domingo, 30 de agosto de 2015

UHUSIANO WA KIROHO NA MUNGU


Kutafakari kutoka Kum 4:1-2.6-8; Mk 7:1-8.14-15.21-23

     Mungu aliwapa watu wake Amri zake na akawafundisha njia ya kuzishika. Haziwezi kubadilishwa kulingana na mapenzi ya kibinadamu. Kama maonyesho makuu ya upendo na utunzaji wa Mungu, Yesu anatukumbusha muhimu zaidi ya sheria na anatufundisha kuishi na uhusiano wa kiroho na Mungu. Uhusiano huu uko juu ya sheria zote.  

       Kulingana na somo la kwanza, kupitia utumishi wa Musa, Mungu anawaalika watu wa Israeli washike amri zake kama miongozo kwa uzima. Baada ya kuwaweka uhuru kutoka Misri, Mungu alianzisha agano na watu hawa huko Sinai na Amri zilikuwa miongozo kama maonyesho ya matarajio yake kuhusu maisha ya watu wake. Kuishi kulingana na Amri kumekuwa umuhimu katika safari ya Watu wa Israeli ambao Sheria ni Neno la Mungu na Neno la Mungu ni Sheria. Wakati wao husema “Sheria ya Mungu ni kamilifu, faraja kwa roho”, wanamaanisha Neno la Mungu. Kuna uhusiano wa ndani kati ya Sheria na Neno, kwa sababu amri za Sheria zinaonyesha utunzaji na upendo wa Mungu anayeongea kuonyesha njia za ukombozi. Na tena zinadhihirisha utambulisho na hekima ya Watu ambao wanamtii Mungu wao. Utii kwa amri ni chanzo cha baraka kinachoelekeza kwa uhai, wakati uasi kwa hizo unaelekeza kwa mauti.      

       Katika Sheria kuu, Wayahudi waliweka maagizo mengi ya kibinadamu na kidogo kidogo walibadilisha mwelekeo kutoka zile zilizokuwa muhimu zaidi. Hata kwa wao wenyewe ni ngumu kuishi maagizo yote yaliyoongezwa. Hii ni maana ya mapambano kati ya Yesu na Waandishi na Mafarisayo ambao walikuwa wakuu kwa mabadiliko ya maana ya Sheria. Kabla ya Yesu manabii wengi walikwisha pinga kuhusu tabia hii. Miongoni mwao wapo Isaya, Hosea na Amosi. Hasa kulingana na nabii Isaya, tunakuta tangazo muhimu kutoka kwa Mungu: “Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao ni mbali nami; nao waniabudu bure. Wanayafundisha maagizo ya kibinadamu tu.”

    Yesu anawakosoa walimu wa sheria na mafarisayo kwa sababu walitafsiri sheria kulingana na mawazo yao na walikuwa vielelezo vibaya kwa watu wote hasa kwa wanafunzi wake. Mara nyingi Yesu alipokutana nao hafikii mafanikio kuhusu mapendekezo yake ya maisha mapya kwa sababu wao ni wanafiki na wanapendelea kumjaribu Yesu kuliko kujiruhusu kubadilishwa kulingana na matarajio yake. Kwa hivyo mkutano wa Yesu nao ni maana ya mapambano daima. Wao ni wenye upayukaji kwa sababu hawatendi yale wanayosema. Waliyaondoa maana ya unabii wa sheria na wanafundisha maagizo ya kibinadamu tu. Wanajifikiria watu wema na wanajijulisha vizuri nje mbele ya wengine, lakini ndani yao ni tofauti, ni hali mbaya. Wanatumia dini kwa uradhi wa binafsi yao na wanawazuia wengine kuishi kwa uhuru na furaha. Kutokuwa na uhalisi na ukweli kuifanya imani yao ishara ya kutafuta heshima  na sifa kwa wao wenyewe, mbali sana na Mungu.   

      Upinzani wa Yesu dhidi ya tabia ya vikundi hivi viwili ni mwaliko kwa mabadiliko ya mawazo yetu kuhusu dini, kuhusu uhusiano wetu na Mungu. Utambulisho wetu wa dini hauwezi kuwa ishara ya nje tu, yaani, kwenda kanisani na ushiriki katika sakramenti, kutii amri za kanisa. Yesu alithamini zaidi maisha ya watu kuliko sheria. Yesu anajali zaidi uhusiano wa kiroho na Mungu, anatualika zaidi kubadilika kiroho. kushiriki kanisani kunatupasa kuwa watu wapya na tofauti nyumbani kwa wema wa familia. Maneno au matendo mabaya ni ishara ya kutokuwa na uzoefu wa ndani na Mungu. Utambulisho wetu kama wafuasi wa Yesu unatuongoza kuheshimu uhuru wa watu na kupendelea mazungumzo kuliko kulazimisha. Kama watoto wa Mungu sheria yetu ni udugu, kuwafikiria wengine kuwa muhimu zaidi kutuliko sisi wenyewe. Yesu anatarajia tuwe na uhusiano wa kiroho na Mungu.

Fr Ndega

Mapitio: Sara

Nenhum comentário: