Kutafakari kuhusu Mt 6, 24-34
Kifungu
hiki cha injili ni andiko la msingi wa kiroho ya Mt. Yohane Calabria. Huyu ni mwanzilishi wa Shirika letu, yaani, Poor
Servants of Divine Providence. Alianza kuwajali watoto maskini na yatima kwa sababu
alitambua kwamba tendo hili lilikuwa mapenzi ya Mungu. Nambari ya watoto
iliongezeka daima na vyakula havikutosha kwa wote. Lakini Mungu aliyekuwa
makini sana kwa hali hii, akapatia daima yale ambayo Yohane Calabria na watoto
waliyahitaji kwa kuishi. Hali hili ilidhihirisha maneno ya injili ambayo tunatafakari.
Kwa upande wa Mungu, yeye anajua kwamba tunahitaji
mambo hayo yote. Kwa upande wa binadamu ni
lazima kuwa na imani na kujisalimisha mikononi mwa Mungu ambaye ni Baba na
Mtoaji. Mtakatifu Yohane Calabria alikuwa na uhakika kuhusu hali hii kwa sababu
“aliishi injili na kwa injili”. Kupitia Injili aliugundua ubaba wa Mungu kwa
njia halisi sana. Ugunduzi huu mkubwa ulisimuliwa na Askofu aliyeitwa Chiot
kutoka Jimbo la Verona - Uitalia ambaye alitembelewa na Mt Calabria kwa kumjulisha
kuhusu tukio muhimu. Huu ni msukumo katika safari yetu kama watoto wa Mungu.
“Usiku
mmoja, padre Calabria aliandika na kuituma barua kwa baba askofu Chiot akisema,
“ningojee kesho saa nne asubuhi maana nahitaji kuongea nawe. Wakati padre
Calabria alipofika nyumbani mwa Askofu Chiot, baba huyo alimwuliza swali: Je, bahati
mbaya gani ilitokea? Barua yako ilinisumbusha. Padre Calabria akamwambia, “hapana
bahati mbaya; hili ni jambo la ajabu.” - “La ajabu!”, aliuliza baba Chiot. Naye
padre Calabria aliendelea kwa kusema, “Alisoma injili nzima!” Baba askofu
alisema, “Hili si jambo la ajabu!” Je, inawezekana kuwepo padre ambaye hajasoma
injili nzima?” Padre Calabria alisema, “Tafadhali, niruhusu kueleza. Mimi pia
nimekwisha soma na kuihubiri injili, lakini juzi baada ya kuishi kwa ugumu
mchana kutwa na bila kupata utulivu kwa kulala usingizi, nilichukua inijili na
kuisoma nzima pamoja na kitabu cha Matendo ya Mitume. Nilipata kusoma kila kitu
kwa usiku mmoja peke yake. Jambo hili lilisababisha uzoefu wa ajabu maishani
mwangu. Kweli injili ni jambo kubwa! Nimestaajabia. Hebu, sikiliza! “Msiwe na
wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili
yenu, mtavaa nini. Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au
kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi.
Lakini nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa kama
mojawapo ya hayo maua.”
Padre Calabria ailikuwa amesisitiza yaliyomhakikishia
maana ya kweli ya kuishi na kutangaza, yaani Mungu ni Baba nasi tu watoto wake.
Alichukua kama ahadi na mpango wa maisha kwake na kwa shirika lake zima maneno
ya mstari wa 23, yaani, “Mtafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na hayo
yote mtapewa kwa ziada.”
Je, Maneno haya yana maana gani katika safari yetu siku
ya leo? Kulingana na Yesu hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili, yaani Mungu na mali. Mali inaweza
kuvuruga uangalifu wetu kwenye njia ya Mungu ya kutenda na kuwajali watoto
wake. Yesu hakanushi kwamba
sisi tunahitaji mambo mengi.
Lakini anajua kwamba kosa la utambuzi linatuongoza kuishi kwa wasiwasi na
kusumbukika kuweka uangalifu katika yale yasiyo muhimu sana.
Kulingana na mafundisho tumepokea kutoka kwa Yesu Mungu
ni Baba kabla ya kuwa Muumba. Yeye si kama baba yeyote bali yu Baba Mwema
ambaye anashughulika sana na hali ya wana wake. Yeye
analinda na kutunza bila kulala. Yeye anajua mahitaji ya wana
kabla ya wamwombe kitu. Kwa utunzaji wa upendo Mungu anashiriki
zawadi zake na wana wake, kutarajia kwamba tufanye vivyo hivyo kwa ajili ya
wengine ili undugu kati yetu uwe maonyesho ya ubaba wake. Matatizo yote yapaswa kufikiriwa na kusomeka kwa maelewano na
ubaba wa Mungu.” Mungu hamsahau hata mmoja wa wana wake.
Tunaalikwa kumwelekea kwa imani na kuwa
na uhakika kwamba tumepokea sana. Mungu hatupatii daima yale tunayomwomba, bali
anatupatia daima tunayohitaji. Ikiwa hatupokei yale tunayomwomba yeye ni kwa
sababu hatuombi ipasavyo. Tufanye upya imani yetu katika riziki yake kuwa na
tabia kamili katika ushusiano wetu naye.
Fr Josuel Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário