sábado, 30 de outubro de 2021

TUNAWEZA KUJIFUNZA KUPENDA

 

Kutafakari kutoka Kum 6:2-6; Waeb 7:23-28; Marko 12,28-34



 
 

    Amri zilizaliwa katika mazingira ya kuaminiana kati ya Mungu na watu wake: kwa upande wa Mungu Yeye ana kusudi la kuokoa ulimwengu wote na aliwakabidhi watu wa Israeli utume wa kuwa chombo cha wokovu wake kwa watu wote. Kwa upande wa watu, walikabidhi maisha yao kwa Mungu, wakipokea maagizo, ulinzi na tunza kama ishara halisi za upendo wa kimungu kwao. Kuishi Amri kulikuwa muhimu kwa watu hawa ambao wanafikiria Neno la Mungu kuwa ni Sheria na Sheria kuwa ni kama Neno la Mungu. Basi, kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno, kwa sababu Amri zinatoka moyoni mwa Mungu ambaye anapoongea anaongoza njia kamili ya maisha ya kweli. Kutii kwa Amri ni chanzo cha baraka ambayo huongoza kwa uzima, wakati kutotii kwa Amri kunaongoza kwa mauti.

    Basi, chanzo cha Amri ndio upendo wa Mungu. Yeye ni upendo na kupenda kwa hiari. Sheria yake ni Upendo. Sheria hii hailazimishi bali ndiyo zawadi na kuonyesha njia ya uhuru wa kweli. Hii ndiyo maana ya hotuba ya Musa kwa Watu wa Israeli katika somo la Kumbukumbu la Torati. Kupitia Musa, Mungu anaongea na Watu kutoka moyo kwa moyo, sababu Mungu anataka kuandika Sheria yake mioyoni mwa wote. Yeyote anaishi sheria ya Mungu kwa kweli ikiwa anaweza kupenda. Kumpenda Mungu kunamaanisha kuishi kulingana na mapenzi yake. Somo la pili kutoka Waraka wa Waebrania linaongea kuhusu ubora wa ukuhani wa Kristo kuliko ule wa Agano la Kale. Tofauti na makuhani wa Agano la Kale Yeye hahitaji kutoa dhabihu kwa ajili ya wenye dhambi kwa maana alijitoa nafsi yake mwenyewe kwa upendo na kwa sababu ya kujitolea kwake kamili alihakikisha wokovu kwa ajili ya wenye dhambi wote.

    Kwa kawaida mkutano wa Yesu na viongozi wa Kiyahudi ni maana ya mgogoro lakini katika nafasi hii mwandishi mkuu anayemwendea Yesu anaonekana kuwa wa kirafiki. Uthibitisho kuhusu hili ni kwamba katika mwisho wa mazungumzo kuna kubadilishana sifa na shukrani kutoka pande hizo mbili. Yeye alimuuliza Yesu kuhusu amri ya kwanza kati ya amri zote. Yesu hakujibu swali lake moja kwa moja bali akikumbuka “Shema Israeli” (Sikiliza, Israeli!), anatufanya kuelewa jambo muhimu la Sheria, yaani, upendo kwa Mungu na kwa jirani. Kuweka ukweli huu moyoni ni muhimu zaidi kuliko kukariri "amri" zote zilizozuliwa nao, kugeuza uangalifu kutoka kwa kile ambacho ni muhimu kweli.

    Amri ya kwanza inatufanya kuelewa kwamba hatuwezi kumpenda Mungu kwa njia yoyote bali kwa nguvu zote za maisha: kwa moyo, kwa nafsi, kwa akili na kwa nguvu. Na bado hautakuwa upendo wa kweli ikiwa hatumpendi jirani pia. Kwa maneno mengine, jibu letu kwa upendo uliotupenda unatolewa kwa pande mbili: Mungu na jirani. haiwezekani kuishi mmoja bila mwingine. Kuhusu hilo Mtakatifu Yakobo anasema: "Ndiye mwongo yeyote anayesema kwamba anampenda Mungu ambaye haoni na hampendi jirani ambaye anaona". Upendo kwa ndugu ni dhabihu ya kweli inayompendeza Mungu. Katika jibu lake, Yesu haongei kuhusu amri ya kutii bali uhusiano tunaopaswa kuishi. Ni lazima tutambue kwamba hii si kazi rahisi sana ya kuitekeleza. Kadiri tunavyoendelea maishani, ndivyo tunavyoona jinsi ilivyo vigumu kumpenda Mungu na jirani kikweli.

    Yesu alijua ugumu huo alipokuwa bado anayekana miongoni mwa wanafunzi wake. Kwa hivyo alijitolea kama mfano na msaada. Kutoka kwake, inakuwa kuzekana kumpenda Mungu bila kumpuuza jirani. Kwake, jambo la muhimu ni kupenda; kwa hivyo ataiita "amri mpya". Maneno haya hayamaanishi kwamba Yesu aliongeza jambo jipya, kwa kuwa amri ya kumpenda Mungu na kumpenda jirani ilikuwa tayari kabla yake. Basi, habari mpya iko wapi? "Iko katika ukweli kwamba maneno mawili haya yakuwa pamoja neno moja, ndiyo amri ya kipekee". Yule anayepata kutoa nafasi ya kwanza kwa upendo na kuufikiria muhimu ya yote alifahamu umuhimu wa sheria naye hayuko mbali na Ufalme kwa sababu anatenda kama Yesu. Kwa kweli, mtu ambaye anamfuata Yesu hafuati sheria au mafundisho bali anamfuata Mtu aliyetupenda mpaka upeo. Nasi tunaweza kujifunza jinsi ya kupenda vivyo hivyo.


Fr Ndega

 

Nenhum comentário: