domingo, 5 de julho de 2015

HATARI YA UNABII


Kutafakari kutoka Eze 2: 2-5; 2Kor 12: 7-10; Mk 6:1-6

      Yesu ni nabii kwa ubora. Anafanya ujumbe wake akiongozana na wanafunzi daima. Wanafunzi walijifunza kumfuata Yesu kupitia hali za kila siku ambazo ziliyashirikisha maisha ya Mwalimu, ikiwamo hali ya dharau iliyopitiwa katika kijiji chake cha Nazarethi. Akidhihirisha mpango wa Mungu, Yesu alidhihirisha utambulisho wake wa kweli. Watu wa kijiji chake walijua kila kitu kumhusu yeye na walitumia hiki kama kigezo cha hukumu. Kujua kwao kwa awali kuhusu Yesu kuliwazuia kumjua nani ndiye. Walimkatalia Yesu kwa sababu walifungwa kwa upya wa Mungu uliodhihirishwa na Mwana wake, ambaye ni Mungu kweli. Je! Kujua kwetu kuhusu Yesu kumetusaidia kukua katika imani, kuimarisha uhusiano wetu naye?  

      Andiko hili linajali kaka, dada, baba na mama wa Yesu kusisitiza mwelekeo wake wa binadamu. Yesu ni mtu kweli. Alikuwa na familia moja na akawa mfanyakazi. Mji wa Nazarethi ulikuwa mahali alipoishi na akafanya kazi kama fundi seremala hadi kuanza tangazo la Ufalme wa Mungu, ujumbe wa wokovu. Bila shaka kwamba kaka na dada yake waliojaliwa hapa hawakutoka kwa tumbo lake Bikira Maria. Hata hawakuwa wana na mabinti ya Yosufu. Wakawa upanuzi wa familia ya Yesu, maana ya kigezo cha tamaduni kama unatokea katika Afrika. Basi, walikuwa ndugu zake Yesu. Katika sehemu nyingine ya injili, Yesu anaeneza mwelekeo huu wa familia kwa wale ambao husikiliza Neno la Mungu na wanaliweka katika vitendo. Maana ya imani moja, katika Yesu sisi ni kaka na dada walioalikwa kukua katika uzoefu naye. Sinodi ya Maaskofu ya Afrika ilisema kwamba Kanisa ni “Familia ya Mungu” na kila kitu ambacho hakisaidii kwa kuendelea kujenga kwa udugu huu lazima kuondolewa.

     Yesu akastaajabu na kutokuamini kwa watu wa kijiji chake na hakuweza kufanya mwujiza miongoni mwao. Imani ni kigezo muhimu kumruhusu Yesu kufanya mijiza maishani mwetu. Tuchukue vielelezo vya Yairo na mwanamke wa Injili ya Jumapili iliyopita. Katika mijiza hii miwili ilikuwa muhimu sana tabia ya imani ya watu hawa wawili iliyotambuliwa na Yesu na kuwekwa kama kigezo cha msingi ili tendo la Mungu liwe ufanisi maishani mwetu. Hasa kuhusu mwanamke huyo, watu wengi walikuwa karibu na Yesu, lakini mwanamke huyo  tu akamgusa kwa imani. Hali hii inatutafakarisha kuhusu utambulisho wetu kama wakristu, ambao wanaishi karibu na Mwana, kushiriki kwa sakramenti, hasa Ekaristi, lakini pasipo imani au kwa imani ndogo. Kama hii tunazuiwa kufikia mabadiliko yanayotarajiwa na tunahitaji kwa maisha yetu.   


    Yesu alikataliwa kijijini chake kwa maana aliuchukua ujumbe wake wa unabii kwa uaminifu. Wakati wa Yesu haukuwa upya kumwonea nabii. Katika Agano la Kale manabii wengi walidharauliwa na wakauawa. Hii ilimaanisha upinzani dhidi ya mapitio ya Mungu. Lakini katika utunzaji kwa watu wake, Mungu hakukoma kamwe kuwaalika watu ili wawe wajumbe wake. Kutokana na uzoefu wa nabii Ezekieli, katika somo la kwanza, tunatambua vigezo muhimu cha utambulisho wa wajumbe hawa wa Mungu: cha kwanza, Mungu anataka kuongea na anaanzisha kukutana na mtu (aliyealikwa); cha pili, Roho Mt. alitenda ndani ya mtu kumhamasisha ili ajibu kwa mapitio ya Mungu; cha tatu, mtu anatumwa kama mjumbe ili atangaze Neno la Mungu tu, si maneno ya binafsi mwenyewe. Kama wajumbe wa Mungu, manabii ni ogofyo kwa jamii kwa sababu wanaushutumu udhalimu na wanatangaza mipango ya Mungu. “Wanachunga kuwa katika upande wa maskini na wadhaifu kwa sababu manabii wanajua kwamba Mungu mwenyewe yupo katika upande wao.” Mt Paulo ni kielelezo kingine aliyetambua kwamba hakuhitaji chochote zaidi, bali neema ya Mungu tu ambayo ilimimarisha kabla ya matusi, mateso na matatizo. Vielelezo vya manabii Yesu, Ezekieli na Paulo vituhamasishe kuwa macho kwa mapitio ya Mungu na kuchukua ujumbe umetukabidhiwa kwa uaminifu na shauku.   

Fr Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: