Kutafakari kuhusu Yohana 6: 60-69
Katika injili, tuko mbele ya maneno ya mwisho ya Yesu
katika sura hii ya sita ya Yohane, baada ya mwujiza wa mikate na samaki. Kile
Yesu alichoongea mpaka sehemu hii ya mwisho kilikuwa kigumu sana kwa
wasikilizaji wake kufahamu na kukubali. Tumetafakari kwamba Yesu alijaribu
kuwathibitishia kuhusu utambulisho wake kama mkate unaoshuka kutoka mbinguni na
mkate ambao ni mwili wake wenyewe, lakini
hakupata mafanikio maana ya mawazo yao yaliyofungwa. Ishara zilizotumiwa na
Yesu zilikuwa ngumu sana kwa wale ambao walikuwa na kujua awali kuhusu mwelekeo
wa binadamu wake. Walijua Yusufu baba yake, Maria, mama yake na walishiriki
pamoja shule moja. Hakika hawakuweza kukubali kwamba mwenzao huyu alishuka
mbinguni. Lakini ugumu huu wao haukumzuia Yesu awadhihirishie njia tofauti na
iliyojaa ya maana kwa maisha yao.
Yesu alipoongea na watu akaongea kuhusu hali ya milele,
ambayo ni mwisho wa safari ya maisha yetu. Anataka kusikika kwa sababu Neno lake
lenye nguvu, linachoma mioyo na kusababisha uamuzi. Hakuna hata mmoja asikilize
neno hili na kubaki alivyo. Miongoni mwa wale waliosikiliza Yesu walikuwapo
wanafunzi kumi na wawili. Ingawa maneno haya yalikuwa magumu pia kwa wao,
wanatambua kitu ambacho hakikutambuliwa na wengine. Hali hii ilionyeshwa kupitia
tangazo la Petro: “Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno ya uhai wa
milele. Sisi tunaamini na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu.” Tunajua
kwamba ingawa wanafunzi kumi na wawili walikuwapo pamoja na Yesu tangu mwanzo wa
huduma yake kwa umma, hawakuweza kuingiza jumla maana ya utambulisho na ujumbe
wa Mwalimu, lakini maneno haya ya Petro yanaonyesha ridhaa ya ndani kwa mtu na
mpango wa Yesu. Maneno ya Yesu yaliyapigia chapa maishani mwao njia maalum kwamba
hawawezi kupata maana mbali na Mwalimu.
Kama hii lazima kuwa utambulisho wetu na mtu wa Yesu. Baba
Mtakatifu Francisco amesisitiza sana kuhusu mahitaji ya “mkutano wa binafsi na
Yesu” ili aliyemfuata aweze kumshuhudia kwa uaminifu. Yesu ni Neno lililofanyika
mwili na Neno hili linayatoa maana kwa maisha yetu. Kwa hivyo tunaalikwa
kuchukua tangazo la Petro kama rejea ili tuwe na tabia kamili mbele ya Neno la
Mungu. Kuhusu mambo hayo Mtakatifu Yohana Calabria alisema: sisi ni makini sana
kwa maneno ya binadamu na kuhusu hiyo ni sawa. Lakini sisi lazima kuwa na
uangalifu zaidi kwa Neno la Mungu ambalo ni – consecratory – linafanya wakfu,
ni kwamba, linalifanya lile linalosema.” Mtakatifu Yohane Calabria alikuwa anasema hasa kuhusu
injili ambayo ni sheria kwetu - Poor Servants of Divine Providence. Katika
sehemu nyingine ya maandiko yake alisema: “Ikiwa sisi huamini katika maneno ya
kuapishwa kwa – consecration – katika misa: “twaeni mle wote, twaeni mnywe
wote”, sisi lazima kuamini pia wakati Yesu asema: “Msiwe na wasiwasi” au “Baba
yeno wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote” au mtafuteni kwanza
juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.” katika
maneno mengine, kutokana na Maneno ya Yesu tunaalikuwa kuwa “Injili hai.” Hili ni
lengo la Maneno ya uhai wa milele.
Kupitia adhimisho la Ekaristi tunalishwa na mkate wa Neno
na mkate wa Ekaristi. Katika uzoefu huu Yesu anajitoa jumla kwetu, kuchoma
mioyo yetu na kutushibisha ili tuwe na hamasa na shauku katika kazi zetu. Eukaristi
hii itusaidie kufikia lengo hili.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário