Tafakari kutoka Zek
12,10-11:13,1; Wag 3,26-29; Lk 9,18-24
Katika somo
la kwanza Bwana aliahidi kuwafanya watu wake wenye unyeti kwa kuwapa roho ya
huruma na dua. Bila aina hii ya roho hakuna mtu anayeweza kukiri udhaifu wake,
kumwomba Bwana huruma yake na kupata maisha mapya iliyo matokeo ya tendo la
Mungu maishani mwake. Kulingana na somo la pili utambulisho wetu ni kuwa wana,
yaani wana wa Mungu na kwa hivyo, kuwa ndugu wa watu wengi kwa sababu ya utume
wa Kristo ambaye alitufanya kuwa wamoja, ingawa sisi tu tofauti. Ubatizo wetu
ni ishara halisi ya hali hii ambayo tunaunganishwa na Kristo na katika Kristo
ili tuweze kuishi kwa ushirika kuhisi uchungu na furaha za wana wengine wa
Mungu kwa sababu sisi tu watu wa Kristo.
Katika
injili, kabla ya kufunua jambo muhimu kwa wanafunzi wake na kuwauliza swali la
msingi, Yesu alikuwa akisali. Mara nyingi injili zote zinamjulisha Yesu akisali
kama alama ya ushirika wake na Baba na pia kama maonyesho ya umuhimu wa tukio
lifuatalo. Ushuhuda wa sala kutoka kwa Yesu ni msukumo/msaada ili wanafunzi
waweze kuelewa kwamba hakuna njia nyingine kwa uaminifu katika safari ya wito
ila kupitia sala. “Lililo kweli kwa Yesu nila kweli pia kwa kila mtu. Ni katika
mazungumzo ya moyoni na Mungu, ninapokubali kuhojiwa naye na hata wengine, na
kisha kujikubali nilivyo mwenyewe... Ni pale tu tunapokuwa na mawasiliano na
Mungu kwa njia ya sala ndipo tunapoanza kujielewa tulivyo.”
Ingawa Yesu
anajua mtazamo wa watu kumhusu yeye, alitaka kuwauliza wanafunzi wake maswali
kama nafasi nzuri ya kuwafundisha vizuri kuhusu utambulisho wake wa Masiha wa
Mungu. Jibu la kwanza la wanafunzi linadhihirisha kwamba watu hawakuwa na wazo
kamili/wazi kuhusu Yesu na wakaridhika kwa kumlinganisha na manabii wa zamani.
Kwa maneno mengine walikuwako mbali na matarajio ya Yesu. “Kumwita Yesu nabii
ni nusu tu ya ukweli wote. Manabii huandaa njia kwa ajili ya mtu mwingine. Lakini
Yesu pekee ndiye ambaye njia yake iliandaliwa na manabii wengine wote.” Kupitia
jibu la pili, Petro pamoja na wengine walitambua umasiha katika Yesu, lakini
hawakuwa na wazo kamili kuhusu umasiha wa Yesu. Maana ya kufikiri hivi ni kwa
sababu ya mawazo yao ya kiyahudi. Kulingana na mawazo hayo Masiha wa Mungu
anapaswa kuwa shujaa na mwenye nguvu ili aweze kuwakomboa watu wa Israeli
kutoka utawala wa Roma. Kwa maneno mengine walikuwa na mawazo ya upungufu
kuhusu utambulisho wa Yesu kama Masiha wa Mungu. Yesu aliwataka kama wanafunzi
wake lakini haiwezekani kuwa wanafunzi wa Yesu kwa njia yoyote. Maana tofauti
ya umasiha na ile ya mwalimu ni hatari Ili wafikie mafanikio katika safari yao.
Kisha, Yesu
aliamua kuwaeleza maana ya umasiha wake kwa kusahihisha mtazamo wao. Umasiha
aliochagua Yesu ni umasiha wa mtumishi wa Bwana ambaye alijiona kupakwa mafuta
ili atangaze wokovu wa wa Mungu kupitia kukataliwa, mateso, kufa na kufufuka
kwake. Njia ya utukufu wa masiha huyu inatokea kupitia njia ya utupu na
unyenyekevu. Yesu anapendekeza njia hii kwa wote ambao wanataka kumfuata kwa
uaminifu. Kwa maneno mengine Kristo anaujulisha msalaba kama njia ya utukufu.
Utambulisho wa wanafunzi na mwalimu Yesu kunatokea kupitia hali ya msalaba wa
kila siku.
Kristo ambaye tunamfuata anajua vizuri hali yetu naye alichukua
changamoto nyingi za kila siku hadi msalaba kama kilele. Kwa upande wa Kristo
msalaba ulikuwa sehemu muhimu katika mwendo wa kufanya mapenzi ya Mungu na
kudhihirisha mpango wa upendo wake. Kwa upande wetu kama wanafunzi msalaba wa
kila siku ni ishara ya utayari wetu kwa kuruhusu kuongozwa na Mungu na
kukaribisha mapenzi yake kwa maisha yetu. Kwa kufikia lengo hili tunapaswa
kujikataa na kujisahau wenyewe ili wengine waweze kukumbukika. Tunapaswa
kujikataa wenyewe ili Mungu aweze kujifunua kwa nguvu yote ya upendo wake.
Kujiondoka kutoka katikati/mahali muhimu ili wengine waweze kuwa na nafasi
zaidi. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuwafikiria wengine kuwa wamuhimu zaidi
kuliko sisi wenyewe. Kama haiwezekani kumfuata Kristo bila msalaba, mfano wake
wa uaminifu kwa mpango wa Mungu utuimarishe ili tuchukue msalaba wetu wa kila
siku, kumfuata kwa uaminifu na kufanya mapenzi ya Mungu.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário