Hek 1: 13-15; 2: 23-24; 2Kor 8: 7.9.13-15; Mk 5: 21-43
Kulingana na mpango wa upendo wake Mungu,
tuliumbwa kwa uzima. Kupitia Yesu Kristu, amezalisha na kusaidia uzima miongoni
mwa watu. Tunapitia mauti wakati hatupendi, kuonyesha upinzani dhidi ya mipango
ya Mungu.
Somo la
kwanza kutoka kitabu cha Hekima linaongea kwamba Mungu ni Mungu wa uhai. Aliviumba
vitu vyote na ameongoza kila kitu kwa hekima na wema. Hakuyaumba mauti, na kila
kitu anafanya ni kwa wema wa wana wake ili wawe na maisha mengi. Ulikuwa mpango
wa Mungu kuumba binadamu kama yeye mwenyewe na kuwakabidhi utunzaji wa vitu
vyote. Mungu aliwapa zawadi ya maisha ya milele, akionyesha furaha yake yote na
uradhi kuhusu tendo maalum la mikono yake. Kuwepo kwa mauti si mpango wa Mungu;
mauti hayatoki kwa yeye. Yalianzishwa duniani na shetani kwa sababu ya wivu na
upinzani wake dhidi ya mapenzi ya Mungu. Yeye ni adui wa Mungu na wale tu ambao
wameamua kumtumikia shetani, wakifanya upinzani dhidi ya Mungu, watayapitia
mauti.
Kabla ya
mahitaji ya wakristu wa kanisa la Yerusalemu, Mt Paulo anauliza usaidizi kutoka
jumuiya zingine za kikristu, ambazo zinajibu mara moja. Katika andiko hili tuna
kielelezo kizuri cha jumuiya ya Wakorinto. Mt Paulo anatambua na anasifu zawadi
za jumuiya hii, hasa zawadi za imani na huduma ya ukarimu. Kupitia tabia hizi
wanatenda kulingana na ukarimu na utupu wa Kristu ambaye, ingawa alikuwa tajiri,
akajifanya maskini ili awatajirishe watu kutokana na umaskini wake. Huu ni
mwaliko kwa kushiriki na wengine zawadi zilizopokewa, kuishi kwa njia ya halisi
umoja wa Mwili wa Kristu.
Wanafunzi
walikubali changamoto ya kulivuka ziwa tena hata baada ya uzoefu wa kutisha wa
dhoruba (kulingana na Injili ya wiki iliyopita). Lakini sasa, kwa kutambua
uwepo na nguvu ya Yesu, wana maana nzuri kulivuka ziwa na kuyachukua matokeo ya
kuishi na Yesu katika upande mwingine, ni kwamba, kufikiri, kuhisi na kutenda
tofauti. Lengo la ujumbe wa Kristu ni kuusaidia uzima miongoni mwa watu.
Anafanya hili kwa nguvu yote ya upendo wake. Kama hili lilitokea kupitia
miujiza miwili iliyojulishwa katika injili siku ya leo. Yesu anayatoa maisha
mapya kwa mwanamke aliyeteseka kwa kutokwa na damu kwa miaka kumi na miwili, na
anafufua binti wa Yairu. Katika miujiza hii miwili ilikuwa muhimu sana tabia ya
imani ya watu hawa wawili ambayo ilitambuliwa na Yesu na kuwekwa kama kigezo
cha msingi ili kuruhusu tendo la Mungu ambaye anataka kuokoa na kutoa maisha
mapya.
Watu wengi
walikuwa karibu na Yesu, lakini mwanamke huyo tu alimgusa kwa imani. Kwa hivyo
Yesu anauliza maswali, “Nani aliyegusa mavazi yangu?” swali hili linatufanya
kutafakari kuhusu utambulisho wetu kama wakristu, ambao tunaishi karibu na
Yesu, kushiriki kwa sakramenti, hasa Ekaristi takatifu, lakini pasipo imani au
kwa imani ndogo. Hali halisi hii inatuzuia kufikia mabadiliko ambayo tunahitaji
kwa maisha yetu. Hiyo ni kama kulivyotokea katika Nazareth ambapo Yesu hakuweza
kufanya mwujiza kwa sababu ya kutokuwa na imani ya watu. Binti Yairo ni ishara
ya maisha yetu ambayo yanahitaji kuhamasishwa na kufufuliwa. Imani ya Yairo ni
imani ya jumuiya yetu, ambayo lazima kuwa macho ili itambue Yesu na imruhusu
kushiriki nguvu za uhai zake nasi. Anajua kwamba bila kitendo chake maishani
mwetu hatuwezi kufanya chochote. Yeye afufue imani yetu ndogo ili tutangaze kwa
shauku uhai wake wa ufufuko na ushiriki wetu naye. Ili ushiriki wetu katika kila
Ekaristi takatifu uwe maonyesho ya uhusiano wetu wa ndani naye.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário