domingo, 23 de abril de 2017

MSAADA YA JUMUIYA KATIKA UZOEFU WA IMANI WA KIBINAFSI


Kutafakari kuhusu Matendo 5,12-16; Ufu 1,9-11a.12-13.17-19; Yoh 20,19-31



            Katika Jumapili hii Kanisa linawaalika waamini kutafakari juu ya jambo la huruma ya Mungu. Tunataka kujifunza kutoka kwa Kristo jinsi ya kuwa na huruma kwa wengine kama yeye alivyo kwa ajili ya Thomas aliye kutokuwepo katika jumuiya. Yesu mwenyewe, katika injili ya Mathayo anatuhakikishia: “Heri walio na huruma, maana watahurumiwa” (Mt 5:7). Kulingana na baba mtakatifu Francisco, “Yesu Kristo ni uso wa huruma ya Baba. Fumbo la imani ya Kikristo linaonekana kukuta awali yake katika neno hili (...) tunahitaji kutafakari fumbo la huruma. Hiyo ndiyo chemchemi ya furaha, utulivu na amani.”

Somo la kwanza linaongea kuhusu njia ya Wakristo wa kwanza ya kuishi kilicho kipimo cha utambulisho wa jumuiya za Kikristo za nyakati zote. Wakristo wa zamani walipata mafanikio katika safari yao kwa sababu ya vipimo vinne, yaani “mafundisho ya mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.” Njia ya kuishi kama wamoja iliwavutia wengine wengi ambao walitambua katika matendo yao ya ajabu tendo la Bwana aliye Mfufuka. Hivyo,  kwa ushuhuda wao watu wengi walikutana na huruma ya Mungu. Katika somo la pili, Paulo anamtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake kwa ajili ya watu wake tulio sisi sote. Kwa ufufuko wa Kristo tulifanywa upya na kuitwa kwa tumaini hai na kuishi imani yetu kwa furaha na kwa ahadi mpaka tupate lengo la imani yetu, yaani wokovu.

Baada ya ukatili kwa Bwana wao, wanafunzi wa Yesu waliishi katika mazingira ya hofu. Hawakutaka kuwa na mwisho sawa wa mwalimu wao, lakini waliendelea wanakutana hata kwa siri. Mambo mengi ambayo walijifunza kutoka kwa Yesu yalikuwa maana ya utambulisho wao. Basi, ingawa walikuwa na hofu hawakuwa wasio na tumaini kwa sababu yule aliyewaita kumfuata aliwataka mashahidi wake. Akijua kwamba walihitaji msaada, Yesu aliwajia akiingia bila kufungua milango maana hakuna kitu ambacho kiweze kuweka mipaka kwa mwili wa Yesu Mfufuka. Hali hii mpya ya mwili wake ni tangazo la hali ijayo ya miili ya wafuasi wake walio waaminifu kwake. Yesu aliingia na kusimama katikati yao kwa sababu anataka kuwa rejeo maishani mwao. Yeye alikuja kuwasaidia kushinda hofu na mashaka mengi katika safari yanayowazuia kumshuhudia kwa kweli.

Matokeo ya kwanza ya uwepo wa Bwana Mfufuka kwa wanafunzi ni furaha, yakithibitisha kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni kuwa mwenye furaha. Furaha inaifungua milango ya moyo kwa kuzipokea zawadi zingine. Bwana anaijalia jumuiya ya wanafunzi amani kama utambulisho na Bwana wao aliye pia “Nabii asiye na ukatili”. Ikiwa Bwana Mfufuka yu katikati ya uzoefu wa jumuiya, wana wa jumuiya hii wanakuwa vyombo vya amani. Pumzi ya Roho Mtakatifu ni ishara ya maisha mapya kwa ubinadamu ulifanyika upya kabisa kwa msalaba na ufufuko wa Kristo. Watu wapya wamekusanika kwa jina la Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu wanaitwa kuishi kwa ushirika na upatanisho na kuzisaidia zawadi hizi kwa wengine.

Thomas hakuwepo katika mkutano wakati Bwana Mfufuka alijifua akitoa zawadi zake. Hakika Thomas alipendelea uzoefu tofauti, yaani uzoefu wa “nje ya jumuiya.” Kipengele cha kwanza kuhusu Thomas ni kuhusu kutokuwepo kwa jumuiya. Mtu huyo ni mfano wa wale ambao wana ugumu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Kutokuwepo huko ni hatari kwa uzoefu wao wa imani wa kibinafsi na kunaweza kuweka vikwazo kwa imani ya wengine. Kwa upande mwingine, tunaweza kusema kwamba mfano wa Thomas unafanya jumuiya kushuhudia imani yake kwa kweli na kuaminika.  Haitoshi kusema “tumemwona Bwana!”. Bali ni lazima kumtambua na kumtangaza bila hofu kama “Bwana wangu na Mungu wangu!”. Kwa sababu ya Thomas, Yesu anatangaza maneno haya ya ajabu, yaani “Heri walioamini bila kuona.”

Kwa mitume Yesu anatupa zawadi ya imani na kumwomba tuishi imani hii pamoja na wengine, kwa kupendana na kusaidiana kama matokeo ya maisha mapya kutokana na ufufuko wa Bwana wao. Mtu ana ugumu wa kuamini ikiwa anaamini peke yake. Imani ya mtu ni matokeo ya uzoefu wa jumuiya ya Kanisa, kwa sababu imani ya Kanisa inaitangulia, inaizaa na kuiimarisha imani ya mtu huyo. Bila ushiriki kwa hamu katika Jumuiya ya Kanisa, tuko na ugumu wa kutambua ishara za uwepo wake miongoni mwetu na imani yetu ni inakuwa haba na tena hatari kwa uzoefu wa wengine.


Andiko hili linatusaidia kutambua umuhimu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Bwana Mfufuka alitaka kujifunua kwetu kupitia msaada wa wengine. Tunapaswa kuwa macho kwa mwelekeo wa ubinafsi katika jamii ambao umeshawishi mahusiano yetu na kuuvuruga undugu wetu. Kwa njia ya ubinafsi maovu mengi unatujia. Ni lazima kumchukua Yesu kama kipimo cha uzoefu wetu wa jumuiya nayo jumuiya inapaswa kuwa na nafasi muhimu katika maisha yetu ili tuweze kushinda hofu na kutokuwa na imani ili ushuhuda wetu uwe ufanisi katika hali iliyo kandokando yetu. 

Fr Ndega

Nenhum comentário: