Kutafakari kutoka Mithali 9, 1-6; Waefeso 5: 15-20; Yoh 6, 51-58
Kulingana
na Somo la kwanza, Hekima ni nafsi ya Mungu ambaye anawaalika watu wote kwa sikukuu
yake. Kwa watu, Kukubali kushiriki katika karamu hii, ambayo Mungu mwenyewe
alitengeneza ilikuwa mwaliko ili kuacha ujinga na kupata kuishi, wakifuata njia
ya akili. Mwaliko huu ni ishara ya Ekaristi takatifu ambayo ni Yesu mwenyewe.
Yeye anatualika kwenye karamu, kushiriki furaha yake kubwa na uzima wa milele. Mt
Paulo anatualika kuishi kama wenye hekima, kutumia kwa njia ya hekima kila
nafasi inayotokea. Kulingana naye njia ya hekima ni kugundua na kufanya mapenzi
ya Mungu. Roho Mt. ndani ya kila mtu anazaa upatikanaji kwa sauti ya Mungu na
uhusiano wema na wengine.
Kristu
aliwaalika wasikilizaji wake kwa uzoefu wa ndani ambao ni ufunuo kuhusu
utambulisho wake kama chakula kilichoshuka kutoka mbinguni si kwa binadamu tu
bali kwa ajili ya uhai wa ulimwengu wote. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu hata alimtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali
awe na uhai wa milele (Jo 3, 16)”. Mwana anajitoa kama chakula kinachodumu hadi
uzima wa milele kwa sababu ya mapenzi ya Baba ambaye ni uhai na anasababisha
uzima ndani ya kila mtu anayempokea Mwanawe. Maneno haya ni awali ya mafundisho
ya Yesu kuhusu ujumbe wake kama mwokozi na mkombozi wa ulimwengu. Yesu
alijaribu kuwathibitishia wasikilizaji wake kuhusu hali hii, lakini hapati mafanikio
maana ya mawazo yao yaliyofungwa. Ishara zilizotumiwa na Yesu – “kama mkate
unaoshuka kutoka mbinguni” na “mkate huu ni mwili wangu wenyewe” - zilikuwa ngumu sana kwa wale ambao walikuwa na
kujua kwa awali kuhusu mwelekeo wa binadamu wa Yesu. Walijua Yusufu baba yake,
Maria, mama yake na walishiriki pamoja shuleni moja. Hakika hawaweza kukubali
kwamba mwenzao huyu alishuka mbinguni. Lakini ugumu huu haukumzuia Yesu
awadhihirishie njia tofauti na iliyojaa ya maana kwa maisha yao.
Yesu
anaongea kuhusu uzima bila mwisho na kwamba uko kwa wote ambao ni yeye
mwenyewe. Inawezekana kuupokea uzima huu kwa kuula mwili wake na kuinywa damu
yake, kwa sababu yeye ni hai – hawezi kufa - na anaishi ndani ya wale ambao
wanampokea. Yesu halazimishwi kufanya hivyo. Haya ni maonyesho ya kujisalimisha
kwake kwa bure, kuendeleza uwepo wake miongoni mwa wanadamu na kufundisha njia
ya utimizaji uliojaa. Hiyo ni Ekaristi kama zawadi kubwa ya Mungu ambaye hataki
kuwapo mbali ya binadamu. Ekaristi ni hazina ya kanisa, uwepo maalum ya mume
wake na awali ya uzoefu wa kiroho yake kama mke wa mume Kristu. Linaishi kwa
sababu ya Kristu. Vivyo hivyo ni kwa wote ambao wanashiriki mkate mmoja na
kikombe kimoja. Uzoefu huu ni ukamilifu wa ushirika wetu na Mungu, chanzo cha uzima
wa kweli na furaha milele.
Tunapokula
chakula cha kawaida miili yetu huweza kuingiza chakula hiki ili uwe na afya
nzuri. Kama hii, chakula kinaingizwa na miili yetu. Kuhusu Ekaristi, chakula
cha uzima, matokeo ni tofauti: wakati tunampokea Yesu, ni sisi tunaoingizwa
naye. Katika maneno mengine, Yesu anatuingiza, anatuchukua kwake ili tuishi
naye. Yeye anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Anatuunganisha naye, kutuhusisha
katika ushirika sawa kati ya yeye na Baba. Bila shaka kwamba matokeo ni pia
udugu wenye nguvu na mwafaka miongoni mwetu. Tumwombe Mungu, kupitia sacrament
hii takatifu, neema ya kuishi kwa ndani uzoefu wetu na Mwanawe ili tufikie
ushirika sawa upo katika Utatu Mtakatifu.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário