Kutafakari
kutoka Yoh 11: 11-27
Tunaposherehekea uzima, tunasherehekea
fumbo kuu ambalo ni zawadi itokayo kwa Mungu. Katika Kristu zawadi hii inapata
ukamilifu na vile vile tunapata kuelewa kwamba maisha hayafikii mwisho hapa
duniani. Urithi wa maisha ya wale waliotuacha ina thamani kuu kwetu tunaoitwa
kuendelea katika imani kuishi
maisha yenye maana. Ikiwa hatuwezi kuwaona tena wale ambao walitutangulia, yale
maadili waliyoishi na kutuachia ndiyo ushuhuda wa kwamba uwepo wao kati yetu
haukuwa utupu. Mtakatifu John Calabria alikuwa na mazoea ya kusema, “Ikiwa tuna
Mungu ndani yetu, tutafanya yale mazuri hata kwa kupita kwetu tu”. Kusherehekea
wafu ni alama kuu ya jinsi wanavyoendelea kuwa muhimu kwetu sote, kwa hivyo
kifo sio mwisho wa maisha: hiki kinadhihirisha tu mwisho wa sehemu moja ya maisha.
Katika nyakati za sorrow na huzuni, tujiruhusu kusaidiwa na maombi ya marafiki
na kuhamasishwa na neno la Mungu linaloimarisha imani yetu na uwezo wetu wa kujitolea
.
Kama Wakristo, tabia yetu kuu ni tumaini. Kwa hivyo,
Mt. Paulo akasema: “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure na tumaini
letu pasipo maana”. Mungu ambaye tunaamini ni Mungu wa uhai na anapotupa uzima,
yeye hujiunganisha nasi na kutufanya wanawe wapendwa. Kwa kuwa mateso katika
maisha haya, hayawezi kulinganishwa na furaha tutakayohisi na utukufu utakaotufunuliwa.
Vilevile, tujifunze kujisalimisha kutoka kwa kielelezo cha Yesu ambaye hata
katika wakati wa huzuni na mateso, aliyohisi kupitia msalaba, aliilenga imani
yake katika tendo la riziki ya Mungu: “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho
yangu”. Hili lazima kuwa kilio cha roho zetu ili tuhakikishie kwamba Mungu
hawezi kutuacha wala kunyamaza mbele ya kinachotufanyikia. Mbele ya kufa kwake
Yesu Jibu la Mungu ni ufufuko wa Mwanawe. Hilo linatupa matarajio ya kufufuka
kwetu na hivyo, yatuhakikishia maisha kamili kwani yeye si Mungu wa wafu bali
wa wanaoishi. Hivyo ni lazima kutangaza kwamba Mungu hataki kifo. Katika Yesu anajifunua
kama ufufuko na uhai.
Kwa nini watu hufa? Yesu alitufundisha kulenga
imani yetu katika Mungu Baba, ambaye anatujali kwa nguvu yote ya pendo lake
lenye huruma na ukombozi. Yeye hutuvuta kwake kwa dhamana za huruma na
anatamani kuwa mmoja nasi. Kwa wakati huo huo, yeye huja kwetu daima na
hutarajia kukaribishwa. Maisha yetu duniani hupitia sehemu moja tu. Yanapaswa kuendelea
safari yake katika sehemu nyingine, kwa sababu twaitwa kwa ukamilifu. Katika maana
hii, Agostino asema: “Ee Mungu ulituumba tuwe wako na mioyo yetu inahangaika
hadi tunapopumzika kwako”. Kwa Yule mwenye imani, kifo ni pumziko katika Mungu
ambako sisi sote lazima kupitia ili tukuwe wakamilifu. Wakati muhimu sana maishani
mwetu utakuja na tutakutana
na Mungu kwa njia ya kipekee. Tutakapokuwa mbele yake hatutaulizwa iwapo
tulishiriki katika dini yoyote wala mara ngapi tulienda kanisani bali kiasi cha
tulivyoweza kupenda. Chaguo tunayochagua katika mkondo wa safari yetu
itadhihirisha mwelekeo ambao maisha yetu yatachukua. Kulingana na mapenzi ya
Mungu, maisha yetu yanafaa kupata ukamilifu uanzao na uangalifu wa kila siku
katika ishara za upendo nyumbani na kujitolea kwa jumuiya. Kwa hivyo tupate kuunganishwa na Mungu
aliye mwanzo na chanzo cha uzima na asiyepungukiwa kamwe.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário