Kutafakari kutoka Yoh 11: 11-27
Tunaposherehekea uzima, tunasherehekea
fumbo kuu ambalo ni zawadi yenye thamani itokayo kwa Mungu. Katika Kristu
zawadi hii inapata ukamilifu na vilevile tunapata kuelewa kwamba maisha
hayafikii mwisho hapa. Urithi wa maisha ya wale waliotuacha ina thamani kuu
kwetu tunaoitwa kuendelea katika imani kuishi
maisha yenye maana. Ikiwa hatuwezi kuona tena wale ambao walitutangulia, yale
maadili waliyoishi na kutuachia ndiyo ushuhuda wa kwamba kuwepo kwao kati yetu
hayakuambulia patupu. Mtakatifu John Calabria alikuwa na mazoea ya kusema,
“Ikiwa tuna Mungu ndani yetu, tutafanya yale mazuri hata kwa kupita kwetu tu”.
Kusherehekea wafu, kwa mfano, ni alama kuu ya kwamba tunafahamu vile wanavyoendelea
kuwa muhimu kwetu sote, kwa vile kifo sio mwisho wa maisha haya: kinadhihirisha
tu mwisho wa sehemu moja ya maisha. Katika nyakati za sorrow na huzuni, tujiruhusu
kusaidiwa na maombi ya marafiki na kuhamasishwa na neno la Mungu linalotuimarisha
katika imani na kujitolea maishani.
Kama Wakristo, tabia yetu kuu ni tumaini. Kwa hivyo,
Mt. Paulo akasema: “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure”. Mungu ambaye
tunaamini ni Mungu wa uhai na anapotupa uzima, yeye hujiunganisha nasi na
kutufanya wanawe wapendwa. Kwa kuwa mateso katika maisha haya, hakuna
kinacholinganishwa na furaha tutakayohisi na utukufu utakaotufunuliwa.
Vilevile, tujifunze kutoka kwa Yesu ambaye hata katika wakati wa huzuni na
mateso aliyopitia kwa njia ya msalaba, alisimamia imani yake katika tendo la
riziki ya Mungu: “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”. Hili lazima kuwa
ujasiri na kilio cha roho zetu ili kutuhakikishia kwamba Mungu hawezi kutuacha
wala kunyamaza mbele ya kinachotufanyikia. Jibu kutoka kwa Mungu mbele ya kufa
kwa Yesu inaandamana moja kwa moja na ufufuko wake. Hilo linatupa matarajio ya
kufufuka kwetu na hivyo, yatuhakikishia maisha kamili kwani yeye si Mungu wa
wafu bali wa wanaoishi. Hivyo ni kusema kwamba Mungu hataki kifo. Katika Yesu anajifunua
kama ufufuko na uhai.
Kwa nini watu hufa? Yesu alitufundisha kukuza
imani yetu katika Mungu Baba, ambaye anatuangazia kwa nguvu na sifa yake yote ya
pendo lake lenye huruma na ukombozi. Yeye hutuvuta kwake kwa dhamana za huruma
na anatamani kuwa mmoja nasi. Kwa wakati huo huo, yeye huja kwa mwelekeo kwetu
na hutarajia kukaribishwa. Maisha yetu humu duniani hupita tu sehemu moja.
Lazima kuendelea safari yake katika sehemu nyingine, kwa sababu twaitwa kwa
ukamilifu. Katika maana hii, Agostino asema: “Ee Mungu ulituumba tuwe wako na moyo
wetu unahangaika hadi tunapopumzika kwako”. Kwa Yule mwenye imani, kifo ni
pumziko katika Mungu ambako sisi sote lazima kupitia ili kuwa wakamilifu.
Wakati muhimu sana maishani mwetu utakuja
na tutakutana na Mungu kwa njia ya kipekee. Tutakapokuwa mbele yake
hatutaulizwa iwapo tulishiriki katika dini yoyote wala mara ngapi tulienda
kanisani bali kiasi cha tulivyoweza kupenda. Chaguo tunayochagua katika mkondo
wa safari yetu itadhihirisha mwelekeo ambao maisha yetu yatachukua. Kulingana
na mapenzi ya Mungu, maisha yetu yanafaa kupata ukamilifu uanzao na uangalifu
wa kila siku katika ishara za upendo nyumbani na kujitolea kwa jumuiya. Kwa hivyo tunapata kuungana na Mungu aliye
mwanzo na chanzo cha uzima na asiyepungukiwa kamwe.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário