domingo, 29 de novembro de 2015

KUWA MACHO KWA KUJA KWAKE MWANA WA MTU


Kutafakari kuhusu Lk 21, 25-28, 34-36

   Tumeanza wakati mpya katika liturujia ya kanisa uitwao Majilio. Wakati huu unayahamasisha matumaini yetu katika matarajio ya Kuja kwake Bwana mara ya pili katika mwisho wa nyakati na unakumbuka pia Kuja kwake kwa kwanza, kutuandaa tusherehekee sikukuu ya kuzaliwa kwake katika Krismasi. Basi, Liturujia ya msimu huu ni mwaliko kwa kukesha ili tutambue na kuzikaribisha ishara za uwepo wa Bwana katika hali yetu ya kila siku. Ni mwaliko pia kwa shukrani kwa sababu Bwana anakuja daima kukutana na sisi, kutupa wokovu wake. Matukio yote makuu yanahitaji maandalizi mazuri ili yaweze kusherehekewa vizuri. Kama hii ni Majilio kwa uhusiano na tukio kubwa la Krismasi.

         Mwanzoni mwa sura ya kumi na tatu ya injili ya Luka Yesu anaongea kuhusu uharibifu wa Yerusalemu. Ufunuo huu uliwahamasisha baadhi ya wanafunzi wake wamwulize swali kuhusu ishara gani, siku na saa gani ya uharibifu huu. Yesu anatumia nafasi hii kutabiri kuhusu mambo mengi akiiandaa mioyo ya wafuasi wake kwa wakati ujao. Aliwaambia kuhusu ishara nyingi mbinguni, taabu, mateso, dhiki kuu na kuja kwake, kulingana na unabii wa Danieli, yaani, juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi. Kanisa katoliki hutafsiri tukio hili kama kuja kwake Yesu mara ya Pili ili kuwahukumu wazima na wafu. Hiyo ndiyo imani yetu ambayo sisi hutangaza kila jumapili. Kuhusu siku na saa hii hakuna mtu ajuaye. Hii ni sehemu ya mpango wa hekima na wema wa Baba. Kwa hivyo huu ni pia mwaliko kwa kukesha.

        Ingawa uharibifu wa mji wa Yerusalemu ulitokea katika mwaka wa 70 B.K., nia ya Yesu haikuwa kuwajulisha kuhusu tukio hili, bali kuhusu matokeo ya tukio hili katika maisha ya wafuasi wake. Alitabiri kwamba “nguvu za mbingu zitatikiswa” akifikiria imani na ushuhuda wa wanafunzi wake kama nguvu za mbingu zipo ulimwenguni. Wanafunzi wa Yesu wataishi kipindi cha machafuko na watajaribiwa kuiacha imani katika Kristo na kukata tamaa kuhusu utambulisho wao wa wanafunzi kwa sababu ya matusi, majaribio, matatizo na mateso mengi. Ilionekana kwamba walikuwa peke yao mbele ya machafuko hayo yote. Lakini Yesu mwenyewe alikuwa amewaahidi uwepo wake daima kupitia maneno haya, “mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamiliifu wa dahari.” Maneno haya ni mwaliko kwa ushuhuda na kusali kama njia ya kukesha. Hao wana jukumu la kuendelea utume wa Mwalimu, wakiwa makini kwa ishara za kuja kwake ili akutane nao na kuwatuza kwa maana ya uaminifu wao.

Andiko hili linatuambia kwamba Kristo ni mshindi na ujio wake unaanzisha wakati mpya anaoshiriki na wanafunzi wote wanaobaki wamesimama na kuinua vichwa vyao kupitia imani na ushuhuda kwa uaminifu. Tunapaswa kuishi imani yetu ya kikristo kwa uhusiano na kila kitu ambacho kinatokea kandokando yetu. Jamii inatarajia imani yenye maana na iwe jibu kwa hali iliyopo na binadamu anayoiishi. Je, imani yetu ni gani? “Je, tena wakristo wanapaswa kuwa na tabia gani wakati wa mazingira magumu? Kama aliwaambia wafuasi wake wa zamani, Yesu anatuhakikishia kuwa mazingira magumu ni sehemu ya safari ya wale ambao wanamfuata katika nyakati zote, lakini Yeye anatukumbusha pia kwamba ni katika machafuko haya ya dunia hii tunapojiandaa kukutana naye mwishoni mwa maisha yetu binafsi hapa duniani. Kwa hivyo kila hatua ya safari yetu ni maandalizi kwa mkutano wa mwisho na Bwana wetu.


         Liturjia linataka kuimarisha imani yetu na kufufua tumaini letu kwa tendo la wokovu wa Mungu ndiye mkuu katika nyakati zote, zilizopita na zijazo. Hali hii inatualika kuishi wito wetu wa wafuasi kwa uaminifu katika nyakati zote pia, hata wakati wa mateso makali. Baada ya machafuko yote tutakuwa washindi pamoja na Bwana wetu mshindi. Kulingana na mithali fulani, “hakuna usiku hata wa muda mrefu pasipo mapambazuko”. Basi, kwa wale wanaomfuata Kristo, mazingira magumu si ishara za mwisho wa nyakati bali ni wakati mpya, wakati wa kuishi wito wetu kwa shauku zaidi, furaha na tumaini, kuushuhudia kwa uaminifu uwepo wa Bwana miongoni mwetu. Anakuja kwa upendo na kutuokoa. Tukaribishe ishara za nyakati kama msaada tutambue uwepo wa Bwana na kuishi mafundisho yake kwa njia mpya.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

quarta-feira, 25 de novembro de 2015

UFALME WA YESU NI TOFAUTI KABISA


Kutafakari kuhusu Yoh 18, 33-37

            Tunasherehekea sikuku ya Bwana Wetu Yesu Kristu Mfalme. Yeye ni Mfalme wa mbingu na dunia; enzi na utawala wote ni wake. Liturjia hii inatualika kumfuata Mfalme huyo ambaye ni njia, ukweli na uzima. Kuutafuta kwanza ufalme wake ni maana ya kweli ya maisha yetu.

Mbele ya Pilato, Yesu hakukanusha juu ya ufalme wake,  bali anafafanua zaidi maana ya ufalme huo. Swali la Pilato kwa Yesu ya kwamba: “Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?”, lilikuwa limewaza kuwa Yesu alikuwa mmoja wa wazalendo ambaye alitaka kuupindua utawala wa Roma na kuanzisha utawala mpya wa kisiasa kwa wayahudi. Wayahudi wengine walitumaini kuwa Masiha angewarudishia tena utawala wa Daudi. Wote, Pilato na Wayahudi, wana wazo ambalo sio kamili kuhusu ufalme wa mbinguni na kuhusu pia Yule aliyechaguliwa na Mungu adhihirishe ufalme huu. Yesu anakubali kuwa yeye ni mfalme, lakini siyo mfalme wa wayahudi tu. Yeye ni Mfalme wa wote na Ufalme wake ni tofauti. Kumbe ufalme wa Yesu si wa dunia hii lakini unawahusu wote waishio hapa duniani.

      Ufalme ni mapenzi ya Mungu ambayo Yesu aliishi na ufalme huu ni pia hali mpya aliyoanzisha ulimwenguni. Uwepo wake unaanzisha wakati mpya, yaani, wakati wa wokovu wa Mungu. Msingi wa ujumbe wa Yesu ni tangazo la wokovu wa Mungu ambalo ni sawa na tangazo la ufalme pia. Kwa kweli Yesu hajitangazi mwenyewe, bali anautangaza Ufalme. Katika Yesu mwenywe ufalme ulikuwa hali halisi ukisababisha mabadiliko ulimwenguni kwa wema wa wote hasa kwa walio na mahitaji mengi, yaani, wagonjwa wanapona, bubu wanaongea tena, vipofu wanapata kuona tena, maskini wanaipokea habari njema na wenye dhambi wanaondolewa dhambi zao. Kuna wengi ambao wanalitambua tendo la wokovu wa Mungu katika ishara za ukombozi za Yesu na wanajiruhusu kubadilishwa, lakini kuna wengine pia ambao wanajifunga wenyewe na hawawezi kutambua kile ambacho kinatokea kandokando yao. Upinzani dhidi ya Yesu ni upinzani dhidi ya mafanikio ya Ufalme wa Mungu. Katika maana hii ni ngumu sana kumfuata nyayo zake na kutangaza ufalme wake.

        Sio kwa Pilato tu, bali kwa wengine pia ilikuwa ngumu kufahamu kwamba Ufalme wa Yesu ni tofauti na wa dunia hii. Ufalme wake ni wa kuushuhudia ukweli na kuwaongoza watu katika njia ya kweli. Ufalme ambao Yesu anatangaza upo ndani yake na unaonyeshwa kupitia matendo yake miongoni mwa watu. Yesu hakufasili Ufalme lakini aliuonyesha upo ulimwenguni kupitia ishara nyingi. Hii si hali kwa kutazama bali kwa kuhisi na kutangaza. Hili ni fumbo la imani. Ingawa hatuna ufafanuzi kuhusu ufalme kutokana na injili, ibada ya Ekaristi ya siku hii inatujulisha baadhi ya thamani ambazo zina uhusiano wa ndani na ufalme ambao Yesu alikuja kutangaza, yaani, “Huu ni ufalme wa milele na ulimwengu wote, ufalme wa kweli na uzima, ufalme wa utakatifu na wa neema, ufalme wa haki, mapendo na amani.”


        Ni lazima kuwa makini sana kwa ishara za ufalme huu, kwa sababu, ingawa ufalme huu ni hali inayochanganyika na hali za binadamu, zipo ishara nyingi zinazoonekana kuwa wa Ufalme wa Mungu, lakini zinaweza kutudanganya. Yesu ni ishara ya ufalme kwa namna ya ajabu. Hatuhitaji nyingine. Msingi wa ufalme wa Yesu ni ushuhuda katika kweli unaoweza kubadili maisha ya watu, ikiwa tumkubali. Tunapomkubali Yesu na kumsikiliza na kisha kumruhusu awe kiongozi wa maisha yetu, tutakuwa tukiishi katika kweli. Kila aliye wa hiyo kweli humsikia sauti ya Yesu anayesema kuamba ndiye njia, ukweli na uzima. Ukweli huu utawapeni uhuru. Ufalme wa Yesu hupingana na uongo, uonevu na ukandamizaji na kila namna. Ufalme wa Yesu hautokani na nguvu au vita. Hivyo kila mmoja wetu ni budi aisikie sauti ya ukweli na kuamua kwa hiari yake kuifuata. Tuchukue pamoja na Mtakatifu Yohana Calabria ahadi ya kutafuta kwanza Ufalme wa Mungu kuiimarisha imani duniani katika Mungu Baba Mtoaji.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

quarta-feira, 18 de novembro de 2015

WAKATI WA MAZINGIRA MAGUMU

Kutafakari kuhusu Dan 12: 1-3; Heb 10: 11-14; Mk 13: 24-32

Tunaweza kuanza kutafakari huku kujiuliza maswali sisi wenyewe: “Je, wakristo wanapaswa kuwa na tabia gani wakati wa mazingira magumu? Liturgia hii ni hamasa Kwetu ambao tunaalikwa kuishi imani yetu katika Kristo kama maana ya utambulisho. Kwa sisi ujumbe kuhusu miisho ya nyakati si ishara kwa kukata tamaa, bali mwaliko kwa tumaini. 

Somo la kwanza kutokana na kitabu cha nabii Danieli ni ufunuo kuhusu hukumu na ufufuko. Ni mara ya kwanza ambayo tangazo la ufufuko linaonekana katika biblia kabla ya Kristo. Watu wa Israeli walitumwa na wagiriki na kuteseka sana. Wengi miongoni mwao waliacha kumwamini Mungu, lakini wengine waliendelea katika imani yao kwa uvumilivu. Kwao Mungu alituma malaika Mikaeli awalinde na kuwahamasisha wakabili wakati wa taabu bila kukata tamaa. Uwepo wa malaika Mikaeli ni dhamana ya ukombozi na ufufuko kwa wale ambao walikuwa waaminifu kutenda mema hadi upeo. Kulingana na somo la pili sadaka ya Kristo ilishinda sadaka za makuhani wa Agano la Kale kwa sababu sadaka zao zilikuwa hafifu, haba na hazikuweza kuondolea dhambi za watu wote. Lakini sadaka ya Kristo iliyotolewa mara moja tu iliweza kuwatakasa watu wote kwa nyakati zote. Katika kila misa takatifu tunasherehekea fumbo la sadaka hii, kuuhisi na kuusaidia wokovu wa Kristo kwa wote. Ni Kristo mwenyewe ambaye anatuhusisha katika mwendo huu.

         Mwanzoni mwa sura ya kumi na tatu ya injili hii ya leo Yesu anasema kuhusu uharibifu wa Yerusalemu. Ufunuo huu uliwahamasisha baadhi ya wanafunzi wake wamwulize swali kuhusu ishara gani, siku na saa gani ya uharibifu huu. Yesu anatumia nafasi hii kuongelea mambo mengi ambayo yatatokea baadaye ili kuiandaa mioyo ya wafuasi wake, ni kwamba, ishara nyingi mbinguni, taabu, mateso, dhiki kuu na kuja kwake kulingana na unabii wa Danieli, yaani, juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi. Kanisa katoliki hutafsiri tukio hili kama kuja kwake Yesu mara ya Pili ili kuwahukumia wazima na wafu. Hiyo ndiyo imani yetu ambayo sisi hutangaza kila jumapili. Kuhusu “Siku ya Bwana”, katika Agano la Kale manabii walikwisha wajulisha Waisraeli kuwa siku hii haingekuwa ya adhabu kwa mataifa mengine tu, bali pia kwa Waisraeli kwa kutokuwa waaminifu katika agano walilolifanya na Mungu. Kuhusu siku na saa hii hakuna mtu ajuaye. Hii ni sehemu ya mpango wa hekima na wema wa Baba. Kwa hivyo huu ni pia mwaliko kwa kukesha. Kwa wale ambao wanamfuata Yesu, kukesha lazima kuwa tabia daima kwa sababu ikiwa tunamjua mwalimu wetu, tutakuwa tayari daima ili kumkaribisha.


    Katika utume wake, Yesu aliwaonya wafuasi wake kuwa, mwisho wa nyakati utatanguliwa na matukio mengi magumu, lakini Yesu hataki kutuogopesha. Anatuambia tutarajie kuja kwa pili kwa mwana wa mtu atayekuja kuwachukua wana wa Mungu. Lengo ni kuimarisha imani yetu na kufufua tumaini letu kwa tendo la Mungu ndiye mkuu katika nyakati zote, zilizopita na zijazo. Anatufundisha kuishi wito wetu wa wafuasi kwa uaminifu katika wakati zote pia, hata wakati wa mateso makali. Ushuhuda wa Yesu ni kwamba Mungu huingia katika historia yetu kwa upendo na anajionyesha tofauti kabisa nasi na hata historia yake ni tofauti na yetu.  Baada ya majaribu yote Mungu atakuwa ndiye mshindi. Ni mwaliko tuwe na imani kwa Mungu na kuacha kutabiri mambo, kushinda hofu na mashaka yote. Kulingana na mithali fulani, “hakuna usiku hata wa muda mrefu pasipo mapambazuko”. Basi, kwa wale ambao wanamfuata Kristo, mazingira magumu si ishara za mwisho wa nyakati bali ni wakati mpya, wakati wa kuishi wito wetu kwa shauku zaidi, furaha na tumaini, kuushuhudia kwa uaminifu uwepo wa Bwana miongoni mwetu. Anakuja kwa upendo na kutuokoa. Tukaribishe ishara za nyakati kama msaada tutambue uwepo wa Bwana na kuishi mafundisho yake kwa njia mpya. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara

segunda-feira, 2 de novembro de 2015

THE DEATH OF CHRIST IS ALREADY OUR VICTORY

Reflection from John 11: 11-27

When we celebrate the life, we celebrate a great mystery, a precious gift which comes from God. In Christ this gift receives a character of fullness and it is through him that we can understand that the life doesn’t finish here in this world. The inheritance of life of the people who advanced us has a great value for us who are called to continue in the faith to live with meaning. If we cannot see any more the people who advanced us, the true values lived and left by them are the evidence that their passage among us wasn’t in vain. Saint John Calabria used to say: “If we have God in us, we shall do the good only with our passing”. Celebrating the dead is fraternal manifestation of our recognition of how they continue being important for us all, because the death is not an absolute end; it only concludes one stage of the life.  In moments of sorrow, of sadness and nostalgia, let ourselves be helped by the prayers of the friends and enlightened by the Word of God, which strengthen us in the faith and commit us in the life.

As Christians, our main characteristic is the hope. Thus expresses S. Paul: “If Christ didn’t rise our faith is vain and our hope is without sense”. The God in whose we believe is the God of life and when gave the life to us he bound us to himself, making us his beloved sons and daughters. For much we suffer while we are in this life, nothing is compared to the joy to be experienced with the glory that will be revealed to us. In this sense, let us learn from Jesus that, although the situation of so great sorrow and suffering which he experienced on the cross, he maintained his unshakable trust in the providential action of God: “Father,In your hands I commend my spirit.” This should be the confident and constant cry of our spirit, raising the assurance that God neither abandons us and nor keeps quiet before what happens with us. The response from God before the death of Jesus comes right away with the resurrection, that is anticipation of our own resurrection and so, guarantee of our full life, for he is not God of dead but of living. In other words, God doesn’t want the death. In Jesus he reveals himself as resurrection and life.


         Why do people die? Jesus taught us to cultivate the faith in God Abbá, who is turned to us with all strength an activity of his compassionate and liberator love. He attracts us to himself with bonds of tenderness and he desires to keep us bound to him. At the same time, he is always coming in our direction and he expects being welcomed. Our life on earth passes only for one stage. It should continue her journey in other stage, because we are called to the fullness. Conscious of this reality, said the wise Augustine: “O God you made us to you and our heart are restless until they rest in you”. For the one who has Faith, the death is therefore, repose in God, through which all of us have to pass to become full. The fundamental moment of our life will come in which we shall meet definitively with God, before whom we won’t be asked if we belonged to some religion or how many times we went to church, but how much we were able to love. The choices which we do in the course of the journey will determine the direction our life. Through Christ’s will, our life should attain the fullness, which starts in the daily care, in the small gestures of affection at home, in the school, in our work and in our community commitment. We are invited to maintain the communion with God who is the primordial and infinite source of life.  

Fr Ndega

KIFO KWAKE KRISTO NDICHO USHINDI WETU

Kutafakari kutoka Yoh 11: 11-27

        Tunaposherehekea uzima, tunasherehekea fumbo kuu ambalo ni zawadi itokayo kwa Mungu. Katika Kristu zawadi hii inapata ukamilifu na vile vile tunapata kuelewa kwamba maisha hayafikii mwisho hapa duniani. Urithi wa maisha ya wale waliotuacha ina thamani kuu kwetu tunaoitwa kuendelea katika imani  kuishi maisha yenye maana. Ikiwa hatuwezi kuwaona tena wale ambao walitutangulia, yale maadili waliyoishi na kutuachia ndiyo ushuhuda wa kwamba uwepo wao kati yetu haukuwa utupu. Mtakatifu John Calabria alikuwa na mazoea ya kusema, “Ikiwa tuna Mungu ndani yetu, tutafanya yale mazuri hata kwa kupita kwetu tu”. Kusherehekea wafu ni alama kuu ya jinsi wanavyoendelea kuwa muhimu kwetu sote, kwa hivyo kifo sio mwisho wa maisha: hiki kinadhihirisha tu mwisho wa sehemu moja ya maisha. Katika nyakati za sorrow na huzuni, tujiruhusu kusaidiwa na maombi ya marafiki na kuhamasishwa na neno la Mungu linaloimarisha imani yetu na uwezo wetu wa kujitolea .
           Kama Wakristo, tabia yetu kuu ni tumaini. Kwa hivyo, Mt. Paulo akasema: “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure na tumaini letu pasipo maana”. Mungu ambaye tunaamini ni Mungu wa uhai na anapotupa uzima, yeye hujiunganisha nasi na kutufanya wanawe wapendwa. Kwa kuwa mateso katika maisha haya, hayawezi kulinganishwa na furaha tutakayohisi na utukufu utakaotufunuliwa. Vilevile, tujifunze kujisalimisha kutoka kwa kielelezo cha Yesu ambaye hata katika wakati wa huzuni na mateso, aliyohisi kupitia msalaba, aliilenga imani yake katika tendo la riziki ya Mungu: “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”. Hili lazima kuwa kilio cha roho zetu ili tuhakikishie kwamba Mungu hawezi kutuacha wala kunyamaza mbele ya kinachotufanyikia. Mbele ya kufa kwake Yesu Jibu la Mungu ni ufufuko wa Mwanawe. Hilo linatupa matarajio ya kufufuka kwetu na hivyo, yatuhakikishia maisha kamili kwani yeye si Mungu wa wafu bali wa wanaoishi. Hivyo ni lazima kutangaza kwamba Mungu hataki kifo. Katika Yesu anajifunua kama ufufuko na uhai.
            Kwa nini watu  hufa? Yesu alitufundisha kulenga imani yetu katika Mungu Baba, ambaye anatujali kwa nguvu yote ya pendo lake lenye huruma na ukombozi. Yeye hutuvuta kwake kwa dhamana za huruma na anatamani kuwa mmoja nasi. Kwa wakati huo huo, yeye huja kwetu daima na hutarajia kukaribishwa. Maisha yetu duniani hupitia sehemu moja tu. Yanapaswa kuendelea safari yake katika sehemu nyingine, kwa sababu twaitwa kwa ukamilifu. Katika maana hii, Agostino asema: “Ee Mungu ulituumba tuwe wako na mioyo yetu inahangaika hadi tunapopumzika kwako”. Kwa Yule mwenye imani, kifo ni pumziko katika Mungu ambako sisi sote lazima kupitia ili tukuwe wakamilifu. Wakati muhimu sana maishani mwetu  utakuja na tutakutana na Mungu kwa njia ya kipekee. Tutakapokuwa mbele yake hatutaulizwa iwapo tulishiriki katika dini yoyote wala mara ngapi tulienda kanisani bali kiasi cha tulivyoweza kupenda. Chaguo tunayochagua katika mkondo wa safari yetu itadhihirisha mwelekeo ambao maisha yetu yatachukua. Kulingana na mapenzi ya Mungu, maisha yetu yanafaa kupata ukamilifu uanzao na uangalifu wa kila siku katika ishara za upendo nyumbani na kujitolea kwa jumuiya. Kwa hivyo tupate kuunganishwa na Mungu aliye mwanzo na chanzo cha uzima na asiyepungukiwa kamwe.


Fr Ndega

domingo, 1 de novembro de 2015

UTAKATIFU KAMA WITO WETU NA MATARAJIO YA MUNGU

Kutafakari kutoka Ufu 7: 2-4, 9-14; Mt 5, 1-12

    Tunaadhimisha sikukuu ya Watakatifu wote. Ni nafasi maalum ya kutafakari kuhusu mwito wa Mungu tangu ubatizo wetu. Utakatifu ni wito wa mkristo: “Muwe watakatifu kama Baba yenu alivyo”, asema Bwana. Mpango wa Mungu ni kutufanya washiriki katika utakatifu wake. Watakatifu ni rafiki za Mungu. Wanatupenda na kutamani tufikie huko walikotutangulia, na Mungu hawezi kuwanyima kitu. Basi, wakati tunawaheshimu watakatifu wote, tukaribishe njia ya utakatifu ya liturujia siku ya leo kama iliyowezekana na iliyotarajiwa na Mungu kwa wote.

     Kulingana na somo la kwanza, ushindi wa Mwana-kondoo ulibadilisha njia ya mauti katika njia ya uzima kwa wale wanaozifuata nyayo zake kwa uaminifu na kujiruhusu kuuawa kwa ajili yake. Wanashiriki furaha milele ya Bwana wao. Hiyo ni njia mno ya utakatifu. Kuuawa ni zawadi maalum ya Roho Mtakatifu: zawadi kwa ajili ya Kanisa nzima. Katika mashahidi, Kristo anaonyeshwa kwa njia maalum: utajiri wa Fumbo la Pasaka yake, Msalaba wake na Kufufuka kwake. Kristo, Mwana-kondoo ni shahidi wa kwanza, Shahidi kwa namna ya ajabu. Ni yeye ambaye kuwahamasisha wanaume na wanawake kujikataa, kuuchukua msalaba wao na kuzifuata nyayo zake. Tabia hii ya kujisalimisha kabisa kwa ajili ya Yesu ni tangazo la thamani kweli ambazo zinadumu milele. Mashahidi wanahisi kama mali ya Kristo na kugundua kwamba maana ya maisha yao ni kujitolea wenyewe kwa ajili ya wengine, kulingana na Mt. Paulo aliyesema, “Mimi ni radhi kabisa kujitolea mimi kabisa kwa ajili ya roho zenu” (2Wko 12:15).

        Injili ya leo inatuonyesha furaha ya watakatifu na njia inayotuwezesha kufika mbinguni. Andiko hili ni mwanzo wa iliyojulikana kama “Hotuba mlimani” ya Yesu (hii inajumuisha sura tatu 5-7). Kwanza kabisa ni muhimu sana kuifahamu nia ya Mathayo. Yeye anamjulisha Yesu kama “Musa Mpya” na kila kitu kuhusu Kristu kinaleta chapa ya upya, yaani, Mlima wa “wenye heri wanane” ni Mlima wa Sinai mpya; “Heri nane” ni mafundisho mapya kuhusu Amri; udugu ni haki mpya, inayoshinda haki ya Waalimu wa Sheria na Mafarisayo; Mwili wake ni Hekalu jipya. Utakatifu si utambulisho ya baadhi ya watu tu, bali pendekezo jipya kwa wote: “Muwe watakatifu kama Baba yenu alivyo”. Wakati Yesu alianza tangazo la Ufalme wa Mungu aliamua kuhubiri kwa maskini waliowakilishwa kupitia nyuso nyingi, yaani: walio maskini wa roho ambao ni wasio na tamaa ya makuu; wenye huzuni ni wenye unyeti mbele ya uchungu wa wenzao; nguvu za wenye upole zinatoka kwa Mungu; wenye njaa na kiu ya haki ni waliojitolea kwa kujenga jamii nzuri; wenye rehema ni walio karibu na Mungu nao ni wenye unyeti mbele ya mahitaji ya watu; wenye moyo safi ni waliomtambua Mungu yupo katika kila mtu; wapatanishi ni waliosaidia upatanisho katika jumuiya zetu; wanaoteswa maana ya haki ni walio mashahidi wa wema wa Mungu kati yetu.   


     Hali hizi zinazojulishwa na Yesu si mbali nasi, bali ni sehemu ya maisha yetu. Yeye anatambua vitu vizuri miongoni mwetu na kwa hivyo anavijulisha kama njia kamili kuingia katika Ufalme wake. Hii ni njia iliyochukuliwa na watakatifu wote kwa sababu walimwamini Yesu na mapendekezo yake. Walitambua kwamba maisha yao hayana lengo lingine ila utakatifu. Kama Mt. Yohana Calabria, waliamini kwamba mtu halazimu kufanya vitu vya ajabu ili awe mtakatifu, bali anaweza kuwa mtakatifu kupitia shughuli za kila siku. Kwa hivyo watakatifu si watu wa zamani tu, bali ni pia wengi miongoni mwetu ambao wanajitolea daima kwa ajili ya jumuiya, kwa ajili ya dunia nzuri. Kupitia uzoefu wa utakatifu wa Yohana Calabria tunajifunza kwamba ikiwa tunataka kuwasaidia wengine kuwa watakatifu, tunapaswa kuutafuta utakaso wetu wenyewe kupitia juhudi ya kila siku kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Mtu hawezi kutoa kile ambacho yeye hana. Sikukuu hii ni hamasa kwa kuyaamsha matumaini makubwa mioyoni mwetu ili tuwe watakatifu. Kupitia msaada wa neema ya Mungu, tuweze kuchukua “Heri Nane” kama mpango wa maisha na njia kamili ili “tuwe watakatifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyo”. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara