domingo, 31 de janeiro de 2016

KUONGOKA KWA MTAKATIFU PAULO NI KIPIMO CHA KUONGOKA KWETU


Kutafakari kuhusu Mk 16, 15-18

      Hii ni nafasi maalum ya kuonyesha upendo wetu kwa kazi ya Mungu kama alivyo Mt. Paulo. Mtu huyo alikuwa mcha Mungu na kushughulika sana kwa ajili ya dini yake. Kupitia njia yake ya kuishi sheria kwa uaminifu, aliamini kwamba akawa anampendeza Mungu. Kwa jina la Mungu aliwatesesha watu wengi. Kwa sababu ya matendo ya Sauli, aliye na ushabiki, watu wengi walikufa. Moyo wa ibada na nguvu zake zote zilitumika kwa kutangaza Mungu wa mauti na uwepo wake ulisababisha hofu na mateso kwa watu. Hakika hakuwa akitumikia Mungu wa kweli. Basi ufunuo wa Yesu wakati wa safari ya Sauli ulikuwa maonyesho ya kwamba kujitoa kwake hakumpendeza Mungu. Sauli alipaswa kugundua tena maana ya maisha na kazi yake. Alikuwa aliyetesesha na sasa ndiye aliyeteseka. Kulingana na maneno yake mwenyewe, tunaweza kusema kwamba Sauli alizaliwa tena akiwa mjumbe mkuu wa Yesu kwa mataifa yote. Alipata kufanya kazi zaidi kuliko mitume wengine wote kwa ajili ya Yesu. Huu ni mwendo wa toba ambao sisi sote tunaalikwa kuchukua.   

       Uwezo wa Paulo wa kuongea na kufundisha unatoka kwa Yesu ambaye ana maneno ya neema na nguvu. Ingawa yeye ni yule peke yake kwa mamlaka ya kutangaza wokovu wa Mungu, alishiriki mamlaka hii na Paulo na wanafunzi wengine wake ili watumikie watu, wakidhamini maisha mengi kwa wote. Kulingana na injili ya siku ya leo, kipimo kwa kuishi maisha mengi haya ni imani, ambayo huja kwetu kupitia hali ya ubatizo. Wanafunzi walitumwa kama wajumbe wa habari njema kwa viumbe vyote kwa sababu injili haina mpaka. Maisha mapya ambayo Yesu alileta kupitia ufufuko wake yanafikia uumbaji mzima. Yesu alikuwa amewaahidia kuandamana na safari yao mpaka upeo. Ingawa uwepo wa mwili wa Yesu usionekana tena, Roho wake yupo daima katika safari ya mitume na maisha ya wote waliomwamini umeyafanya maneno yao ufanisi kupitia ishara nyingi na matendo mengi mazuri.

      Utumishi kwa watu ambao ni wa Mungu ni utumishi kwa Mungu. Kwa hivyo ni lazima kuwa macho kuepuka kuyatumia mamlaka kwa njia mbaya. Mbele yao Yesu alitenda kwa mamlaka kinyume na nguvu za maovu ambayo yaliwapooza watu, yakiwazuia kushiriki kikamilifu katika jamii. Aliwadai njia ya unyenyekevu wa maisha kupitia kujinyima na kujitolea hasa kwa ajili ya wagonjwa, kutangaza ukaribu wa ufalme wa Mungu. Ni jukumu lao kutangaza ufalme wa Mungu, lakini ikiwa watu hawalikubali pendekezo lao si jukumu lao tena. Wanafunzi wa Yesu wanapaswa kutenda kama mwalimu wao alivyo, yaani kuheshimu uhuru wa wengine. Ufalme wa Yesu ni ufalme wa uhuru na amani, wa haki na msamaha. Habari ya ufalme huu inatokana na ukarimu wa Mungu. Nayo ni njema maana ni matokeo ya bure, kuusaidia uhuru.
 
     kama wanafunzi wapya wa Yesu sisi pia tunahitaji mkutano wa kuongoka/toba kama ilivyotokea na mt. Paulo. Kwanza kabisa, tunapaswa kuwa macho kwa msukumo wa Mungu na kuzifuata nyayo za Yesu kuchukua njia yake ya maisha, yaani njia ya unyenyekevu. Hatuwezi kufikiri kwa hakika kwamba tunampendeza Mungu wala kwamba hatuhitaji mwendo wa toba. Mwendo huu ni wa muda mrefu sana. Ingawa Paulo alikuwa mtume mkuu aliruhusu kusaidiwa na marafiki wengi, yaani Luka, Marko, Barnabas, Timotheo, Tito na viongozi wengine wa jumuiya ambazo alitengeneza. Kulingana na uzoefu wake mafanikio ya utume wetu yanawezekana ikiwa uzoefu wa kutenda pamoja unapata kushinda uzoefu wa kutenda mtu akiwa peke yake, kusaidiana katika jumuiya na kwa manufaa wa jumuiya. Tunaweza kutangaza halisi ukaribu wa ufalme kupitia utumishi wetu wa ukarimu na bure, kuheshimu wale waliotenda tofauti nasi. Baadhi ya ugumu katika safari yetu tunapaswa kukabili kupitia roho ya sala na toba daima. Ukarimu na utayari wetu uwe vyombo ambavyo Mungu aweze kutumia kuwajalia wote maisha mengi.

Fr Ndega

Mapitio: Sara   

Nenhum comentário: