domingo, 1 de novembro de 2015

UTAKATIFU KAMA WITO WETU NA MATARAJIO YA MUNGU

Kutafakari kutoka Ufu 7: 2-4, 9-14; Mt 5, 1-12

    Tunaadhimisha sikukuu ya Watakatifu wote. Ni nafasi maalum ya kutafakari kuhusu mwito wa Mungu tangu ubatizo wetu. Utakatifu ni wito wa mkristo: “Muwe watakatifu kama Baba yenu alivyo”, asema Bwana. Mpango wa Mungu ni kutufanya washiriki katika utakatifu wake. Watakatifu ni rafiki za Mungu. Wanatupenda na kutamani tufikie huko walikotutangulia, na Mungu hawezi kuwanyima kitu. Basi, wakati tunawaheshimu watakatifu wote, tukaribishe njia ya utakatifu ya liturujia siku ya leo kama iliyowezekana na iliyotarajiwa na Mungu kwa wote.

     Kulingana na somo la kwanza, ushindi wa Mwana-kondoo ulibadilisha njia ya mauti katika njia ya uzima kwa wale wanaozifuata nyayo zake kwa uaminifu na kujiruhusu kuuawa kwa ajili yake. Wanashiriki furaha milele ya Bwana wao. Hiyo ni njia mno ya utakatifu. Kuuawa ni zawadi maalum ya Roho Mtakatifu: zawadi kwa ajili ya Kanisa nzima. Katika mashahidi, Kristo anaonyeshwa kwa njia maalum: utajiri wa Fumbo la Pasaka yake, Msalaba wake na Kufufuka kwake. Kristo, Mwana-kondoo ni shahidi wa kwanza, Shahidi kwa namna ya ajabu. Ni yeye ambaye kuwahamasisha wanaume na wanawake kujikataa, kuuchukua msalaba wao na kuzifuata nyayo zake. Tabia hii ya kujisalimisha kabisa kwa ajili ya Yesu ni tangazo la thamani kweli ambazo zinadumu milele. Mashahidi wanahisi kama mali ya Kristo na kugundua kwamba maana ya maisha yao ni kujitolea wenyewe kwa ajili ya wengine, kulingana na Mt. Paulo aliyesema, “Mimi ni radhi kabisa kujitolea mimi kabisa kwa ajili ya roho zenu” (2Wko 12:15).

        Injili ya leo inatuonyesha furaha ya watakatifu na njia inayotuwezesha kufika mbinguni. Andiko hili ni mwanzo wa iliyojulikana kama “Hotuba mlimani” ya Yesu (hii inajumuisha sura tatu 5-7). Kwanza kabisa ni muhimu sana kuifahamu nia ya Mathayo. Yeye anamjulisha Yesu kama “Musa Mpya” na kila kitu kuhusu Kristu kinaleta chapa ya upya, yaani, Mlima wa “wenye heri wanane” ni Mlima wa Sinai mpya; “Heri nane” ni mafundisho mapya kuhusu Amri; udugu ni haki mpya, inayoshinda haki ya Waalimu wa Sheria na Mafarisayo; Mwili wake ni Hekalu jipya. Utakatifu si utambulisho ya baadhi ya watu tu, bali pendekezo jipya kwa wote: “Muwe watakatifu kama Baba yenu alivyo”. Wakati Yesu alianza tangazo la Ufalme wa Mungu aliamua kuhubiri kwa maskini waliowakilishwa kupitia nyuso nyingi, yaani: walio maskini wa roho ambao ni wasio na tamaa ya makuu; wenye huzuni ni wenye unyeti mbele ya uchungu wa wenzao; nguvu za wenye upole zinatoka kwa Mungu; wenye njaa na kiu ya haki ni waliojitolea kwa kujenga jamii nzuri; wenye rehema ni walio karibu na Mungu nao ni wenye unyeti mbele ya mahitaji ya watu; wenye moyo safi ni waliomtambua Mungu yupo katika kila mtu; wapatanishi ni waliosaidia upatanisho katika jumuiya zetu; wanaoteswa maana ya haki ni walio mashahidi wa wema wa Mungu kati yetu.   


     Hali hizi zinazojulishwa na Yesu si mbali nasi, bali ni sehemu ya maisha yetu. Yeye anatambua vitu vizuri miongoni mwetu na kwa hivyo anavijulisha kama njia kamili kuingia katika Ufalme wake. Hii ni njia iliyochukuliwa na watakatifu wote kwa sababu walimwamini Yesu na mapendekezo yake. Walitambua kwamba maisha yao hayana lengo lingine ila utakatifu. Kama Mt. Yohana Calabria, waliamini kwamba mtu halazimu kufanya vitu vya ajabu ili awe mtakatifu, bali anaweza kuwa mtakatifu kupitia shughuli za kila siku. Kwa hivyo watakatifu si watu wa zamani tu, bali ni pia wengi miongoni mwetu ambao wanajitolea daima kwa ajili ya jumuiya, kwa ajili ya dunia nzuri. Kupitia uzoefu wa utakatifu wa Yohana Calabria tunajifunza kwamba ikiwa tunataka kuwasaidia wengine kuwa watakatifu, tunapaswa kuutafuta utakaso wetu wenyewe kupitia juhudi ya kila siku kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Mtu hawezi kutoa kile ambacho yeye hana. Sikukuu hii ni hamasa kwa kuyaamsha matumaini makubwa mioyoni mwetu ili tuwe watakatifu. Kupitia msaada wa neema ya Mungu, tuweze kuchukua “Heri Nane” kama mpango wa maisha na njia kamili ili “tuwe watakatifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyo”. 

Fr Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: