Kutafakari toka Kutoka 16: 2-4, 12-15; Efe. 4: 17, 20-24; Yn. 6: 24-35
Mungu anawapatia
watu wake chakula ishara ya uzima wa milele ambao tunaupokea katika kila Ekaristi
takatifu tunayoadhimisha.
Ingawa wana
wa Israeli walikuwa watumwa katika Misri, wakawa na vyakula vingi ili wale hata
kushiba. Walipoacha Misri na nguvu ya Mungu, wakapata utambulisho mpya kama Watu
wenye uhuru. Utambulisho huu mpya
ulileta baadhi ya changamoto kama kuishi jangwani, kuwa na chakula kidogo au
kutokuwa na chakula, kutokuwa na maji, uvamizi/utekaji na watu wengine, na
kadhalika. Hali hii ya kutokuwa na chakula iliwafanya kulalamika dhidi ya Musa
na Mungu. Mungu Aliyasikiliza malalamiko yao, kupitia upatanishi wa Musa na
akionyesha upendo na utunzaji kwao, akawapa mkate kwa kila siku, yaani, mana.
Wakala wakashiba.
Mt. Paulo
anafanya tofauti wazi kati ya maisha ya mtu kabla ya ubatizo na kutoka ubatizo.
Kabla ya ubatizo mtu huishi maisha ya dhambi na bila ahadi. Kupitia ubatizo mtu
anabadilishwa kabisa na kualikwa kuishi maisha mapya, yaliyojaa na maana. Mbele
ya majaribio ya kuishi kama kabla ya utambulisho huu mpya, Mt Paulo anatuonya
tuishi kama wautu wapya, yaani tuishi kitakatifu. Hii ni hali ya mtu
aliyepokewa kuzaliwa kupya katika kristo.
Yesu
alitenda ishara kuu, kupitia kushirikiana kwa mikate na samaki kwa umati wa
watu, akiwaonyesha unyeti mbele ya mahitaji yao na uamuzi kuhusu hali ya wenye
njaa. Baada ya kula hata kushiba watu walitaka kumfanya Yesu mfalme wao. Yeye akijua
mpango wao alitoroka akienda mlimani peke yake. Lakini watu walimtafuta na walimkuta
na wanafunzi wake katika kapernaumu. Kulingana na Yesu hawakufahamu ishara na
hawakuwa na maana kamili ili kumtafuta. Kwa hitimisho aliwaalika kumkubali kama
mkate wa kweli kutoka kwa Mungu ambao unaupa ulimwengu uzima. Yeyote ambaye
anakuja kwake na kumwamini hataona njaa na kiu kamwe.
Yesu
alikuwa na unyeti mbele ya mahitaji ya watu na alijaribu kuutoa mwelekeo upya
kwa maisha yao kupitia uzoefu wa huruma na kushirikiana, lakini maana ya tumbo
lao, wakawa vipofu na wasio na imani. Hawakufikia mafanikio katika kumtafuta
Yesu kwao kwa sababu ya Kutokuwa na maana kamili. Kwa kweli nia ya Yesu
akiwalisha watu ilikuwa kuwaandaa kwa mafundisho yake kuhusu mkate tofauti na
kweli. Yeye anatutolea chakula kinachodumu mpaka uzima wa milele ambacho ni
yeye mwenyewe. Anadhihirisha pia kwamba siyo Musa ambaye aliwapa watu mana,
lakini ni Mungu. Mana ni mfano wa zawadi kuu ambayo Mungu aliitoa kwa uzima wa
ulimwengu, ambaye ni Mwanawe wa pekee. Kupitia
Neno lake na kujitoa kwake Mwanao katika Ekaristi, Mungu anaendelea kuwalisha
watu wake na kuwaonyesha upendo na utunzaji wake.
Basi, Ekaristi ni
ishara kubwa ya upendo wa Mungu na maonyesho ya kujitoa kwake Kristo kwa bure.
Ekaristi ina maana tu ikiwa ni maonyesho ya upendo na udugu. wale tu wanaopenda
kwa kweli wanaweza kwenda mpaka matokeo ya mwisho kama Kristo alivyo. Upendo tu
unazaa ushirika na “vitu tu vinavyofanywa kwa upendo vina ushupavu”. Kupitia
Ekaristi tunabadilishwa kamili katika Yule tunayeadhimisha, kukubali ahadi ya
kuishi maisha mapya yanayozaliwa kutokana na mkutano naye. Hivyo Baada ya kila
adhimisho ya Ekaristi sisi hukubali changamoto ya kurudia shughuli za kila siku
kama mashahidi wa Kristo ambaye anayatoa maisha yake kwa upendo ili watu wote
wawe na uzima wa milele.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário