Kutafakari kutoka Ezekieli 17:
22-24; 2Wakorinto 5: 6-10; Marko 4: 26-34
Umuhimu wa liturujia hii ni uwepo kimya na ufanisi wa ufalme
wa Mungu miongoni mwetu. Mungu anafanya kila kitu kwa wema wetu na anatarajia
imani yetu kijumla katika kitendo chake. Somo la kwanza linaongea kuhusu hali
ya utumwa wa Babeli katika mwaka wa 597 K.K. na linamzawadisha Ezekieli kama
mmoja wa manabii aliyewaandama watu wa Israeli katika kipindi hiki kigumu. Watu
hawakuwa na matarajio ya ukombozi, na Ezekieli aliwahamasisha kama mjumbe wa
Mungu. Kulingana na nabii huyo, Mungu hakusahau watu; yeye yupo miongoni mwao
na atawaokoa, akiwaletea maisha mapya na akiwafanya rejea kutangaza wema wake
kwa mataifa yote. Katika mwendo huu wa ukombozi watu ni kama mmea mdogo utaokuwa
mti mkubwa. Basi, Mungu atachukua watu wake waliodhulumiwa na walioaibishwa, atawainua
kama chombo cha wokovu wake. Njia hii ya kutenda kwa Mungu inakumbukika katika
wimbo wa Bikira Maria: “Bwana amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya
enzi, na akawakweza wanyenyekevu”.
Kulingana na Mtakatifu Paulo, sisi ni kama wageni, watu
waliohamishwa ulimwenguni huu, mbali sana kutoka makao yetu penyewe. Sisi ni wa
Mungu na hatuwezi kushikiliwa kwa ulimwengu huu, kwa sababu zawadi kuu ya imani
tumepokea kutoka kwake inautoa mwelekeo kamili wa maisha yetu ili tufikie
marudio salama katika Mungu mwenyewe. Zawadi ya imani inatuhamasisha kuchukua
utambulisho wetu wa kikristu kwa uhusiano wa ndani na Kristu ambaye anatungojea
ili kutuza kila mtu kulingana na chaguzi ambazo tumefanya katika dunia hii.
Sisi sote tunaalikwa kwa maisha mapya yanayoweza kufikika kupitia neema ya
wokovu wa Mungu katika Kristu na juhudi ya kufanya mema wakati tuko katika
maisha haya.
Katika injili Yesu anaongea kwa watu kutumia mifano ili
kutueleza nguvu ya Ufame wa Mungu. Mfano wa kwanza ni kuhusu mbegu ambao unaota
na unakua kwa nguvu wenyewe; ushirikiano wa binadamu ni kuutawanya tu, na
kusubiri kwa mavuno ili kukusanya matunda. Wa pili ni kuhusu udogo wa kipimo
cha mbegu ya haradali na ukuu wa matokeo yake. Kwa nini Yesu aliongea kwa watu
akiitumia mifano? Chaguo la Yesu kwa njia hii ya lugha ni kwa sababu ya
utambulisho wake na hali halisi ya watu wanyenyekevu na maana pia ni rahisi
zaidi kwa ufahamu wao. Kama hii alifanya kufikika mafumbo makubwa ya Ufalme wa
Mungu kwa wanyenyekevu. Hiyo ni njia iliochaguliwa na Mungu kutenda, akisababisha
mchafuko kwa wenye uwezo na wenye nguvu, na akidhihirisha mafumbo yake kwa
wanyenyekevu na maskini.
Katika ujumbe wake, Yesu hakujitangaza; yeye aliutangaza
Ufalme wa Mungu. Ufalme ni wa umuhimu katika ujumbe wake. Kulingana na Yesu,
hali na nguvu ya Ufalme wa Mungu inategemea juhudi ya binadamu, bali kitendo
cha neema ya Mungu inayotolewa bure. Kila mtu anaalikwa kufanya bora mwenyewe
ili kushirikiana kwa ongezeko la Ufalme wa Mungu duniani, lakini aliyekabidhiwa
kabisa katika kitendo cha Mungu. Kama hii alifanya Mt. Yohana Calabria, akitafuta
kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake kupitia imani na kujisalimisha kabisa kwa
riziki ya Mungu Baba. Huu ni umuhimu wa ujumbe wetu kama Poor Servants of
Divine Providence.
Watu wengi miongoni mwetu ni wakulima na mifano hii badala
ya mafundisho kuhusu hali ya Ufalme wa Mungu, ni hamasa pia ili waendelee
shughuli yao ya kila siku kwa uvumilivu na imani katika kitendo ya Mungu.
Mifano hii anatualika kuangalia mwendo wa ongezeko la mashamba katika uwanja,
hasa kuhusu mahindi na maharagwe. Sisi sote tunajua kwamba baada ya kazi ya kwanza
ya kupanda tunategemea mvua na nguvu ndani ya mbegu. Hiki ni kitendo cha Mungu
anayethamini juhudi ya binadamu kama ushiriki katika uumbaji na anatubariki kwa
mavuno mengi. Tumshukuru Mungu kwa nguvu ambayo anatupa ili kufanya kazi kwa
uaminifu na aendelee kutupatia Baraka zake kwa manufaa ya familia zetu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário