quinta-feira, 25 de junho de 2015

MOYO SAFI KABISA WA BIKIRA MARIA

Kutafakari kutoka Is 61: 9-11; Lk 2: 41-51

Tuliadhimisha kumbukumbu ya moyo safi kabisa wa Bikira Maria. Kumbukumbu hii ni uenezaji wa sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Bwana. Tunaalikwa kutafakari kuhusu uwezo wa Mama Maria, wa kuweka moyoni Neno la Mungu na kuzaa tunda zuri kwa dunia. Tunaalikwa kutafakari pia mshikamano wa Mariamu kabla ya mateso ya mwana wake kama ushirika wa mioyo miwili.

          Somo la kwanza, kutoka kitabu cha Isaya, linaongea kuhusu uhusiano wa ndani kati ya Mungu na watu wake. Mungu anaitumia nguvu yake ili kutenda matendo ya ajabu kuyaokoa maisha yao. Mungu ni mwaminifu kwa watu wake na anaahidi kuanzisha agano jipya la milele, kuuthibitisha ukaribu wake nao, kuwaalika kuishi hisia ya mali kwake. Uhusiano huu na Mungu unawafanya kupitia baraka nyingi na unawabadilisha katika rejea kwa mataifa yote. Hali halisi hii ni kama ndoa: Mungu ni mume na anauoa mji wa Yerusalemu, ambao ni ishara ya watu wake, na anaualika kwa shukrani na furaha kwa sababu Bwana mume wake alitenda matendo mazuri kwake, akiuvalisha kwa wokovu na ushindi. Kupitia ishara hii Mungu anaahidi kufikia watu wote kwa wokovu wake. Jumuiya ya kikristu hutafsiri hali halisi hii kama umbo/ishara ya Bikira Maria aliyekubali kuwa mama wa Yesu, ambaye ni wokovu wa Mungu kwa dunia.

       Injili inaongea kuhusu ushiriki ya Familia takatifu (Yesu, Maria na Yosefu) katika jumuiya yake. Kulingana na andiko hili la Luka ushiriki wa familia hii ulikuwa desturi. Kwa kweli miongoni mwa Wayahudi ni desturi kwamba kila Myahudi lazima kwenda Yerusalemu mara moja kwa mwaka kusherekea sikukuu ya pasaka pamoja na wengine. Yesu alikuwa kijana wa umri wa miaka kumi na miwili, na inavyoonekana alipotea hekaluni, lakini kwa kweli yeye alijikuta. Hali halisi hii ilikuwa ngumu sana kwa Maria na Yosufu wafahamu. Hasa Mariamu, ingawa hakufahamu hali halisi hiyo, lakini alikuwa na tabia nzuri ya kuweka moyoni mwake matukio muhimu, akitafakari na akitafsiri ili atende mapenzi ya Mungu.

          Kulingana na kumbukumbu ya leo, umakini uetu unarudi kwa moyo huu wa mama, wa mtumishi, wa mwanafunzi, wa kielelezo kwa wote. Maria alikuwa na uhusiano wa ndani na Mungu kwa sababu moyo wake ulikuwa wa Mungu na kwa Mungu. Maria alikuwa makini sana kwa matendo ya Mungu katika historia ya watu wake. Moyo wa Bikira Maria ulikuwa makao ya Mungu, mahali pa kwanza, ambapo Yesu alizaliwa. Kwa hivyo haikuwa ngumu sana kwa mama Maria kuishi ushirika wa ndani na moyo wa mwana wake Yesu. Kabla ya mateso ya Mwana, tunatafakari huruma ya Mama, ambaye anajua jinsi ya kupenda na jinsi ya kuteseka kwa mtu anayependwa. Maria alichukua katika moyo wake huzuni zote za mwanawe. Kama hii ulitimizwa unabii wa Simeoni katika Hekalu wakati yeye alichukua mtoto mdogo Yesu mikononi mwake: “Upanga utachoma moyo wako mwenyewe”.
       

         Kati ya tabia kadhaa za Bikira Maria tukaribisheni ushahidi wake wa ukimya kama mwanafunzi wa kwanza na mwaminifu wa Mwanawe. Yeye alichukua jukumu lake hadi matokeo ya mwisho. Wakati wanafunzi wengine walienda zao, Maria akabaki amesimama kando ya msalaba. Mwana na Mama wanatusaidia kutafakari kuhusu hali halisi ngumu ya mateso ya binadamu na kuamini kwamba Mungu hawaachi wale wanaoteseka. wanatufundisha jinsi ya kukaribisha mateso kwa utulivu na kuwa uwepo imara katika maisha ya watu wanaoteseka. Hebu mfano huu wa Maria, utuhamasishe kuishi kwa uaminifu utambulisho wetu wa wanafunzi wa Mwana wake Yesu na kuyasalimisha maisha yetu kama Yesu kwa wema wa wengine.   

Fr Ndega
Mapitio: Sarah

Nenhum comentário: