quinta-feira, 4 de junho de 2015

USHIRIKA KWA UPENDO


Kum 4: 32-34, 39-40; Rum 8: 14-17; Mt 28: 16-20

       Tunaadhimisha sikukuu ya Utatu Mtakatifu. Utatu Mtakatifu ni fumbo la Mungu katika Watatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Jumuiya ya umungu na ukamilifu. Utatu Mtakatifu ni ushirika wa upendo kwa maana Mungu ni upendo. Upendo ni asili ya Mungu. Hivyo, “Mungu ni Utatu kwa sababu ndiye upendo”. Mungu alitaka kuwa jumuiya ili kushiriki upendo na uhai wake. Yeye ni wakipekee bali haishi peke yake kwa sababu alitaka kuwa na ushirika. Uumbaji wote ni uenezi wa kuwa kwake na fumbo lake. Wote wanaitwa kuwa maonyesho ya upendo na wema wake. Tumsifu Mungu kwa ushirika wake wa upendo, atukuzwe Baba na Mwana na... 

       Tunaposema “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu”, tunaongea kuhusu Mungu wakipekee na usawa, ambaye yupo hapa na kila mahali. Yeye ni mbali sana lakini yu pia karibu sana nasi. Hilo si fumbo kufahamiwa bali kukaribishwa. Hadithi fulani inaweza kutusaidia katika mwendo huu, “Siku moja Mtakatifu Agostino alikuwa akitembea kwa kuambaa pwani, akijiuliza maswali kuhusu fumbo la Utatu Mtakatifu, “inawezekanaje Mungu kuwa Mmoja na Mtatu kwa wakati sawa? Ghafla, aliangalia mtoto mdogo aliyefanya shimo katika mchanga na akakimbia mpaka bahari, akachukua maji kidogo, akarudi na akaweka maji shimoni. Baada ya ameangalia mchezo huu wa mtoto mdogo kwa mara nyingi, Agostino aliamua kumuliza maana ya mchezo huo. Mtoto mdogo akamjibu akasema: “Najaribu kuweka maji yale yote ndani shimo hii”. Alishangaa, Agostino akasema: “Bali isiowezekana!” Kisha, mtoto mdogo akajibu akasema: “ni rahisi zaidi kwangu kweka maji yale yote shimoni humu kuliko wewe kupata kufahamu fumbo la Utatu Mtakatifu na akili yako. Hatimaye mtoto mdogo alitoweka na Mtakatifu Agostino akajiambia: “Labda mtoto mdogo huyo angekuwa malaika.”

       Hadithi hii inatuandaa ili kuukaribisha ujumbe wa masomo ya siku ya leo. Somo la kwanza ni mwaliko kwa utambulisho wa ukuu na nguvu ya Mungu. Anaitumia nguvu yake ili kutenda matendo mazuri kwa maisha ya watu wake, mali yake. Mbele ya uaminifu na utunzaji wa Mungu watu wanaalikwa kuifuata miongozo yake kwa sababu hiyo ni maonyesho ya upendo wake na kigezo ili kuhifadhi maisha yao. Ujumbe wa Somo la pili ni sehemu ya kiroho kilichositawi na Mtakatifu Yohana Calabria. Kulingana na somo hili, Baba wa Yesu ni Baba yetu pia. Ametupa Roho wake Mtakatifu ili tuishi kama watoto. Kitendo cha Roho huyu Mtakatifu ndani yetu kinathibitisha kwamba sisi ni watoto wake na tunaweza kumwita Baba yetu kwa uhuru jumla. Ikiwa sisi ni watoto sisi pia ni warithi na Yesu kuhusu zawadi za umungu sawa, ni kwamba, ushiriki katika uhai wa Mungu pia. Ushiriki huu unawezekana kupitia ubatizo. Tulipobatizwa tulikuwa hekalu hai la Mungu, makao wa Utatu Mtakatifu. Kama alivyowatokea na wanafunzi wa kwanza, Yesu ameshiriki mamlaka yake nasi, kutufanya washiriki katika fumbo la uhusiano wake na Baba na ametutuma kama wajumbe wa habari njema hii.     


        Umuhimu wa ujumbe Yesu ametukabidhi ni kwamba yeye ndiye ukweli mmoja na Baba wake na Roho wake Mtakatifu. Wao ni pamoja na wanatenda pamoja kwa ushiriano kamili. Uhusiano huu usiofungwa katika wenyewe bali ni mwaliko kwa ushiriki. Familia ya binadamu ilizaliwa kutokana na fumbo hili na jumuiya zetu lazima kufuata kielelezo hiki ili kuwa na uwepo ufanisi katika jamii. Wakati sisi hupendana tunaonyesha nguvu za uhai kutokana na Utatu Mtakatifu. Tunapouishi uhusiano wa ndani na Yesu sisi ni karibu na Baba na Roho Mtakatifu kwa njia sawa. Uzoefu wetu wa Yesu katika Ekarist ni uzoefu wa Utatu. Mungu anatumikia, yeye ni karibu nasi na ndani yetu; anatuunganisha naye na miongoni mwetu wenyewe. Hilo ni fumbo la ushirika ambao tunahusishwa kama washirika katika uhai wake. Kwa hivyo tuombe Atukuzwe Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu...

Fr Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: