domingo, 28 de fevereiro de 2016

MUNGU ANATUPA NAFASI MOJA ZAIDI TUWEZE KUZAA MATUNDA MAZURI

Kutafakari kuhusu Ex 3, 1-8a. 13-15; 1Kor 10,1-6.10-12; Lk 13,1-9

      Somo la kwanza linaongea kwamba huko mlimani Horebu Mungu anatokea kwa Musa na kuudhihirisha utambulisho wake kama Mungu aliye yupo katika historia ya ubinadamu daima. Yeye ana unyeti mbele ya hali ya mateso ya watu wake na kuamua kuwaokoa kutokana na utumwa wa Misri, kuwaongoza kwa nchi njema, yaani nafasi ya kuishi maisha mapya. Katika mwendo huu Mungu anatumia Musa kama chombo cha huruma yake na Musa anakubali kuiacha mipango yake ya maisha na kuchukua mpango wa Mungu ili ukombozi wa Mungu ufikie Watu wake kubadilisha hali ya mauti kuwa hali ya uzima. Katika somo la pili, Mt Paulo anawakumbusha Wakristo wa Korinto kwamba miongoni mwa wale waliopitia huruma na ukarimu wa Mungu wengi waliangamizwa jangwani kwa sababu maisha yao hayakumpendeza Mungu. Hili ni onyo kwa sisi sote ya kuishi kulingana na zawadi za kiroho tumepokea kwa sababu yule ambaye anatoa zawadi hizi antarajia mabadiliko ya maisha yetu kama matokeo ya tendo lake la ukarimu.  
        Katika injili, baadhi ya watu alimwendea Yesu na kumpasha habari kuhusu ukatili wa Pilato kwa ajili ya Wagalilaya. Kama ilivyotokea mara zingine, hii ni nafasi zaidi aliyotumia Yesu awafundishe na kuwaalika kwa toba. Kwanza kabisa alipaswa kusahihisha mawazo fulani yapo miongoni mwao kwamba watu ambao wanateseka ni kwa sababu ya dhambi walizotenda. Kulingana na mawazo haya, mateso yote yalionekana kama matokeo ya dhambi. Kama hii ilikuwa hali ya wagonjwa wote katika mazingira ya Yesu. Kwa hivyo, kabla ya kufanya muujiza wowote alimwambia mgonjwa, “Nakuondolea dhambi zako”. Alisema hivyo kama ushuhuda kwa jamii nzima ambayo pia ilipaswa kupona na hali ya ubaguzi kuhusu wagonjwa. Kulingana na Yesu njia hii ya kufikiri ni hatari kwa sababu inaweza kuwa kikwazo kwa watu kukataa kuwasaidia wale walio katika mateso. Kutokuwa na ahadi kwa ajili yao na kutofautiana kunayaongeza zaidi mateso yao.
        Kwake Yesu, mateso hayatokani na Mungu, bali yanaweza kuwa ni nafasi kwa mtu kumrudia Mungu kwa moyo wote na kumtukuza. Inawezekana pia kuwa ni nafasi ya jumuiya nzima kujifunza juu ya huruma waipokeayo kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kuwaongoza waonyeshe upendo na huruma hasa kwa wale wanaoteseka. Sisi ni kama wagonjwa kwa sababu ya uzoefu wa dhambi. Wakati Yesu aliposimulia mfano kuhusu mti bila rutuba, alitaka kuongea kuhusu uvumilivu na huruma ya Mungu kwa ajili ya wanadamu wote. Kama ilivyotokea na mti ule, Mungu anataka kutupa nafasi moja zaidi ili tuweze kuzaa matunda anayotarajia. Mungu hutupa muda ya kukomaa na kuishi maisha bora. Subira ya Mungu ni nafasi kwetu ya kupata wokovu kwa njia ya toba.

        Kwaresima ni nafasi tupewayo na Mungu ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu kwa uthabiti zaidi. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuacha kuwatenga watu katika makundi tofauti ya walio wema na walio dhambi na kuwaona wote kama walio dhambi wanaohitaji msamaha wa Mungu. Kulingana na Yesu, Mungu anatarajia maisha yetu yaweze kumpendeza kupitia matunda mazuri. Tumepokea nafasi nyingi ili tufikie lengo hili. Katika uzoefu wa watu wa biblia yeye anajifunua kama mkombozi na mwenye uvumilivu mbele ya hali ya udhaifu wa watu. Kwa upande wa Mungu uvumilivu na huruma; kwa upande wetu ushujaa na toba. Kama ilivyotokea na Musa, Mungu anatualika kwa uzoefu tofauti ambao unalenga kutubadilisha kuwa katika vyombo vya huruma yake.          

Fr Ndega 
Mapitio: Sara

quarta-feira, 24 de fevereiro de 2016

HALI YA MASKINI INA UHUSIANO NASI


Kutafakari kuhusu Lk 16, 19-31

     Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Siku ya leo Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo na kama matokeo ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea ya kuitumainia mali bila unyeti kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Wao walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Kwa wakati sawa, Lazaro pia ni pendekezo la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki yake hawaachi wale ambao wanamwamini.
      Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha hali katili ipo katika jamii yetu, yaani kukosekana kwa usawa kati ya watu. Katika Amerika Latina, kanisa lilikuwa limekwisha shutumu baadhi ya miaka iliyopita kwamba “Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri waliokuwa na utajiri zaidi daima juu ya maskini waliokuwa maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio na haki, tena kwa walio wema na mabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote vipatikane kwa wote.. wimbo wa Bikira Maria unashuhudia hali hii kwa njia ya ajabu na furaha kubwa kwa sababu ya njia ya Mungu ya kutenda, yaani yeye huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na kwa usawa wa haki na heshima.  
     Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamfikia Mungu ndiye yumo ndani yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na unyeti kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo, watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake awadharau wengine anatupa maisha yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda mema. Kuhusu mambo haya Mt Yohana Calabria asema: “Maskini wako ili matajiri waokoke/waokolewe”. 

     Kipindi cha Kwaresima kinatukumbusha kwamba hali ya maskini ina uhusiano nasi, kwa sababu dhambi ya jamii ni matokeo ya kiasi cha dhambi kibinafsi. Basi, ni lazima toba sio kwa dhambi za kibinafsi tu, bali kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya jamii pia. Mwendo huu unaweza kwanza kupitia kuacha njia ya ukuzaji na ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kwa kutofautiana ili tuchukue njia ya unyenyekevu ya maisha ambayo inakihusu kitu kidogo na kutufanya wenye unyeti kuwahusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa kwa sababu ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alisema Baba Mt Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu, lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unakudai kukubalika kwangu kuonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo na kutembea baada yake.”

Fr Ndega
Mapitio: Sara 

domingo, 21 de fevereiro de 2016

“HUYU NI MWANANGU MPENDWA, MSIKILIZENI”


Kutafakari kuhusu Lk 9, 28b-36

Tukio la kugeuka sura kwa Yesu kulitokea baada ya siku sita ya ufunuo kuhusu mateso, kufa na kufufuka kwake na mwaliko wake kwa wanafunzi wa kumfuata kulingana na njia yake mwenyewe, yaani “Kujikana mwenyewe, kuuchukua msalaba wake na kumfuata Yesu.” Habari ya kugeuka sura kwa Yesu tena inafuatwa na tangazo la pili kuhusu kifo na ufufuko wake. Kwa uzoefu huu Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo na Yohana. Kwa nini wafuasi hawa? Labda kwa sababu aliwapendelea kuliko wengine. Injili haiongei maana ya habari hii. Yesu aligeuka mbele ya wafuasi wake na ishara kuu zilikuwa nguo na mwili wake. Yesu aliwaonyesha kidogo utukufu wake na hali ya wakati ujao kuhusu mwili wa yeyote anayemfuata kwa uaminifu. Yesu anashiriki utukufu wake na wanafunzi wake kwa maana inampendeza kufanya hivyo ili wawe na furaha moja ya vile Mwalimu wao alivyo.

Kama illivyotokea kuhusu jangwa, Mlima pia ni mahali muhimu katika uhusiano wa Watu wa Israeli na Mungu; katika mwendo huu, Musa na Eliya wana ushiriki maalum. Katika Agano la Kale milima iliyojulikana sana ni Mlima Sinai na Horebu. Ilikuwa katika Mlima Sinai ambapo Mungu alikutana na Musa na kuwawekea Waisraeli mkataba/agano. Ilikuwa katika Mlima Horebu ambapo Eliya alijiandaa kwa muda mrefu akutane na Mungu. Katika Agano Jipya Yesu alitumia sana mahali huko mlima kama rejeo ya uhusiano wake na Baba na kama eneo kwa matukio muhimu katika kazi yake. Kulingana na utamaduni mmoja wa zamani, tukio la injili ya siku ya leo lilitokea juu ya milima Tabor.   

       Uwepo wa Musa na Eliya unaongea kuhusu rejea ya ufunuo katika Agano la Kale. Waliongea na Yesu wakionyesha kwamba hakuna mpasuko/mshipa kati ya mafundisho yao na mafundisho ya Yesu, bali uhusiano na mwendelezo. Lakini kulingana na sauti iliyosikika kutoka kwenye wingu, mwendelezo huu, ambao ni Yesu, lazima kuwa kipaumbele katika maisha ya wanafunzi kwa sababu ni Yesu peke yake kwa mamlaka aliyoyapokea kutoka kwa Baba ili kufundisha na kutafsiri kamili lile lililosemwa na mababu wa zamani.  Kusikiliza katika Biblia ni kitenzi chenye nguvu sana. Hii ni tabia ya myahudi mbele ya Neno la Mungu, akiweka vitendoni au kufanya mazoezi/vitendo kuhusu yale aliyosikia. Kusikiliza kuna uhusiano na kushika au kutenda. Baba anashuhudia kuhusu Mwana wake, anamweka kama rejeo cha maisha yetu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni”. Huu ni pia mwaliko ili tufananishe maisha yetu kulingana na Neno la Yesu. Neno la Yesu ni kipimo ili mtu awe pia mwana mpendwa wa Mungu kama Yeye. Tunashiriki katika kugeuka sura kwa Yesu kupitia kusikiliza makini kwa Neno lake.

     Kuhusu mambo hayo Mtakatifu Yohana Calabria alisema: sisi ni makini sana kwa maneno ya binadamu na kuhusu hiyo ni sawa. Lakini tunapaswa kuwa na uangalifu zaidi kwa Neno la Mungu ambalo ni – consecratory – huweka wakfu, ni kwamba, linalifanya lile linalosema.” Mtakatifu Yohane Calabria ilikuwa anasema hasa kuhusu injili ambayo ni sheria kwetu Poor Servants of Divine Providence. Katika sehemu nyingine ya maandiko yake alisema: “Ikiwa sisi huamini katika maneno ya kuapishwa kwa – consecration – katika misa, yaani “twaeni mle wote, twaeni mnywe wote”, tunapaswa kuamini pia wakati Yesu asema: “Msiwe na wasiwasi” au “Baba yeno wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote” au “mtafuteni kwanza ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.” katika maneno mengine, kutokana na Maneno ya Yesu tunaalikwa kuwa “Injili hai.” Hiki ni kipimo kwetu ili tuweze kumtambua uso uliogeukwa wa Yesu katika nyuso zenye mateso za ndugu wengi miongoni mwetu. Neema ya Mungu itusaidie kulisikiliza Neno lake kwa uangalifu na kutangaza habari njema ya siri ya Mwanae kama njia ya wokovu kwa ulimwengu wote.  

Fr Ndega

Mapitio: Sara  

segunda-feira, 15 de fevereiro de 2016

ALITUONYESHA NJIA KAMILI JINSI YA KUYASHINDA MAJARIBU YOTE

Kutafakari kuhusu Kum 26, 4-10; Rum 10, 8-13; Lk 4, 1-13 

Kwaresima ni siku arobaini za maandalizi kwa adhimisho la fumbo la Pasaka ya Kristo. Wakati wa kwaresima unalenga kuwa uzoefu wa jangwa. Kwa upande wa viongozi wengi katika biblia jangwa palikuwa mahali pa mkutano na Mungu kwa hamu na uzoefu wa utakaso. Walitafuta mahali huko kabla ya matukio muhimu maishani mwao ili waweze kuchukua ahadi kwa nguvu na uaminifu. Vivyo hivyo, ni Kwaresma kama maandalizi kwa tukio muhimu sana la imani yetu, yaani Ufufuko wa Yesu. Wakati huu unatukumbusha siku arobaini ambazo Musa alibaki milimani Sinai ili azipokee Amri Kumi; na tena miaka arobaini ya utakaso wa Wana wa Israeli jangwani; tena siku arobaini za Eliya akitembea mpaka milima Horebi ili akutane na Mungu na kuyapokea maelekezo ya kazi yake kama nabii; kuna pia uhusiano na uzoefu wa Yesu wakati wa siku arobaini jangwani kabla ya kwanza kazi yake. Basi, kwaresima ni wakati maalum ya kuikuta maana kwa kuyashinda majaribu yote katika safari yetu, kwa sababu ya Kristo kwanza aliyashinda.
Somo la kwanza linaongea kwamba kumbukumbu ya historia ya Wana wa Israeli ni maana ya utambulisho wao na msaada wakumbuke daima mamba makuu ya Mungu katika safari yao. Walifurahi sana kwa sababu, katika nchi mpya walipokuwa wakiishi, wakapata kupanda na kuvuna malimbuko ya mazao. Musa anawaongoza kuungana tukio hili na mambo yote yaliyotokea katika safari yao ya ukombozi, wakimshukuru Mungu kwa sababu ya uaminifu wake na riziki yake kwa ajili yao. Sadaka ya watu ni mwendo wa kumrudishia Mungu zawadi ambazo zinatokana na ukarimu wake. Somo la pili linaongea kuhusu ukaribu wa Mungu kupitia neno lake ambaye ni Yesu Kristo. Kwa upande wake Kristo amekwisha tuokoa, lakini imani ni kipimo muhimu kwa kupata wokovu huu. Bwana wetu yuko tayari kutusaidia wakati tumwitapo ili tushinde majaribu ya kuishi mbali sana naye. Uaminifu wake ni maana ya nguvu yetu na utajiri wetu.   
Katika injili, Yesu aliongozwa jangwani na nguvu ya Roho Mtakatifu. Kama jangwa ni mahali pa uzoefu mzuri wa Mungu, Yesu alienda huko kwa sababu alitaka kutambua vizuri mpango wa Mungu. Uzoefu huu ulimhamasisha sana ili aanze kazi yake aliyomkabidhi Baba yake. Wakati huu pia alijaribiwa na Shetani ili akate tamaa kuhusu kila kitu ambacho kilikuwa maana ya utambulisho wa Yesu. Alimshawishi Yesu atumie uwezo wake kwa manufaa yake binafsi. Yesu alijaribiwa pia kutumia mamlaka badala ya upendo, huruma na utumishi. Tena Yesu alishawishiwa kusifiwa badala ya kutangaza Mungu na Ufalme wake. Majaribu matatu ya Yesu yanamaanisha majaribio yote ambayo yalikuwapo maishani mwake wakati wa kazi yake. Hata hivyo, alipata kushinda majaribu yote kwa sababu akaongozwa na Roho Mtakatifu na kuwa mtiifu kwa Baba yake. Hakuna kilichomvuruga kutokana na muhimu sana kwa sababu alikuwa mtu mwenye kupatikana na hatia.

Majaribu ya mali, nguvu na utukufu aliyokabili Yesu hayakumzuia kufanya mapenzi ya Mungu. Kama ilivyotokea naye, mitego ya mshawishi yanatuongoza kuacha ahadi yetu katika kanisa/jumuiya ama kutumia nguvu zaidi kuliko utumishi ama kuongea zaidi kuliko kusikiliza ama kuamuru zaidi kuliko kutii ama kudanganya kuliko kusaidia ama kulazimisha kuliko kupendekeza ama kutafuta upendeleo zaidi kuliko kupenda. Lakini, kulingana na Mtakatifu Agostino “Ikiwa katika Kristo tumeshawishiwa, katika yeye tunashinda shetani. Kristo angeweza kumtupa mshawishi mbali sana nawe; lakini ikiwa yeye hakuwa ameshawishiwa hangetufundisha jinsi ya kushinda juu ya majaribu.” Mfano wa Yesu katika uaminfu wake kwa Baba ni mwaliko kwa uaminifu pia. yeyote ambaye anazifuata nyayo zake, na kufunguliwa kwa msaada wa Roho wake anapata kufanya mapenzi ya Mungu kama yeye alivyo. Ushindi wake unafufua tumaini letu la kufikia mafanikio katika mapigano yetu dhidi ya kila kitu kinachotuvuruga kutokana na muhimu sana katika safari yetu ya watumishi wa Mungu.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

quinta-feira, 11 de fevereiro de 2016

WAKATI WA MABADILIKO NA WA WOKOVU NDIO SASA


Kutafakari kutoka  Yoe 2, 12-18; 2Kor 5, 20-6:2 Mt 6, 1-6; 16-18

        Kwaresima ni siku arobaini za maandalizi kwa adhimisho la fumbo la Pasaka ya Kristo. Wakati huu unatukumbusha siku arobaini ambazo Musa alibaki milimani Sinai; pia miaka arobaini ya Wana wa Israeli jangwani; tena siku arobaini za Eliya akitembea mpaka milima Horebi na siku arobaini za Yesu jangwani aliyeongozwa na Roho Mtakatifu. Wakati wa kwaresima unalenga kuwa uzoefu wa jangwa. Kwa upande wa viongozi wengi katika biblia jangwa palikuwa mahali pa mkutano na Mungu kwa hamu na uzoefu wa utakaso. Walitafuta mahali huko kabla ya matukio muhimu maishani mwao ili waweze kuchukua ahadi kwa nguvu na uaminifu. Vivyo hivyo, ni Kwaresma kama maandalizi kwa tukio muhimu sana la imani yetu, yaani Ufufuko wa Yesu.   

       Ni wakati kwa kutafakari kwa njia ya ndani kuhusu huruma ya Mungu na hali yetu ya wenye dhambi. Hasa katika Mwaka huu wa Jubilei, kutafakari kwetu kuhusu huruma ya Mungu kunatuongoza kuishi katika mwanga wa maneno ya Bwana: “Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma (Lk 6, 36).” Dhamiri kuhusu matokeo ya dhambi katika maisha yetu inatuongoza kumwomba Mungu kulingana na somo la kwanza, yaani “Wahurumie watu wako ee Bwana!” nasi tunajua kwamba Mungu anawahurumia watu wake sio kwa sababu wanastahili, lakini kwa sababu hii ni tabia yake ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa rehema. Kulingana na Baba Mtakatifu Francisco, “Mbele ya ukubwa wa dhambi, Mungu anajibu kwa msamaha kamili. Huruma itakuwa daima kubwa kuliko dhambi yoyote, na hakuna awezaye kuuwekea mipaka upendo wa Mungu anayesamehe daima.” Kwa hivyo tunaalikuwa kumrudia yeye kwa imani na kuutumainia wokovu wake. Kama mwendelezo, somo la pili linaongea kuhusu mahitaji ya upatanisho na Mungu kwa sababu yeye mwenyewe anatupa nafasi ya kufanya hivyo kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo. Huu ni wakati wa neema, nasi hatuwezi kuipokea neema ya Mungu bure. Wakati wa mabadiliko na wa wokovu ndio sasa.

     Katika dini ya kiyahudi, kuna hatua tatu muhimu sana ambazo zinadhihirisha utambulisho wa myahudi wa kweli, yaani sala, sadaka (itolewayo kwa maskini) na kufunga. Hasa wakati huu wa kwaresima tunaalikwa kuchukua hali hizi kama ishara ya toba yetu. Yesu alipopendekeza hatua hizi tatu, yeye aliwakumbusha wafuasi wake kuhusu maana na roho ambayo lazima kuimarisha hatua hizi. Wakati wa Yesu, kufunga kulikuwa shughuli ya kawaida, naye pia alifunga kwa wakati wa siku arobaini jangwani kabla ya kuanza ujumbe wake kwa umma. Yesu alitaka kwamba wanafunzi watende kwa tabia ya kweli sio kama ile ya baadhi ya watu (wanafiki) ambao walipofunga wakaonyesha huzuni; hao walikunja nyuso zao wapate kuonekana kwa watu kuwa wanafunga. Yesu aliihakiki tabia hii na akasema kwamba wamekwisha pata tuzo lao. Kwa Yesu kufunga kuzuri ni kujinyima baadhi ya chakula kwa mshikamano na maskini. Tunaweza kueneza ujumbe huu kwa kufunga baadhi ya maneno, ya matendo na ya mawazo ambayo si mazuri katika uhusiano wetu na wengine. Kwa hivyo kanisa katoliki linapendekeza hayo hasa wakati huu ambao ni kipindi maalum cha toba na mabadiliko ya maisha.


         Kuhusu sala, ni vizuri pia kuufuata mfano wa Bwana wetu. Yeye alikuwa mtu wa sala na aliijulisha sala kama njia ya uaminifu kwa mpango wa Mungu. Sala yake ilikuwa maonyesho wa uhusiano wake na Baba na mwaliko kwa wanafunzi wake wafanye vivyo hivyo kama utambulisho naye. Kwaresima ni wakati wa sala kwa hamu zaidi, kufungua akili zetu na mioyo yetu kwa tendo la wokovu wa Mungu. Huu ni wakati pia wa kutenda matendo ya huruma kwa wenzetu, kuonyesha juhudi yetu ya kubadili hali yetu na kandokando yetu. Majivu usoni ni ishara ya hali yetu ya ndani na kwamba tunakubali mwaliko wa Kanisa wa toba kwa sababu wakati wa kuukaribisha wokovu wa Mungu na kuiamini injili ndio sasa.   

Fr Ndega
Mapitio: Sara