quinta-feira, 29 de outubro de 2015

IMANI YA KWELI NA HALISI

Kutafakari kutoka Mk 10, 46-52

     Yeriko ni mmoja miongoni mwa miji ya zamani ulimwenguni. Hii nieneo ya baadhi ya matukio makuu ya biblia; hata katika muda wa Musa ilikuwa tayari kuongelewa kuhusu mji huu. Tukumbuke “kuzingirwa na kuchukuliwa kwa Yeriko” na Waisraeli katika wakati wa Yoshua (Yoshua 6, 1-27). Tukumbuke pia Zakayo; mabadiliko ya maisha yake yalitokea katika Yeriko. Mji huu ni karibu na mto Yordano na Yesu alipita mahali huko mara nyingi. Andiko siku ya leo linaongea kuhusu mkutano wa Yesu na kipofu Bartimayo, aliyeketi kando ya barabara ya mji. Hakika alikuisha amesikia kuhusu Yesu na alitaka sana nafasi ili kukutana naye. Lakini hakujua kwamba Yesu pia alitaka kukutana naye ili kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kisha, nafasi imefika! Shauku ya kipofu ilikuwa kubwa sana kwamba hakuna kitu au mtu kumfanya  anyamaze.

    Kilio cha kipofu ni kilio cha kila binadamu mwenye dhamiri kuhusu udhaifu wake na mahitaji ya huruma ya Mungu. Kipofu ni ishara ya kivuo dhahiri cha ndugu zetu wengi. Ni nafasi ya kutambua kwamba watu wengi wanaanguka au wameachwa barabarani. Wanapaza sauti kwa huruma na kwa nafasi kwa sababu wanaamini kwamba wale ambao wanajiita wafuasi wa Yesu wanaweza kusikiliza sauti yao na kuwatendea mema. Yesu alisikia si kilio cha kipofu tu, bali pia kilio cha wale ambao walimwambia kipofu “anyamaze”! jibu la Yesu linaonyesha mchanganyiko wa huruma na hasira, kwa sababu alikuwa kushughulika kwa upofu wa aina mbili tofauti, yaani, upofu wa Bartimayo na upofu wa umati wa watu ambao walikuwa wakimfuata Yesu bila ushirika na hisia zake. Je, ni nani ana upofu zaidi, yule aliye kipofu asili au wale ambao hawapati kuona walio na mahitaji kandokando yao? Hata hivyo kuna tumaini, kwa sababu miongoni mwa wale ambao walimwambia kipofu “unyamaze!” walikuwapo wengine ambao walimwambia “jipe moyo, anakuita! Yeye hajamsahau na hawaachi wale ambao wanamwamini”. Sauti hizi ni za watu ambao wanachukua ujumbe wa unabi na wanapata kuwahamasisha wenye kukata tamaa. Ni ishara pia ya walio upatanishi wa Mungu katika maisha ya yeyote anayegundua wito wake ili aweze kumjibu Mungu kulingana na matarajio yake.


     Yesu ambaye tunamfuata ni mwenyeunyeti sana. Ana macho na masikio makini sana kwa hali halisi ya watu. Anatualika kuwa na unyeti sawa. Kwa kawaida sisi ni kama kipofu huyo, tunahitaji mkutano wa mabadiliko ya maisha ili kuona bora nini inatokea kandokando yetu na kumfuata yesu ambaye anatuleta maana mpya kwa maisha yetu. Sisi ni pia kama wengine karibu na Yesu, lakini mbali sana na ndugu zetu, waliofungwa kabisa kwa hali halisi kandokando yetu na hata tunafikiri kwamba tuna mamlaka ya kuwaambia wengine: “mnyamaze”. Sisi  tuko na kosa kubwa. Sisi lazima kuwamakini sana kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na haitufanyi wenye huruma, imani hii ni udanganyifu. Kupitia Ekaristi hii, tumwombe Mungu neema ya imani ya kweli na halisi.

Fr Ndega
Mapitio: Nikoletee

Nenhum comentário: