Mit 8: 22-31; Rum 5:
1-5; Yoh 16,12-15
Tunaadhimisha
sikukuu ya Utatu Mtakatifu. Utatu Mtakatifu ni fumbo la Mungu aliye ushirika wa
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hii ni Jumuiya ya umungu na ukamilifu. Utatu
Mtakatifu ni ushirika wa upendo kwa maana Mungu ni upendo. Upendo ni asili ya
Mungu. Hivyo, “Mungu ni Utatu kwa sababu ndiye upendo”. Mungu alitaka kuwa
familia ili ashiriki upendo na uhai wake. Yeye ni Mungu wa kipekee lakini
haishi peke yake kwa sababu alitaka kuwa na kuishi katika familia. Uumbaji wote
ni uenezi wa nafsi yake na fumbo lake. Viumbe vyote vinaitwa kuingia katika
mwendo huu wa upendo na kuwa maonyesho ya wema wake. Tumsifu Mungu kwa ushirika
wake wa upendo, atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu...
Tunaposema
ishara ya msalaba, yaani, “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”,
tunaongea kuhusu Mungu wa ukweli, ambaye yupo hapa na katika kila mahali. Yeye
yu upendo aliye juu ya vyote na ndani ya vyote. Hadithi fulani inatusaidia
kulikaribisha viizuri mwendo huu, yaani “Siku moja Mtakatifu Agostino, aliye
mchungaji na mwalimu wa kanisa, alikuwa akitembea katika pwani ya bahari,
akijiuliza swali kuhusu fumbo la Utatu Mtakatifu, akisema, “inawezekanaje Mungu
kuwako kama Mmoja na Utatu wakati huo huo? Ghafla, alimwona mtoto mdogo
aliyefanya shimo katika mchanga na kukimbia kuenye bahari, akichukua maji
kidogo na kuyaweka shimoni. Baada ya kuangalia mchezo huu wa mtoto mdogo kwa
mara nyingi, Agostino aliamua kumwuliza maana ya mchezo huo. Mtoto mdogo
akamjibu akisema: “Najaribu kuweka maji yale yote ndani ya shimo hii”. Ameshangaa
sana, Agostino akasema: “Hutapata kufanya hivyo kamwe!” Kisha, mtoto mdogo akamwambia
akisema: “ni rahisi kwangu kuyaweka maji yale yote shimoni kuliko wewe upate
kufahamu fumbo la Utatu Mtakatifu kwa akili yako. Mwishowe, mtoto mdogo alitoweka
na Mtakatifu Agostino akajiambia: “Labda mtoto huyo angekuwa malaika!”
Hadithi hii
inatufundisha hali muhimu sana, yaani, fumbo la Utatu mtakatifu si fumbo la
kufahamiwa bali la kukaribishwa. Ikiwa tunajifungua zaidi kwa fumbo hili
tunaweza kuhisi zaidi fumbo hili ndani yetu. Ujumbe wa masomo ya siku ya leo
unatusaidia katika mwendo huu. Katika somo la kwanza hekima alijidhihirisha
kama nafsi ya Mungu. Hekima hii yu Yesu Kristo ambaye alikuwako na yuko pamoja
na Mungu milele na kufanya kazi naye kabla ya kuumbwa chochote. Yeye ni nafsi
ya pili ya Mungu na viumbe vyote vilivyokuwako viliumbwa kwa njia yake, pamoja
naye na ndani yake. Yeye ni ukamilifu wa viumbe vyote. Bwana wetu Yesu Kristo
alitushirikisha katika utukufu wa Mungu. Kupitia yeye tulipewa Roho Mtakatifu
ili tuishi kama watoto. Tendo la Roho huyu limemimina mioyoni mwetu pendo la
Mungu kuthibitisha kwamba sisi ni watoto wake na tunaweza kumwita Baba yetu kwa
uhuru kabisa. Ikiwa sisi ni watoto sisi pia ni warithi pamoja na Yesu kuhusu
zawadi sawa, yaani, ushiriki katika uhai wa Mungu pia. Ushiriki huu unawezekana
kupitia ubatizo. Tulipobatizwa tulikuwa hekalu hai la Mungu, makao ya Utatu
Mtakatifu.
Umuhimu wa
ujumbe ambao Yesu ametukabidhi ni kwamba yeye ndiye ukweli wa Baba katika Roho
Mtakatifu. Hao ni Utatu na hutenda pamoja kwa ushiriano kamili. Yesu,
aliyetumwa na Mungu Baba, alitangaza ukweli akiwahusisha watu katika ushirika
mmoja ambao anaishi na Baba na Roho Mtakatifu. Utimizaji wa ahadi kuhusu ujio
wa Roho huyo unatuhakikishia umoja wetu, kutunganisha kama wana wa familia moja.
Kupitia Roho huyo tunaangazika ili tuweze kukumbuka mafundisho ya Yesu na
kuyatangaza kwa uaminifu. Wakati sisi hupendana tunaonyesha ukweli wa uhusiano
wetu na Mungu aliye Utatu Mtakatifu. Tunapoishi uhusiano wa kweli na Yesu vivyo
hivyo tunahisi ndani yetu tendo la Baba na Roho wake. Uzoefu wetu wa Yesu
katika Ekarist ni uzoefu wa Utatu Mtakatifu. Mungu anatumikia, yeye yu kati
yetu na ndani yetu; anatuunganisha naye na miongoni mwetu. Hili ni fumbo la
ushirika ambao Mungu ametuhusisha kwa maana anataka tuwe washiriki katika uhai
wake mwenyewe. Kwa hivyo tuombe, atukuzwe Baba na Mw...
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário