domingo, 24 de janeiro de 2016

MJUMBE WA HABARI NJEMA KWA MASKINI NA WALIOKATALIWA NA JAMII


Kutafakari kuhusu Lk 1, 1-4: 4,14-21

        Liturujia ya jumapili hii inaongea kuhusu umuhimu wa Neno la Mungu ambalo lazima kusikika kwa heshima na kutangazwa kwa shauku. Neno hili ni alama ya upendo na utunzaji wa Mungu kwa watu ambao ni mali yake. Katika somo la kwanza, Ezra aliitangaza Torati ambayo ni Neno la Mungu kwa Waisraeli. Watu walisikiliza kwa uangalifu na kujibu kwa utayari. Neno la Bwana ni faraja na kutia moyo. Hili Neno ni maana ya furaha ambaye inakuja kutoka kwa Bwana na kuitoa nguvu kwa watu wote. Kupitia Neno la Mungu watu wanakumbuka mambo makuu ambayo yaliwapa maana ya utambulisho kama Watu wa Mungu. Ni mwaliko wa kumsifu Mungu kwa sababu ya uaminifu wake na kufanya upya ahadi yao ya waruhusu kuongozwa na Mungu ambaye anaongea kuzionyesha njia za uzima na ukombozi. Kama Watu wa Agano la Kale waliokusanyika kama mtu moja kwa sababu ya Neno la Mungu, vivyo hivyo ni uzoefu wetu kama washiriki wa mwili wa Kristo, yaani ingawa sisi ni wengi, tulibatizwa kuwa mwili mmoja. Karama mbalimbali ambazo tumepokea ni kwa ajili ya manufaa ya mwili mmoja huu.
Sehemu ya kwanza ya injili inaongea kwamba habari njema ya Kristo iliwazaa mashahidi wengi. Imani yetu ni matokeo ya uzoefu, yaani uzoefu ambao tumepokea kutoka kwa waliotutangulia na uzoefu wa kutafuta binafisi. Maisha ya wale waliotutangulia yanaendelea kushuhudia kwamba bila uzoefu imani yetu katika Kristo ni haba. Mwinjilisti Luka analitoa andiko lake kwa heshima ya mtu fulani aliyeitwa Theofilo, kwa sababu katika karne ya kwanza yalikuwa mazoea kufanya hivyo. “Theofilo alikuwa mtu wa maana aliyesifika katika jamii ya Wapagani, aliye kuwa Mkristo kutokana na mahubiri ya mitume.” Maana ya neno Theofilo ni “mpendwa wa Mungu”. Kama haya ni matokeo ya uzoefu wetu wa Neno la Mungu, yaani tunakuwa wapendwa. Sehemu ya pili ni kuhusu uzoefu wa Yesu mjini mwake Nazareti, mahali alipolelewa. Alienda huko akiongozwa na Roho Mtakatifu na kutangaza kwa shauku Neno la Mungu kama mpango wake kwa watu waliotarajia ufunuo wa Masiya kwa hamu sana.
Yesu alichagua wakati wa liturujia kwa kutangaza kipaumbele cha kazi yake. Anajihisi aliyetiwa mafuta na kutumwa na Roho ili atangaze habari njema kwa maskini na ukombozi kwa wanaoonewa; yeye anaweza kuyafufua matumaini yao na kuwarudishia furaha ya maisha yao. Hali hizi ni maana ya utambulisho wa Yesu na sehemu ya mpango wa upendo na wokovu wa Baba yake. Kipaumbele cha Yesu ni kipaumbele cha Mungu. Basi, tunaweza kuwaza furaha kubwa imo ndani ya Yesu kwa sababu ya njia hii ya Mungu ya kutenda. Mungu anapenda kila mtu na kutaka kuwafikia wote kwa upendo wake. Lakini kuna baadhi ya watu ambao wanahitaji utunzaji maalum, kwa sababu wanakataliwa na jamii. Mungu anatudai kuwa macho kwa hali hii. 
Katika Yesu wakati wa neema na wokovu unaanza. Yesu ni mkombozi ambaye alikuja kuwaweka huru wanadamu wote waliopoteza uhuru wao kwa sababu ya dhambi. Ukombozi ambao Yesu anatangaza ni zaidi kuliko hali ya roho iliyosababishwa na dhambi. Anataka kuifikia jamii kabisa, kwa sababu hali hii ina mawazo kinyume na mpango wa Mungu uliodhihirishwa na Yesu. Kama inavyotokea katika kifungu kingine (k.m. Mathayo) hii ni sehemu ya tangazo la Ufalme wa Mungu ambalo linalihusu pendekezo la mabadiliko. Sisi sote pamoja na jamii nzima tunapaswa kufikiri vizuri kuhusu mwelekeo ambao tumechagua kwa maisha yetu. Yesu anataka kuujenga ubinadamu na jamii mpya. Anaweza kufanya hivi peke yake, lakini anapendelea kutuhusisha ili tuwe na unyeti kama yeye alivyo na tuweze kuchukua vipaumbele vya utume wake. Nguvu ya neno la Yesu ilitokana na upako wa Roho Mtakatifu. Roho mmoja aliyemwongoza Yesu katika kazi yake anataka kutuongoza pia ili tuwe na uhusiano mpya na walio maskini na waliokataliwa kati yetu. Ufunuo wa Yesu ni hamasa ili tufanye tofauti maishani mwa watu wengi. Neema yake itusaidie tuwe vyombo vya wema na utunzaji maalum kwa walio na mahitaji mengi.
Fr Ndega

Mapitio: Sara

Nenhum comentário: