Kutafakari kuhusu Yer 1, 4-5. 17-19; 1Kor 12,31. 13,1-13; Lk 4, 21-30
Liturjia ya jumapili hii inaongea kuhusu umuhimu na
hatari za unabii. Kwa kuchukua kazi hii ngumu ni lazima ujasiri na utayari,
hasa katika mazingira magumu kama yale ya Yeremia na Yesu. Somo la kwanza
anasimulia wito wa Yeremia kama historia ya upendo. Mungu mwenyewe anamwita ili
awe mjumbe wake. Mungu anajua kuhusu ugumu na udhaifu wa Yeremia na, kwa hivyo,
anaahidi utunzaji na ulinzi. Wito wa Yeremia ni matokeo ya uzoefu wa Neno la Mungu
ambalo linampa uwezo wa kuongea na kushauri kwa jina la Bwana. Nabi wa kweli
hasemi katika jina lake mwenyewe, bali asema tu yale ambayo Bwana anamwamuru
kusema. Kulingana na somo la pili msingi wa uzoefu wa binadamu ni upendo.
Upendo lazima kuwa hamasa ya matendo yetu kwa sababu bila upendo kila kitu
tunachofanya ni bila maana. Kama sisi ni manabii tangu ubatizo, wito wetu ni pia historia ya upendo na mafanikio katika safari yetu inawezekana tu kupitia
upendo. Upendo ni maana ya utambulisho wetu kama wakristo.
Kulingana na kutafakari kwetu kuhusu injili ya jumapili
iliyopita, Yesu alienda kijijini
mwake Nazareti na kutangaza Neno la Mungu kama mpango wake wa
maisha. Watu walishangazwa sana kwa sababu ya maneno ya neema yaliyotoka
kinywani mwake. Kwa kweli Yesu aliishi kwa furaha
na shauku utambulisho wake kama aliyechaguliwa
na Mungu ili atangaze mpango wa upendo
na wokovu wake. Uzoefu wake miongoni mwa wenzake ungalikuwa mzuri ikiwa Yesu angalisema
tu yale ambayo walitaka kusikiliza. Lakini Yesu hana hofu na neno la Mungu
halina mipaka. Aliwapendekezea njia mpya ya maisha na mabadiliko ya mawazo.
Pendekezo la Yesu si ngumu; yeye anatarajia tabia tofauti tu. Hii ndiyo ni
maana ya umwingilio wao/kukasirika kwao. Mara nyingi maneno ya Yesu
yalisababisha mabadiliko maishani mwa watu wengi kwa sababu maneno yake yana
nguvu yenyewe. Kwa hivyo alipata wafuasi wengi. Ikiwa mabadiliko yaliyotarajiwa
hayatokei kwa baadhi ya watu, shida siyo kwa upande wa Yesu.
Watu wa kijiji cha Yesu walijua kila kitu kumhusu yeye na walitumia hiki
kama kipimo cha hukumu au utambuzi. Kujua kwao kwa awali kumhusu Yesu
kuliwazuia kumjua nani ndiye. Yesu kama
wokovu wa Mungu, ndiye utimizaji
wa maandiko, lakini alikataliwa na wale wanajiona
waliojua maandiko. Labda walikuwa na mazoea ya kukubali tu yale yaliyokuwa
rahisi kwao, wakirekebisha Neno
la Mungu kulingana na njia yao ya
maisha, bila kuwa tayari ya
kuishi kwa mapitio yanayotokana na Neno hili. Walimkataa
Yesu kwa sababu walijifunga kwa upya wa Mungu uliodhihirishwa na Mwana wake.
Ilikuwa ngumu sana kwao kufahamu kwamba ingawa Yesu alikuwa mwana wa Yosufu
ndiye Mungu kweli. Je! Kujua kwetu kuhusu Yesu kumetusaidia kukua katika imani
na kuimarisha uhusiano wetu naye?
Wakati Yesu alichukua hali yetu ya binadamu, alijitambulisha na hali hii,
lakini akatambua pia kwamba vitu vingi vilipaswa kubadilika. Kwa hivyo
alijulisha pendekezo mpya la maisha. Kwa upande wetu, kuishi kwa uhusiano wa
kweli na Yesu hautoshi mshangao mbele ya hekima ya maneno yake kama wenzake
walivyo, bali tunapaswa kuruhusu kwamba ujumbe wake wa upendo na ahadi uwe hai
ndai yetu. Kama watu kutoka Nazareti, mara nyingi sisi pia tumelipinga Neno la Yesu ambalo linauliza
maswali kuhusu tabia na matendo yetu ya
kila siku. Kushiriki katika utume wa Yesu ni kuchukua pamoja naye hali ya
wengine, hasa watu maskini.
Hatuwezi kufikiri kwamba habari tumepokea kuhusu Yesu yatosha
kwa safari yetu ya wito. Ni muhimu kuruhusu kwamba yeye mwenyewe ajidhihirishe
kwetu kwa nguvu yote ya upendo
wake siku zote za maisha yetu. Kama ilivyotokea na Yesu, sisi pia
tunapaswa kuwa watu ambao wanalenga mapendekezo ya Neno la Mungu. Turuhusu
kwamba maneno haya yatuongoze ili tufanye mapenzi ya Mungu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário