domingo, 21 de junho de 2015

NGUVU JUU YA VITU VYOTE


Jb 38: 1.8-11; 2Cor 5:14-17; Mk 4:35-41

        Liturujia ya Jumapili hii ni mwaliko kufanya mpya imani yetu katika Mungu aliye makini sana kwa maombi yetu kwa usaidizi na ni mwaliko pia kumpa mahali anapostahili katika maisha yetu. Somo la kwanza linachukuliwa kutoka kitabu cha Ayubu. Ayubu ni mwenye haki ambaye, hata kupitia mateso mengi hakukata tamaa kumwamini Mungu. Hadithi yake ni ishara ya maisha ya myahudi mwenye moyo ibada, anayetumia uhusiano wake na Mungu juu ya vitu vyote. Yeye ni kielelezo cha mtu anayechukua imani katika Mungu kama maana ya utambulisho na anabaki mwaminifu hata katika nyakati za majaribio. Andiko la leo linaeleza jinsi Mungu anavyoshinda upinzani wa bahari na aliifanya kumtii. Kwa watu wa kale bahari ilikuwa ishara ya nguvu za kupinga au mbaya, lakini haikupinga kwa nguvu na hekima ya Mungu. Kupitia kazi zake Mungu anaonyesha utunzaji na ulinzi wake kuhusu maisha, hasa maisha ya binadamu. Hali halisi hii inamsaidia Ayubu kufahamu kwamba vitu vizuri tu hutoka kwa Mungu. Somo la pili linaongea kwamba Kristu alikufa na alifufuka kwa ajili yetu ili tuishi kwake peke yake. Hali ya ubatizo inathibitisha kwamba wito wetu na utambulisho wetu ni kuwa kwake. Upendo wake kwetu unatuhamasisha kufanya vizuri zaidi sisi wenyewe kwa wema wa wengine kama alivyofanya kwetu. Kama hivyo tunahisi umoja naye, kuchukua njia yake ya kufikiri, kuhisi na kutenda.  

       Baada ya kutangaza Ufalme wa Mungu katika mifano, Yesu anawaalika wanafunzi wake “kuvuka juu ya ziwa kwa upande mwingine”. Upande mwingine ni ishara ya njia nyingine ya kufikiri, kuhisi na kutenda. Hii ni awali ya uzoefu wa wanafunzi na Yesu. Walialikwa kubadilisha mawazo yao ili yawe zaidi kulingana na mpango wa Mungu. Katika baadhi ya muda Yesu aliitikia kidogo tu na Petro kwa sababu upinzani wake katika mambo haya. Wanafunzi waliingia mashuani na wakamchukua Yesu nao”. Hii ni ishara muhimu ya utambulisho wao na Mwalimu na mapendekezo yake. Hawapo peke yao. Mashua ni ishara ya shughuli ya kila siku na ujumbe ambao wanaalikwa kuchukua na kuendelea. Kuchukua Yesu katika mashua ni kumchukua katika maisha na kumkabidhi matokeo ya kazi. Hii ni imani ya kubadilishana: Yesu anawakabidhi ujumbe na wao wanamkabidhi maisha yao.

        Upepo wenye nguvu na bahari katika hali halisi hii ni ishara ya majaribio na matatizo. Wakati wote walijaribiwa kufikiri kwamba waliweza kutatua hali halisi ya ugumu wao peke yao, wakimwacha Yesu asiyetenda maishani mwao. Bila shaka kwamba kusema maneno haya “Yesu alikuwa akilala usingizi” hayamaanishi usingizi wa kweli, bali wakati ambao uwepo wake ulipuuzwa. Hali halisi hii ilisababisha utisho na mchafuko maishani mwa wanafunzi. Wafuasi wanamwomba Yesu kuwaokoa”. Dua kwa usaidizi ni maonyesho kwamba wakati wa ujumbe wao walialikwa kuonyesha imani yao katika Yesu ambaye alikuwapo daima, akidhibitisha maneno yao kupitia matendo ya ajabu. Hofu na kutokuwa na imani kulikuwa ishara kwamba hawakujua Yesu vizuri sana: “Ni nani huyu, basi hata upepo na bahari humtii?”


     Kulingana na mawazo ya watu wa Agano la Kale, Mungu peke yake ana uwezo ili kutawala bahari, kuweka kikomo katika mwambao wake. Yesu ni Mwana wa Mungu wa kweli kwa sababu ana nguvu juu ya bahari na juu ya kila kitu. Huu ni ukweli kwamba sisi kama wafuasi wapya wa Yesu tunaalikwa kushuhudia. Mara nyingi tunakabiliana na upinzani, mashaka na hofu inayoupunguza uwezo wetu wa kuamini. Yesu anaonekana kutokuwepo maishani mwetu labda kwa sababu hatukumtoa mahali anapostahili. Tunajua kwamba nguvu zetu hazitoshi kukabili changamoto ya safari. Yesu anatuongozana na utunzaji na uangalifu, Hata hivyo anatarajia kushauriwa si kwa muda wa kihakiki tu, bali daima. Turuhusu kwamba yesu awe mwenye kuwa macho  miongoni mwetu ili alifufue tumaini letu na aiongeze imani yetu. 

Fr Ndega 
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: