Kutafakari kuhusu
Mdo 5,12-16; Ufu 1,9-11a.12-13.17-19; Yoh 20,19-31
Siku ya leo ni jumapili ya huruma ya
Mungu. Tunataka kujifunza kutoka kwa Kristo jinsi ya kuwa na huruma kwa wengine
kama yeye alivyo kwa ajili ya Toma aliye kutokwepo katika jumuiya. Yesu
mwenyewe, katika injili ya Mathayo anatuhakikishia: “Heri walio na huruma,
maana watahurumiwa” (Mt 5:7). Katika somo la kwanza watu walitambua tendo la Yesu
likitendeka miongoni mwao kupitia maneno na matendo ya mitume. Kwa kweli yale
ambayo Mitume walifanya yaliwavutia watu, lakini walijiona kuwa vyombo peke
yake, kwa sababu mabadiliko maishani mwa watu ni kazi ya Bwana aliye Mfufuka.
Katika somo la pili, Yohane alipewa ufunuo wa utambulisho wa Mtu mfano wa
Mwanadamu ambaye alikufa, lakini anaishi milele. Bwana huyo anamwalika Yohane
kushuhudia bila hofu kwa sababu mauti yalishindwa na hayatawali tena kamwe.
Baada ya ukatili
kwa Bwana wao, wanafunzi wa Yesu waliishi katika mazingira ya hofu. Hawakutaka
kuwa na mwisho sawa na mwalimu wao, lakini waliendelea wanakutana hata kwa
siri. Mambo mengi ambayo walijifunza kutoka kwa Yesu yalikuwa maana kwa
utambulisho wao. Basi, ingawa walikuwa na hofu hawakuwa wasio na tumaini. Lakini
walikuwako na shida kwa maana yeyote ambaye anafunga milango inawezekana awe na
upinzani kwa tendo la Bwana ama ugumu ili awe mashahidi. Kristo aliingia bila
kufungua milango kwa sababu, baada ya ufufuko, ana mwili mtukufu, yaani hakuna
kitu ambacho kiweze kuweka mpaka kwa mwili wa Yesu. Hali hii mpya ya mwili wake
ni tangazo la wakati ujao wa miili ya wafuasi wake walio waaminifu. Yesu
aliingia na kusimama katikati. Anajua vizuri hali ya utisho ambayo wanafunzi
walikuwa wakiishi. Yeye anapaswa kuwa rejeo maishani mwa wanafunzi na, kwa
hivyo, alikuja kuwasaidia katika udhaifu wao akiondoa hofu na mashaka mengi
maishani mwao ambayo yanawazuia kumshuhudia kwa kweli.
Matokeo ya kwanza ya uzoefu wa Bwana Mfufuka ni furaha, kuthibitisha
kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni kuwa mwenye furaha. Furaha inaifungua milango
ya moyo kwa kuzipokea zawadi zingine. Nazo zawadi zifuatazo zinadhihirisha
ukarimu wa Bwana Mfufuka kwa manufaa ya jumuiya ya wanafunzi wake. Bwana
anaijalia jumuiya amani kama utambulisho na Bwana wao aliye “Nabii asiye na
ukatili”. Kama Bwana mfufuka yu katikati ya uzoefu wa jumuiya, wana wa jumuiya
wanakuwa vyombo vya amani. Zawadi ya Roho Mtakatifu ni uhakika kwamba
hatutembei peke yetu. Msaada wake unatukumbusha kwamba lengo la utambulisho
wetu kama wanafunzi ni kuusaidia uzoefu wa ushirika na upatanisho. Huyo Roho Mt
ndiye Roho wa umoja na kutenda ili tuweze kushinda mgawanyiko na ugumu wa
uhusiano miongoni mwetu. Toma hakuwapo katika mkutano wa ufunuo wa Bwana
Mfufuka kwa sababu alipendelea uzoefu tofauti. Huyo ni mfano wa wale ambao wana
ugumu wa kushiriki pamoja katika jumuiya na kuchagua kuomba radhi kuliko
mabadiliko ya tabia yao. Pamoja na imani haba, watu hawa wanaweka vikwazo
katika imani ya wengine. Kwa kweli uwepo wao ni hatari kwa imani ya jumuiya.
Lakini Yesu anatenda kwa utulivu na kumsaidia Toma
kupitia ishara halisi za ushindi wake. Kama hitimisho, Yesu anampa zawadi ya
imani na kumdai aishi imani hii pamoja na wengine, kupendana na kusaidiana kama
matokeo ya maisha mapya kutokana na ufufuko wa Bwana wao. Mtu ana ugumu wa
kuamini ikiwa anaamini peke yake, yaani, imani yake si kweli. Imani ya mtu
lazima kuwa matokeo ya uzoefu wa ushiriki wake katika Kanisa, yaani jumuiya ya
upendo, kwa sababu imani ya kanisa inaitangulia, inaizaa na kuilisha imani ya
mtu huyo. Bila ushiriki kwa hamu katika Kanisa lililo jumuiya ya wafuasi wa
Bwana Mfufuka, tuna ugumu wa kutambua ishara za uwepo wake miongoni mwetu na
imani yetu ni haba. Andiko hili linatusaidia kutambua umuhimu wa kushiriki
pamoja katika jumuiya. Bwana Mfufuka alitaka kujifunua kwetu kupitia msaada wa
wengine. Tunapaswa kuwa macho kwa mwelekeo wa ubinafsi katika jamii ambao unaambukiza
uhusiano wetu kutuzuia kuishi kwa ndugu ya kweli. Kupitia ubinafsi uovu mwingi unawezekana
kutokea. Yesu anapaswa kuwa katikati ya jumuiya nayo jumuiya inapaswa kuwa na
nafasi muhimu katika maisha yetu ili tuweze kushinda hofu na hali mbaya ambayo
inatuzuia kuwa mashahidi wa kweli.
Fr Ndega
Mapitio na marekebisho: Sarah
Nenhum comentário:
Postar um comentário