Kutafakari kutoka
Yoh 13, 1-15
Liturujia ya Kikristu ina asili katika ibada ya Wayahudi,
ambayo ina kama umuhimu Jahveh, Mungu
aliyeamua kufanya historia na watu wake, akianzisha agano la upendo nao. Tukio hili
lilitanguliwa na tendo la nguvu, likiweka huru mababu wa Wayahudi kutoka utumwa
wa Misri. Watu hao walipokea kutoka kwa Mungu uongozi ili kusherehekea nafasi
maalum ya uhuru wao kwa kula mwana-kondoo wa mwaka mmoja. Hatimaye, walizipokea
Amri jangwani Sinai kama alama ya agano aliloanzisha Mungu nao. Hao walikuwa
Watu wa Mungu. Tangu kipindi hiki na kuendelea Wayahudi wameadhimisha uhuru wao
kila mwaka kwa kula hasa kile mababu wao walikuwa wamekula katika usiku maarufu
wa uhuru. Mkutano huu unaitwa Mlo wa Pasaka.
Kutumia Ibada sawa, Yesu alianzisha Ibada mpya, ni
kwamba, Mlo wa Ekaristi, akitangaza kwa Wafuasi wake ukombozi kamili ambao
ulikuwa ukija na kwamba alitamani kwa shauku kushiriki na rafiki zake. Katika
karamu hii kwa hali ya familia na matarajio makuu, Yesu alijitoa kama chakula,
akitangulia kwa njia ya ibada kile kitatokea naye msalabani. Kupitia ishara na
mifano alionyesha maana ya kujisalimisha huria na kwamba pia lazima kuwa tabia
ya maisha ya wafuasi wake. Kwa hiyo, aliwaosha wafuasi miguu, akiwapa mfano wa
unyenyekevu na utupu (Kenosis), akiunganisha milele adhimisho la Mwili na Damu
yake na utumishi wa udugu. Wale ambao wataendeleza kazi ya Mwalimu ulimwenguni,
wanapaswa kuchukua tabia sawa ya utumishi, mawazo mapya na uhusiano mpya.
Yesu ni Mwalimu ambaye anatumikia na anapenda hadi
matokeo upeo. Akijua kwamba upendo unahitaji uwepo, yeye aliendeleza uwepo wake
ulimwenguni kupitia Ekaristi. Ekaristi ni maonyesho ya kujisalimisha kwake
Kristu huria na alama ya upendo inayokuwa utumishi. Hali hii una uhusiano na
utumishi wa ukuhani, ishara ya Kristu Mchungaji ambaye anaendelea kuongoza kundi
lake. Kupitia ubatizo tuna ukuhani pamoja na waminifu wengine kushiriki katika mwili
mmoja wa Kristu, kuchukua jukumu la kuendeleza kujenga mwili huo kwa upendo. Ekaristi
ina maana tu ikiwa ni maonyesho ya upendo wa udugu na wale tu ambao wanapenda
wanaweza kutumikia. Wale tu ambao wanapenda kweli wanaweza kuendelea hadi matokeo upeo. Upendo tu
unazaa ushirikiano na “vitu tu vinavyofanywa na upendo vina uimara”.
Hili ni fumbo la imani yetu: ukweli wa ndani na utajiri tunaoalikuwa
kukaribisha kwa upendo na unyenyekevu na kumjua Mungu kama yeye ndiye. Ukweli
huu unaitwa Fumbo la Paska, ambalo linajumuisha mateso, kifo na ufufuko wa
Yesu. Yesu alianzisha Ekaristi katika Alhamisi Kuu, kutoa mwili na damu
yake kwa kula na kunywa wakati wa Karamu
ya Mwisho. Ijumaa Kuu tena akatupa mwili wake na damu yake, lakini wakati huu
kwa kufa msalabani. Hii ni sadaka ya kweli kwa njia mbili tofauti. Siku hizi
mbili, Alhamisi Kuu na Ijumaa Kuu zinahusiana kwa karibu. Katika Jumapili ya Pasaka ushindi wake juu ya
mauti unakamilika na maisha mapya yanapatikana kwa wote.
Basi, Ekaristi ni adhimisho ya mateso, kifo na ufufuko wa
Yesu. Uwepo wake ni hai, una nguvu, nao ndio ufanisi, yaani, una uwezo wa kutoa
matokeo. Katika Ekaristi Yesu hutenda kazi na kusababisha mabadiliko katika
maisha yetu. Kama hii, kwa Ekaristi tunabadilishwa kamili katika fumbo
tunaloadhimisha, kukubali ukweli wa Fumbo la pasaka kama “Pasaka ya Kristu katika
Pasaka yetu na Pasaka yetu katika Pasaka ya Kristo”. Hivyo Baada ya kila
adhimisho ya Ekaristi tuna changamoto ya kurudi shughuli zetu za kila siku kama
mashahidi wa Kristo anayetoa maisha yake kwa upendo ili watu wote wawe na uzima
wa milele.
Ee Yesu, tunakushukuru kwa utajiri wa Ekaristi.
Tunakushukuru pia kwa uzoefu wa udugu ambao tunaishi katika kila misa takatifu
ambayo sisi huadhimisha. Tunasadiki kwamba uwepo wako ni wa kweli na ufanisi
kati yetu na tunataka kufanya upya ahadi ya kuishi urafiki mwafaka na wenye
nguvu nawe, kutumikia wengine kwa ukarimu. Mfano wako wa unyenyekevu na utupu
utufanye kugundua ukuu wa utumishi wa ndugu. Amina.
Fr Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário