domingo, 22 de novembro de 2020

MUNGU ANAJITAMBULISHA NA WALIO NA SHIDA

 

Tafakari kutoka Ezekieli 14: 11-12.15-17; 1Kor 15: 20-26.28; Mat 25: 31-46




 

       Likiuhitimisha Mwaka wa Kiliturujia, Kanisa linasherehekea Sherehe ya Bwana Wetu Yesu Kristo Mfalme na kutukumbusha kwamba tamani lake ni tushiriki katika Ufalme wake. Maandiko haya yaliyochaguliwa kwa siku hii yasema kwamba Mungu ni kama Mfalme-Mchungaji ambaye anawajali wana kondoo wake na kuwa na upendo maalum hasa kwa ajili ya wasio na nguvu. Tabia yake ni kipimo cha matendo yetu.

        Kwa jina la Mungu, Nabii Ezekieli anawashutumu viongozi wa Watu wa Israeli kwa sababu tabia yao ya kutowajibika ilisababisha kipindi cha huzuni na mateso kwa watu hawa katika uhamisho wa Babeli. Lakini katika ujumbe wake, nabii anatangaza pia utunzaji wa Mungu kwa ajili ya watu hawa. Yeye atawaongoza kwenye hali mpya kama vile mchungaji kwa ajili wa wana kondoo wake. Kweli watu walikombolewa kutoka uhamisho. Lakini tukio hilo lilikuwa tangazo tu la kazi ya Yesu kama Mchungaji Mwema aliyesalimisha ili wanadamu wote wapate maisha mapya.

         Kulingana na Mtakatifu Paulo, Yesu amefufuka kama limbuko, yaani kwa ajili ya kuwa wa kwanza wa wengi. Yeye alifungua kwetu mlango wa maisha kamili na kweli. Alifanya hivyo akizishinda nguvu zote duniani, kupitia kifo chake na ufufuo wake, akiwaokoa wanadamu na kuanzisha Ufalme wa Mungu Baba yake. Wanadamu wote wanaalikwa kuingia katika ufalme huu. Lakini ni muungano na Kristo ambao unatusaidia kufanya uzoefu wa ufalme huu.  

     Andiko hili ya Injili linajulikana kama “Hukumu ya mwisho” na wengi kati yetu wanapendelea kumfikiria Yesu kama “hakimu” atakayekaa kitini chake akiwahukumu wanadamu, kuwatuza wengi na kuwaadhibu wengine kama wafalme wa ulimwengu walivyo. Lakini hatuwezi kusahau yale aliyosema, yaani “Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili kuwa hakimu wake, lakini kwa kuwa mkombozi wake” (Yohane 3, 17). Hivyo, lengo lake sio kuhukumu bali kuokoa kwa sababu ya upendo na huruma yake. Basi, inawezekanaje kufahamu andiko hili la Mathayo linaloongea kuhusu hukumu?

      Wainjilisti wanaonyesha kwamba Yesu alikataa cheo cha mfalme katika wakati wa utukufu, na kukubali katika wakati wa kushindwa, mfano msalaba. Upinzani wake kwa cheo hiki ulikuwa kwa sababu ya mawazo ya kisiasa ya watu kuhusu suala hili. Yeye anatumia mfano wa mfalme-mchungaji katika andiko hili ili kuelea maana kamili ya Ufalme wake na lengo lake kama Mfalme. kwanza kabisa, Ufalme wake sio kutoka ulimwengu huu wala haiwezekani kuuonwa na kusema ndipo hapa au ndipo huko. Ufalme huu una tabia tofauti, yaani haiwezekani kuonwa bali kuwepo.

       Yesu hakufafanua Ufalme wa Mungu ni nini, lakini alisema kwamba ndio kati yetu nasi tunaalikwa kufanya uzoefu wa ufalme huu kwa kupitia matendo mema kwa ajili ya wengine. Kweli ufalme unaonyeshwa na baadhi ya matendo letu, lakini tuwe macho! Ufalme sio tendo tunalofanya bali ni tendo la Mungu katika maisha yetu katika ulimwengu na katika historia. Yesu ndiye mfalme aliyekubali msalaba kama kiti chake cha enzi alipoonyesha upendo wake kubwa kwa ulimwengu. Ndio Hukumu: mfano wake wa kupenda na kuwa na huruma kama kipimo cha kutenda. 

       Mfalme huyo anataka kuwakusanya watu wote kuzunguka naye katika ufalme wake kama mchungaji anavyofanya kwa kundi lake. Yeye anajitambulisha na ndugu wadogo na kuyaanzisha matendo ya upendo na huruma kwa ajili yao kama kipimo cha wokovu. Aina ya mahusiano yetu na wale walio na shida na wadogo inatuhukumu.

     Sehemu ya mwisho ya hukumu itakuja kwa wote nayo inapaswa kuwa ukamilifu wa maisha yetu kwa sababu mambo yote ambayo tumeishi ndiyo maandalizi kwa wakati huu. Tutakapokutana na Mungu, hatutaulizwa ikiwa tumeshiriki katika dini fulani wala mara ngapi tulienda kanisani, bali kiasi gani tuliweza kupenda. Kwa hivyo tuko na ishara za Kristo kwa ajili ya wadogo kama mfano. Mambo yote tunayoweza kufanya kwa ajili yao ni kwa Kristo tunayofanya.

      Hatuhitaji kuacha ubinadamu wetu ili kukutana na Mungu. Yeye mwenyewe anajiruhusu kukuta katika ubinadamu wetu, hasa wakati ubinadamu huu unateseka. Ndizo chaguo zetu zitakazoamua mwelekeo wa maisha yetu. Tusisahau kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba maisha yetu yapate ukamilifu na kwa hivyo anakaa ndani yetu kwa Roho wake. Tumpe nafasi ya kutenda sababu, “Ikiwa Mungu yumo ndani yetu, tutafanya yale mema hata kwa kupita kwetu tu”.


Fr Ndega

Nenhum comentário: