Kutafakari kuhusu Yoh 13, 31-35
Umuhimu wa liturjia ya siku ya
leo ni amri ya upendo kama Yesu alivyofundisha. Kila kitu ambacho tunatenda
kinapaswa kuwa alama ya upendo. Tendo bila upendo halina maana. Mtume Paulo
aliliweka wazi jambo hilo: “Pia nikiwa na unabii, na kujua mafumbo yote na
maarifa yote, na kuwa na imani yote hata kuhamisha milima, nikikosa upendo,
sina maana” (1 Wakorintho 13:2).
Mazingira ya andiko la siku ya
leo ni ya karamu ya mwisho ambayo Yesu alianzisha Ekaristi iliyo sakramenti ya
upendo na utumishi. Yesu alijua wazi kwamba Saa yake ilikuwa imefika. Katika
injili ya Yohane, kila ishara ambayo Yesu anatenda ni tangazo kuhusu Saa hii
ambayo inajumuisha mateso, kifo na kufufuka kwake. Kupitia Saa hii atamtukuza
Baba na kutimiza utume wake. Kwa upande wa wanafunzi wa Yesu, Saa hii ni
kipindi cha uamuzi, yaani, wanapaswa kuamua ikiwa wanataka kuendelea kazi ya
mwalimu au la. Mwinjilisti Yohane alitaja wakati kamili ambao Yuda alitoka
mahali pa mkutano na wakati wa kumtukuzwa kwa Yesu na Baba yake. Yuda alitoka
kwa sababu mbele ya ishara ya kujisalimisha kwa Yesu haiwezekani kutofautiana. Yesu
alimsaidia Yuda kuamua kwa sababu, ingawa Yuda alikuwa mmojawapo wa kikundi,
yeye ndiye alimpinga Yesu. Naye Yesu mwenyewe alikuwa amekwisha tangaza kwamba
yeyote asiyetenda pamoja naye anagawa. Basi, kupatikana na hatia kwa Yesu
kulikuwa msaada kwa uamuzi wa Yuda. Yeyote anayekubali pendekezo la Yesu ndiye
anabadilishwa na upendo wake na kualikwa kufanya vivyo hivyo. Yeyote anayekataa
hili anapaswa kuondoka mahali na kukiacha kikundi.
Mazungunzo ya Yesu na Yuda na
kuondoka kwake kulikwa maandalizi kwa kipindi kifuatacho cha zawadi kubwa ya
amri mpya kama urithi wa Yesu kwa watoto wadogo wake. Yesu alikuwa akizungumza
nao kama vile mama na baba wanavyofanya na watoto wao. Yeye alishiriki nao
hisia zake na kitu muhimu sana, yaani, amri mpya ya upendo. Kwa upande wa
wanafunzi amri hii siyo amri mpya kwa sababu imekwepo tangu Agano la Kale.
Lakini wanapaswa kuishi kwa njia mpya, kulingana na hayo aliyowafundisha Yesu.
Basi, pamoja na zawadi kubwa ya amri hiyo Yesu aliwaonyesha jinsi ya kuishi zawadi
hii. Kipimo cha upendo wao kinapaswa kuwa upendo wa Bwana wao. Nayo njia yao ya
kupendana inapaswa kuwa njia ya kupenda aliyochagua Yesu.
Yesu anawapenda wanafunzi wake mpaka
upeo, kwa sababu hajui kupenda kwa njia nyingine. Ilikuwa kwa upendo kwamba
Mungu alimtoa Mwanawe pekee kwa wokovu wa ulimwengu. Upendo tu uliimarisha kazi
yake katika nyakati zote. Ilikuwa kwa upendo kwamba Mwana wa Mungu aliutoa uhai
wake. Umuhimu wa mafundisho yake ni upendo kama amri mpya na maana ya
utambulisho wa wanafunzi wake. kupitia kupendana wao kwa wao kama Yesu
alivyowapenda watu wote watawatambua kama wafuasi wa Yesu. Upendo wa Yesu ni
alama ya furaha yake, yaani, furaha ya ushirika wake na Baba, furaha ya kuishi
miongoni mwa binadamu, furaha ya kuwachagua baadhi ya wanadamu kama washirika
katika kazi yake na furaha ya kuutoa uhai kwa ajili yao. Akiushiriki upendo na
wafuasi wake, Yesu aliyajaa maisha yao kwa furaha kubwa, maana kati ya upendo
na furaha uhusiano uko. Mtu anayependa kwa kweli yu mwenye furaha ya kweli.
Ilikuwa kutokana na mfano wa
unyenyekevu na utumishi kwamba Yesu aliwapa wafuasi wake amri yake mpya. Huu ni
ushuhuda wetu wa kwanza kulingana na uzoefu wa wakristo wa kwanza, yaani,
“Mwone kama wanavyopendana!” Upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao,
kushiriki pamoja, mshikamano, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa
moyo. Tunaalikwa kuchukua hayo kama mpango wa maisha. Upendo unapaswa kuwa
umuhimu kati yetu na maana ya kazi zetu. Kupitia kupendana tunaalikwa kujitolea
kama vile Kristo na kuwafanya wanafunzi wapya kwake. Kupitia kupendana tunakuwa
wajumbe wa habari njema kwa wote. Kupitia upendo twatambua kwamba hatutendi
peke yetu bali kwamba sisi tu vyombo mikononi mwa Bwana ambaye ana nguvu kwa
kubadilisha kila kitu tena na tena kupitia upendo.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário