Kutafakari kuhusu Lk 16,
19-31
Kama tujuavyo, mifano ni sehemu ya
ajabu ya ufundishaji wa Yesu. Kupitia mfano yeye anaweka rahisi na kupatikana
kwa wote siri za Ufalme wa Mungu. Siku ya leo Yesu anasimulia mfano wa mtu tajiri
na Lazaro maskini anawaonya wasikilizaji wake kuhusu hali ijayo na kama matokeo
ya chaguzi za watu katika wakati huu. Mtu tajiri ni ishara ya walio na mazoea
ya kuitumainia mali bila unyeti kuhusu kile kinachotokea kandokando yao. Wao
walichagua kwa nafsi yao njia ambayo itawaongozea mauti. Lazaro ni ishara ya
walio maskini ambao wameachwa bila ulinzi na utunzaji; wanapiga kelele ili
wapate nafasi ya kuishi kwa heshima. Kwa wakati sawa, Lazaro pia ni pendekezo
la kuishi tofauti, kuyalenga maisha katika thamani za kweli. Huyo ni ishara ya
uvumilivu, ya mapigano na mwaliko wa kumtumainia Mungu ambaye katika riziki
yake hawaachi wale ambao wanamwamini.
Kupitia mfano huu Yesu anatukumbusha hali katili ipo
katika jamii yetu, yaani kukosekana kwa usawa kati ya watu. Katika Amerika
Latina, kanisa lilikuwa limekwisha shutumu baadhi ya miaka iliyopita kwamba
“Hali mbaya ya jeuri imezaa matajiri waliokuwa na utajiri zaidi daima juu ya
maskini waliokuwa maskini zaidi daima.” Hali hii ni tofauti kabisa na matarajio
ya Mungu ambaye, kulingana na wema wake, ananyesha mvua kwa wenye haki na wasio
na haki, tena kwa walio wema na mabaya ili vitu vyote alivyoumba kwa wote
vipatikane kwa wote.. wimbo wa Bikira Maria unashuhudia hali hii kwa njia ya
ajabu na furaha kubwa kwa sababu ya njia ya Mungu ya kutenda, yaani yeye
huwashusha wakuu na kuwapandisha wadogo ili waweze kuishi pamoja kama ndugu na
kwa usawa wa haki na heshima.
Mungu anajitambulisha na hali ngumu ya
wasio na nguvu na ya maskini. Udhalimu wote unaofanyika kwao unamfikia Mungu ndiye
yumo ndani yao. Katika wakati ujao, baada ya hali ya dunia, hali itakuwa
tofauti, yaani waliopokea mambo mema katika maisha yao bila ahadi na unyeti
kuhusu hali ya wengine wataumizwa na wale waliopata mabaya kama Lazaro alivyo,
watafarijiwa. Yeyote ambaye anatumia mali yake awadharau wengine anatupa maisha
yake takatakani kwa sababu maisha hayamaanishi mali mengi bali uwezo wa kutenda
mema. Kuhusu mambo haya Mt Yohana Calabria asema: “Maskini wako ili matajiri
waokoke/waokolewe”.
Kipindi cha Kwaresima kinatukumbusha
kwamba hali ya maskini ina uhusiano nasi, kwa sababu dhambi ya jamii ni matokeo
ya kiasi cha dhambi kibinafsi. Basi, ni lazima toba sio kwa dhambi za kibinafsi
tu, bali kuchukua jukumu kuhusu dhambi ya jamii pia. Mwendo huu unaweza kwanza
kupitia kuacha njia ya ukuzaji na ukusanyaji ambayo kwa kawaida inatuongoza kwa
kutofautiana ili tuchukue njia ya unyenyekevu ya maisha ambayo inakihusu kitu
kidogo na kutufanya wenye unyeti kuwahusu wale wasio na kitu. Mungu anatuokoa
kwa sababu ya upendo wake, lakini anathamini sana juhudi zetu kama alisema Baba
Mt Benedito wa kumi na sita: “kwa kweli, wokovu ni zawadi iliyo neema ya Mungu,
lakini ili uwe ufanisi katika maisha yangu unakudai kukubalika kwangu
kuonyeshwa kupitia matendo, yaani kupitia utayari wa kuishi kama Yesu alivyo na
kutembea baada yake.”
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário