Kutafakari kuhusu Is 49: 14-15; Mt 6:
24-34
Liturujia inatujulisha
mifano miwili yenye nguvu kuhusu Mungu. Katika Somo la kwanza Mungu
analinganishwa kwa mama na katika injili Mungu analinganishwa kwa baba. Mungu anawapenda watu wote na hamsahau yeyote wa wana
wake. Yeye anakijali kila kitu ambacho wana wake wanahitaji. Mtakatifu Yohana
Calabria aliishi kwa uzoefu huu kwa mkazo na aliweza kuushuhudia kwa
wengine.
Watu wa Israeli walikuwa watumwa
katika Babeli na wakajihisi walioachwa na kusahauliwa. Nabii Isaya aliwasaidia
kutambua kwamba Mungu alikuwapo miongoni mwao na hakuwasahau. Yeye ni Mungu
mpole ambaye anawapenda na kuwalinda watu wake zaidi kuliko mama ampendaye
mtoto wake anyonyaye. Basi, uwepo wake ni dhamana ya utunzaji na ulinzi. Katika
injili Yesu anawafundisha wanafunzi wake kuhusu umuhimu zaidi wa maisha.
Anaongea kuhusu hatari ya utajiri na miliki yote ambayo inaweza kumshika mtu
hivi hata asiweze kifikiria mambo yanayomhusu Mungu. Nia kuu ya Yesu ni kuongea
kuhusu Mungu kama Baba aliye na wasiwasi kwa utunzaji
wa upendo kwa kila kitu. Baba huyu anatarajia jibu la ukarimu kutoka
kwa wanadamu ambao wana thamani zaidi kuliko viumbe vingine vyote. Kuwa
mwanafunzi wa kweli wa Yesu ni kutafuta kwanza Ufalme wa Mungu Baba na haki
yake kama rejea ya maisha. Kwa maneno mengine, anatualika kujisalimisha
mikononi mwa Mungu ambaye anayajua mahitaji yetu na yuko tayari daima
kutusaidia.
Injili hii inafikiriwa
msingi wa kiroho ya Mt. Yohane Calabria kwa sababu kupitia injili hii aliufanya
ugunduzi mkubwa. Aligundua jinsi ya kuishi kwa njia halisi ubaba wa Mungu na
kuwa ishara ya riziki yake kwa watu. Kutokana na andiko hili alichukua mistari
33 kama ahadi kwake: “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake; na hayo
yote mtapewa kwa ziada.” Kulingana naye “Injili anatuongelea kwamba Mungu ni
Baba, anatujali zaidi kuliko ndege wa angani na maua ya mashamba hata
atatujalia kile ambacho tunahitaji kwa chakula na kwa mavazi, lakini tunapaswa
kuutafuta kwanza Ufalme wake na haki yake”. Mt Calabria alifahamu kwamba
ililazimu
kuifufua imani duniani kwa Mungu Baba wa wanadamu wote, kupitia kujisalimisha
kabisa kwa Riziki yake. Kwake imani kweli na asili inafikiria Mungu si kama Muumba na Bwana tu, bali kwanza
kama Baba”. Mungu ni Baba, hutujali na wote ambao tunawapenda; macho yake ni
makini sana kwa kila kitu na kila kitu kinapangwa na kuongozwa na hekima, nguvu
na wema wake pasipo mwisho.
Mt. Yohana Calabria
alikuwa mtu mwenye unyeti mno kuuhusu ugumu na mateso ya wengine. Aliweza kuweka matendoni maneno yake kuhusu
wema na utunzaji
wa Mungu katika Riziki yake, akisema, “Riziki ni Mama mpole ambaye hupatia kila
kitu kwa wema wetu, hata kwa wema wetu mkubwa. Tunapaswa kuhisi tumebebwa kwa
mikono yake ya mama”. Yohana Calabria aliamini katika ukweli huo na hata
aliyapanga maisha na kazi zake zote kulingana na hali hii. Kama ishara ya
utunzaji wa Mungu alikuwa na unyeti mkubwa kwa uhusiano na wagonjwa. Alimwona
Kristo mwenyewe katika walio wagonjwa. Alifikiria mateso ya wagonjwa kama
thamani na msaada mkubwa kwa mtume wa kanisa. Aliwahamasisha na kuwaonya
wagonjwa kuukaribisha ugonjwa na mateso kwa utulivu na sala. magonjwa kwao yana
maana kwa wokovu wao na wokovu ulimwenguni. Kristu mwenyewe aliwapenda wagonjwa
na wakati wa maisha yake alikwenda mara nyingi kuwatembelea na kuwaponya. Kwa
njia Mtakatifu Yohana Calabria, tumwombe Mungu kwa ajili ya wagonjwa wote, hasa
kwa hawa ndugu zetu wapo katika misa hii ili neema ya Mungu iimarishe imani na
nguvu zao. Maisha yenu yawe ushuhuda wa wema wa Mungu kwa sisi sote.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário