Kutafakari kuhusu Kum 26, 4-10; Rum
10, 8-13; Lk 4, 1-13
Kwaresima ni siku arobaini za maandalizi kwa
adhimisho la fumbo la Pasaka ya Kristo. Wakati wa kwaresima unalenga kuwa
uzoefu wa jangwa. Kwa upande wa viongozi wengi katika biblia jangwa palikuwa
mahali pa mkutano na Mungu kwa hamu na uzoefu wa utakaso. Walitafuta mahali
huko kabla ya matukio muhimu maishani mwao ili waweze kuchukua ahadi kwa nguvu
na uaminifu. Vivyo hivyo, ni Kwaresma kama maandalizi kwa tukio muhimu sana la
imani yetu, yaani Ufufuko wa Yesu. Wakati huu unatukumbusha siku arobaini
ambazo Musa alibaki milimani Sinai ili azipokee Amri Kumi; na tena miaka
arobaini ya utakaso wa Wana wa Israeli jangwani; tena siku arobaini za Eliya
akitembea mpaka milima Horebi ili akutane na Mungu na kuyapokea maelekezo ya
kazi yake kama nabii; kuna pia uhusiano na uzoefu wa Yesu wakati wa siku
arobaini jangwani kabla ya kwanza kazi yake. Basi, kwaresima ni wakati maalum ya kuikuta maana kwa kuyashinda majaribu yote katika safari yetu, kwa sababu ya Kristo kwanza aliyashinda.
Somo la kwanza linaongea
kwamba kumbukumbu ya historia ya Wana wa Israeli ni maana ya utambulisho wao na
msaada wakumbuke daima mamba makuu ya Mungu katika safari yao. Walifurahi sana
kwa sababu, katika nchi mpya walipokuwa wakiishi, wakapata kupanda na kuvuna
malimbuko ya mazao. Musa anawaongoza kuungana tukio hili na mambo yote
yaliyotokea katika safari yao ya ukombozi, wakimshukuru Mungu kwa sababu ya
uaminifu wake na riziki yake kwa ajili yao. Sadaka ya watu ni mwendo wa
kumrudishia Mungu zawadi ambazo zinatokana na ukarimu wake. Somo la pili
linaongea kuhusu ukaribu wa Mungu kupitia neno lake ambaye ni Yesu Kristo. Kwa
upande wake Kristo amekwisha tuokoa, lakini imani ni kipimo muhimu kwa kupata
wokovu huu. Bwana wetu yuko tayari kutusaidia wakati tumwitapo ili tushinde
majaribu ya kuishi mbali sana naye. Uaminifu wake ni maana ya nguvu
yetu na utajiri wetu.
Katika
injili, Yesu aliongozwa jangwani na nguvu ya Roho Mtakatifu. Kama jangwa ni
mahali pa uzoefu mzuri wa Mungu, Yesu alienda huko kwa sababu alitaka kutambua
vizuri mpango wa Mungu. Uzoefu huu ulimhamasisha sana ili aanze kazi yake
aliyomkabidhi Baba yake. Wakati huu pia alijaribiwa na Shetani ili akate tamaa
kuhusu kila kitu ambacho kilikuwa maana ya utambulisho wa Yesu. Alimshawishi
Yesu atumie uwezo wake kwa manufaa yake binafsi. Yesu alijaribiwa pia kutumia
mamlaka badala ya upendo, huruma na utumishi. Tena Yesu alishawishiwa kusifiwa
badala ya kutangaza Mungu na Ufalme wake. Majaribu matatu ya Yesu yanamaanisha
majaribio yote ambayo yalikuwapo maishani mwake wakati wa kazi yake. Hata
hivyo, alipata kushinda majaribu yote kwa sababu akaongozwa na Roho Mtakatifu na
kuwa mtiifu kwa Baba yake. Hakuna kilichomvuruga kutokana na muhimu sana kwa
sababu alikuwa mtu mwenye kupatikana na hatia.
Majaribu
ya mali, nguvu na utukufu aliyokabili Yesu hayakumzuia kufanya mapenzi ya
Mungu. Kama ilivyotokea naye, mitego ya mshawishi yanatuongoza kuacha ahadi
yetu katika kanisa/jumuiya ama kutumia nguvu zaidi kuliko utumishi ama kuongea
zaidi kuliko kusikiliza ama kuamuru zaidi kuliko kutii ama kudanganya kuliko
kusaidia ama kulazimisha kuliko kupendekeza ama kutafuta upendeleo zaidi kuliko
kupenda. Lakini, kulingana na Mtakatifu Agostino “Ikiwa katika Kristo tumeshawishiwa,
katika yeye tunashinda shetani. Kristo angeweza kumtupa mshawishi mbali sana
nawe; lakini ikiwa yeye hakuwa ameshawishiwa hangetufundisha jinsi ya kushinda
juu ya majaribu.” Mfano wa Yesu katika uaminfu wake kwa Baba ni mwaliko kwa
uaminifu pia. yeyote ambaye anazifuata nyayo zake, na kufunguliwa kwa msaada wa
Roho wake anapata kufanya mapenzi ya Mungu kama yeye alivyo. Ushindi wake
unafufua tumaini letu la kufikia mafanikio katika mapigano yetu dhidi ya kila
kitu kinachotuvuruga kutokana na muhimu sana katika safari yetu ya watumishi wa
Mungu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário