nchi zao na kuruhusu kuongozwa na nyota hii ili wafikie mwelekeo kamili wa maisha yao. Mamajusi walithamini nyota. Hivyo, kuona nyota tunahitaji moyo wa kuthamini.


      Siku ya leo Mungu anatualika kuwa macho kuhusu nyota anayotumia kutuongoza. Je, umegundua nyota ambayo inatoa maana ya kweli kwa maisha yako? Katika injili zote tunaweza kukuta ishara nyingi za nyota hii. Tuchukue mfano wa wavuvi waliovua samaki wengi; kwao samaki walikuwa ni nyota ya Yesu. Kwa wakulima mbegu ulikuwa nyota ya Yesu. Kwa wanaharusi huko Kana divai ni nyota ya Yesu kwa sababu muujiza wa maji kubadilika na kuwa divai ulimtangaza Yesu. Kwa mwanamke aliyekuwa anachota maji nyota ya Yesu ilikuwa ni maji. Kwa Petro aliyemkana Yesu aliandaa moto na kuweka samaki moto ukawa nyota ya kumrudisha Petro kwa Yesu. Kwa wafuasi wake  wa Emmaus waliokata tamaa, nyota yake ulikuwa ni mkate. Walimtambua katika kuumega mkate. Kama mamajusi, maisha yetu ni safari ya imani tukutane na Mungu na kuruhusu aweze kuzibadilisha njia zetu. Tunaalikwa kuacha baadhi ya mawazo na usalama usio kweli na kuanza safari yetu walioongozwa na msukumo Mungu. Kwake tunaalikwa kujitoa muhimu sana ya maisha yetu kwa maana yeye anastahili. Zawadi ambazo tunaweza kuzitoa zinatokana na ukarimu wake mwenyewe. Huyo Yesu ambaye tunatambua katika uzoefu wetu wa ndugu anataka kuwa mwanga wetu daima ili tutafute thamani za kweli na kukuta maana ya kweli kwa maisha yetu.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

sexta-feira, 1 de janeiro de 2016

BIKIRA MARIA NI MAMA WA MUNGU


Kutafakari kuhusu Lk 2, 16-21

Katika hali hii ya furaha na shukrani ya krismasi, tunaalikwa kusherehekea sikukuu ya Bikira Maria kama Mama wa Mungu. Yeye ni Mama wa Mungu kwa sababu ni Mama wa Yesu aliye Mwana wa Mungu na, kwa hivyo, ndiye Mungu. Maria ni mfano maalum katika safari yetu ya kikristu. Yeye ni kielelezo cha jibu letu kwa Mungu na mfano wa mafanikio ya Kanisa kama mama wa wote ambao wanamfuata Mwana wake. Ukweli wa Maria Mama wa Mungu uliheshimiwa na wakristo wa Kwanza tangu mwanzo wa safari yao, lakini ulitangazwa na Kanisa tu kupitia Mtaguso wa Efeso katika mwaka wa 431. Yeye ni kama kioo kwa ubinadamu wetu, yaani, tunapomwangalia tunajiona wenyewe vizuri. Siku hii pia ni nafasi nzuri kumshukuru Mungu kwa mwaka huu unaoisha na kumjulisha matarajio yetu kuhusu mwaka mpya hasa matarajio ya amani katika ushirika na watu wote wa dunia nzima kwa sababu leo ni siku ya amani.   
Katika Yesu, aliyezaliwa Bethlehemu, Mungu anaonyesha upendo wake mkuu kwetu, kufanya makao kati yetu na kutuletea wokovu. Wokovu ni kazi ya Mungu, lakini unatokea duniani na ushiriki wa binadamu, hasa wa Bikira Maria, aliyechaguliwa awe Mama wa Mwana wa Mungu. Mariamu alikubali kazi hii kwa upendo mkubwa na, kabla ya kuzaa Yesu katika tumbo lake, alimzaa moyoni mwake. Kama mwanamke mwangalifu, alikuwa makini sana kwa hali ya dunia na mahitaji ya wokovu kwa wanadamu wote. Aliikataa mipango yake binafsi kama kijana ili aishi mpango wa wokovu wa Mungu. Mariamu alipata kutenda wito wake kwa kulisikiliza na kulishika Neno la Mungu kwa njia ya ukimya, kuwa macho na kutafakari daima. Vile vile, alipata kuzitambua na kuzikubali ishara za huruma ya Mungu katika safari ya watu wake, kulingana na maneno haya ya Luka, “Bikira Maria aliyaweka maneno hayo yote, akiyatafakari moyoni mwake.” Mwendo huu uliwezekana kwa sababu moyo wake ulikuwa makao ya Mungu daima.
Bikira Maria aliandaliwa na Mungu ili awe mtumishi wake na, katika mwendo huu, akasaidiwa na neema yake Mungu. Hali hii ilimfanya Bikira Maria aliyefunguliwa kabisa kwa msukumo na mapitio ya Mungu. Tangazo la Malaika Gabrieli lilikuwa wakati wa maamuzi wa jibu lake. Ingawa Mungu aliamua kuiokoa dunia kupitia Mwana wake wa pekee, alitaka ushiriki wa Bikira Maria ambaye alikubali. Mariamu alikuwa mshirika mwaminifu wa Mungu kwa kazi ya wokovu. Katika udogo na unyenyekevu wake tunaweza kutambua ukuu wake, kulingana na maneno yake mwenyewe: “Mungu amemwangalia mtumishi wake katika unyenyekevu wake; watu wote wataniita mbarikiwa”. Maisha na chaguzi za Mariamu ni tangazo kubwa la makuu ya Mungu. Kulingana na maisha yake, yeyote aliyeamini katika ahadi za Mungu ni mwenye furaha, kwa sababu Yule aliyeahidi ni mwaminifu. Imani inakuwa kipimo cha msingi wa furaha.
Kama mama wa Yesu, Maria ni mmoja wetu ambaye ana ushiriki maalum katika fumbo la wokovu wetu. Yeye anakuwa ishara ya ubinadamu mpya, uliobadilishwa na kuokolewa na Mwanae. Kama hii, alimsaidia Mungu awe mmoja wetu, akichukua hali halisi yetu ya binadamu na kulitoa pendekezo mpya la maisha. Kwa njia ya Bikira Maria Mungu anaendelea kutenda makuu ulimwenguni. Kupitia jibu lake la ukarimu, Mariamu aliutoa uhai ulimwenguni. Jukumu lake lina maana pamoja na utume wa Mwanawe Yesu. Kama mwanafunzi aliandamana na utume wa mwanawe kwa uaminifu hadi matokeo upeo. Yeye anajua jinsi ya kupenda na jinsi ya kuteseka kwa ajili ya yule anayependa. Ukarimu na upatikanaji wake kama mtumishi wa Mungu unatuhamasisha katika majibu yetu ya kila siku kwa mapitio yake. Kulingana na Mariamu, jibu letu kwa Mungu linapaswa kuwa alama ya ukarimu na upatikanaji. Mfano wa Bikira Maria uwe mwaliko kwetu ili tupende Mwana wake kwa uhusiano wa ndani na kumsaidia kupitia utumishi wa ukarimu na unyenyekevu. Tukikaribisha pia mfano wa wachungaji tuwe tayari kukutana na Mungu na kumtambua katika hali zote. Kutokana na  mkutano huu tuwe vyombo vya amani katika mahali popote tuendapo.

Fr Ndega

Mapitio: Sara