Kutafakari kutoka Lk 9, 51-62
Baada ya
Petro kumkiri Yesu kama Kristu, aliye Masiya wa Mungu, Yesu aliwalika
Thenashara wote wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima. Yesu alitambua
kwamba walihitaji kujua zaidi kuhusu maana ya umasiha wake na kuyafahamu vizuri
mapendekezo yake. Kwa hivyo, alitumia wakati wa safari hadi Yerusalemu
kuwafundisha kamili. Mambo mengi yanatokea wakati wa safari hii na hayo yote
yalikuwa nafasi ya mafundisho, hasa kuhusu njia kamili ya kutenda mbele ya
kukataliwa. Safari kwenda Yerusalemu siyo safari ya kimwili tu bali ni hasa ya
kiroho. Mwanzoni mwa injili inasemekana kwamba “wakati siku za kupaa kwake
zilipokuwa karibu kutimia...” Basi, hii ni safari kuelekea mbinguni. Mti wa
Yerusalemu unafahamiwa kama “Mti wa Mungu” ulio makao ya dini ya kiyahudi.
Ingawa Yesu anajua kwamba mti huu ni mahali pa kuwaua manabii, kama ishara ya
upinzani kwa mavutio ya Mungu, hata hivyo anataka kwenda huko ili mapenzi ya
Mungu ya kuwaokoa watu wake yatimie.
Kwa kufika
mahali huko Yerusalemu ilikuwa lazima kupitia katika eneo la Samaria. Basi,
Yesu aliwatumia baadhi ya wanafunzi wamtangulie katika Samaria wamtengenezea
mahali pa kupumzika kidogo kwa sababu ya safari ya muda mrefu. Wanafunzi wa
Yesu walikuwa na mazoea ya kushughulika kwa mawazo na tabia tofauti na mwalimu
wao. Hii ndiyo maana ya kupatwa na hasira sana walipokataliwa wakipita katika
Samaria, na kutaka Mungu aliteketeze eneo hilo. Katika safari hii kwenye Yerusalemu
Yesu alikuwa akiwaongoza wanafunzi wake katika njia ya upatanisho na amani. Kwa
hivyo hakubali pendekezo lao na kuwapendekezea kwenda kijiji kingine, yaani,
njia nyingine. Kumfuata Yesu si rahisi sana. Wakati uliopita tulitafakari
kuhusu masharti matatu ya kumfuata kwa uaminifu, yaani, “kujikana mwenyewe,
kuuchukua msalaba wa kila siku na kumfuata Yesu.” Siku ya leo masharti
yanaendelea kuwa matatu, lakini hapo ni kama onyo, shauri. Yesu hataki
kuwadanganya wafuasi wake kupitia ahadi pasipo maana. Katika mapendekezo yake,
Yesu ni wazi sana. Yeye anauheshimu uhuru wa watu, lakini anayajulisha masharti
kwa wale ambao wanataka kumfuata. Vingenevyo hawatapata kumfuata kwa uaminifu.
Wanafunzi
wa Yesu walitaka kutenda kwa njia ya kibinafsi, yaani bila utambuzi na
kutafakari (ishara ya kutokwepo kwa Kristo moyoni mwao). Walikuwa waaminifu kwa
mwelekeo wa kibinadamu wa kisasi kuliko njia aliyopendezwa Yesu. Mwaliko waa
Yesu wa kuenda mahali pengine ni uthibitisho kwamba ni lazima kuheshimu uhuru
wa watu. Kumfuata Yesu ni kuchagua kuishi na kutenda tofauti. Mtu hawezi
kutazama nyuma ili aongozwe kulingana na hali ya zamani kukanusha utambulisho
mpya ulio matokeo ya mkutano na Kristo. Katika mwendo wa kumfuata Yesu mtu
anakuwa mtumishi wa ufalme wa Mungu. Katika mwendo huu masharti hayatoki kwa
mtu bali yatoka kwa Yesu. Kutazama nyuma kunaweza kuwa hatari kwa safari kwa
sababu katika safari hii muhimu sana sio tulichoacha nyuma bali tutakachopokea
mbele kwa sababu ya uamuzi wa kumfuata Yesu. Bila kujikana na kujinyima mtu
hawezi kumfuata Yesu na kupata uzima.
Yesu halazimishi uhuru wa wanafunzi wake,
lakini anaanzisha masharti ili waweze kumfuata kweli. “Kama wafuasi, wakristo
tunaweza kukosa uvumilivu na kuwadharau watu wa makanisa, dini na imani
nyingine. Kama Wayahudi na Wasamaria, Wakristo wa Afrika kutoka makabila
mbalimbali wanaweza kuwa na chuki kubwa kati yao, kiasi cha kushiriki katika
mapigano ya kikabila. Huu siyo mwelekeo wa Yesu.” Kutokana na mfano wa Kristo, anayeitwa pia mtu
asiye na ukatili, njia ya kipekee ya kuushinda ukatili ni kujibu kwa ishara za
amani. Yesu anataka kwamba tabia zetu zishinde mwelekeo wa jamii kwenye kisasi,
ukatili na ukabila. Ukabila unauharibu undugu, kukanusha utambulisho wetu wa
wakristo. Yesu anatualika kufahamu kuwa uovu hauwezi kuondoa uovu, bali ni wema
tu unaoweza kufanya hivi. Ekaristi hii takatifu itusaidie kupenda kama Yesu
alivyo na, kupitia upendo huu, tuweze kuijenga jamii inayotarajiwa na Mungu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário