Kutafakari
toka Kutoka 24: 3-8; Ebr 9: 11-15; Mk 14: 12-16, 22-26
Siku ya leo tunaalikuwa kuadhimisha sikukuu ya Mwili
na Damu ya Kristu, fumbo la imani yetu. Hii ni nafasi maalum kuonyesha shukrani
yetu na upendo wetu kwa zawadi kuu ya Ekaristi takatifu. Hii ni siku ili
kutafakari kuhusu uwepo wa kweli wa kristu katika maumbo ya mkate na divai. Ekaristi
takatifu ni fumbo la kujisalimisha kwake kwa upendo kwa wokovu wa ulimwengu. Ekaristi
ni adhimisho la fumbo la Mungu ambaye anatumikia, yupo karibu nasi na ndani
yetu. Hilo ni fumbo la ushirika ambao tunahusishwa kama washirika katika uhai
wake. Ekaristi ni sakramenti ya Agano jipya na milele kupitia hilo Kristu
anatuunganisha naye na miongoni mwetu wenyewe kama wana wa watu wapya wa Mungu,
Kanisa.
Masono ya leo yanaongea kuhusu hali halisi hii. Kulingana na somo la kwanza, umuhimu wa agano ambalo Mungu anaanzisha na
watu wake ni Amri kumi. Amri ni mwongozo, zawadi zake Mungu kwa watu ili waishi
kulingana na matarajio yake. Musa ni mpatanishi mwema ili maneno ya Mungu
yatangazwe kwa watu kikamilifu yakiwahamasisha kuchukwa Amri hizi kwa uaminifu.
Damu ya wanyama waliomchinjia Mungu ikanyunyizwa
juu ya watu ikithibitisha ahadi ya kubadilishana kati ya Mungu na watu wake. Somo la pili linaongea
kwamba Yesu
ni Kuhani wa agano jipya na milele. Ukuhani wake ni mkubwa zaidi kuliko ukuhani wa agano la kale kwa sababu una asili ya Mungu. Yeye hakuhitaji kumtolea Mungu sadaka, bali alijitoa
kama sadaka kamili na, kupitia damu yake alipata wokovu kwa ubinadamu wote.
Hali halisi ambayo Injili linatutafakarisha ni
Ekaristi ambayo ina mizizi katika ibada
ya Wayahudi. Yesu alitaka kusherehekea pasaka na wanafunzi wake. Basi, akihisi wenye uhuru kabisa, "Alitwaa mkate, akashukuru, akaumega,
akawapa...” “Kisha akatwaa kikombe akifanya vivyo hivyo na wote wakakinywea”. Vitendo
hivi vya Yesu na wanafunzi wake vilivyofanyika katika hali ya familia na
kujiamini, vilikuwa mwaliko wa uzoefu wa kushiriki pamoja na makubaliano. Mkataba
kati ya Mungu na watu wake katika agano la Sinai ulishindwa na Yesu ambaye
alifanya mkataba mpya, Agano jipya kati ya Mungu na Watu wake wapya - ambalo ni Kanisa. Akitumia Ibada ya Wayahudi, Yesu alianzisha Ibada mpya,
ni kwamba, Mlo wa Ekaristi, akitangaza kwa Wafuasi wake ukombozi kamili ambao
ulikuwa ukija na kwamba alitamani kwa shauku kushiriki na rafiki zake. Katika
karamu hii ya mwisho, Yesu alijitoa kama chakula na kinywaji, akionyesha maana
ya kujisalimisha kwake kwa uhuru na kwamba pia lazima kuwa tabia ya maisha ya
wafuasi wake. Wao lazima kuendelea mwendo huu kwa kumkumbuka Yesu.
Hili
ni fumbo la imani yetu: tunaalikwa
kuadhimisha fumbo la Mwili na Damu ya Kristu kwa upendo na unyenyekevu na
kumjua Mungu kama yeye ndiye. Hili ni Fumbo la Paska, ambalo linajumuisha
mateso, kifo na ufufuko wa Yesu. Yeye alianzisha Ekaristi akiutoa mwili na damu
yake katika ibada, akiandaa wanafunzi wake kwa kujisalimisha kwake msalabani.
Katika sakramenti hi jumuiya ya kikristu inaalikwa kuhisi mmoja na Kristu, kuchukua
naye tangazo la ushindi wake juu ya mauti ambao unakamilika na maisha mapya
yanapatikana kwa wote.
Katika Ekaristi uwepo wa
Yesu ni hai, wenye nguvu, una maana ufanisi, wenye uwezo wa kutoa matokeo
mazuri. Yesu katika Ekaristi huleta mabadiliko katika maisha yetu. Kama hii,
katika Ekaristi tunabadilishwa katika fumbo tunaloadhimisha, kukubali ukweli wa
Fumbo la pasaka kama “Pasaka ya Kristu katika Pasaka yetu na Pasaka yetu katika
Pasaka ya Kristo”. Hivyo baada ya kila adhimisho ya Ekaristi tuna changamoto
kurudia shughuli za kila siku kama mashahidi wa Kristo anayetoa maisha yake kwa
upendo kwa wote kuwe na maisha kamili. Basi, tumshukuru Mungu kwa uzoefu wa
udugu tunaoishi katika kila misa takatifu tunayoadhimisha. Ili tuweze kulima uhusiano
wa ndani na Yesu ili kutumikia wengine kwa ukarimu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário