domingo, 19 de julho de 2015

MAFANIKIO YA UJUMBE

Amosi 7: 12-15; Waefeso 1: 3-14; Mk 6: 7-13

      Nabii Amosi alichaguliwa na Mungu ili kutabiri katika rali ralisi ya ugumu ya watu wa Israeli (Ufalme wa Kaskazini), ni kwamba, kukosekana kwa usawa katika jamii, udhalimu dhidi ya maskini na matumizi ya dini kulingana na mvuto binafsi ya mfalme. Badala ya hekalu la Yerusalemu (Ufalme Kusini) lilikuwa na hekalu nyingine likaloitwa Betheli kwa muda wa mfalme Yeroboamu wa II. Amosi alipoanza ujumbe wake katika mahali hapo, alikutana na kuhani wa hekalu la Betheli, aliyeitwa Amazia, ambaye alifanya upinzani dhidi ya unabii wa Amosi. Amazia ni aina ya mtu aliyelipwa ili kudumisha mfumu wa hekalu na kuhalalisha mfumu wa udhalimu wa mfalme. Kabla ya kutendewa vibaya, Amosi alidhihirisha maana na hamasa ya wito wake. Ujumbe wake wa nabii hautegemei ada, bali ni ari ya bure ya Mungu na ni mwaliko kwa bure.

       Somo la pili ni wimbo wa shukrani kwa Mungu ambaye ametubariki katika Kristu tangu mwanzo wa ulimwengu. Maana ya upendo wake, sisi ni wana na mabinti wake. Kwa ujumbe wa Yesu Kristu tumesamehewa dhambi zetu ili tustawi wito wetu kwa utakatifu. Wito huu ni sehemu ya mpango wa hekima na wema wa Mungu ambaye katika Kristu ametuchagua ili tuwe watu wake mwenyewe. Roho wa Mungu anatusaidia kuishi wito wetu kwa uaminifu na atatupatia utimizaji wa ahadi yake. Kulingana na Baraza ya Vatikano ya II utakatifu ni wito wa mambo yote. Sisi sote tunaitwa kwa wito huu. Kulingana na Mt Yohana Calabria, “hatuhitaji kufanya vitu vya ajabu ili kuwa takatifu. Tunaweza kufikia utakatifu kupitia hali ya kawaida maishani ya kila siku. Inatosha kwamba nia zetu kufanya chochote ziwe takatifu.”      
      Baada ya kumekataliwa kijijini chake, Yesu aliendelea ujumbe wake vijijini kandokando pale ambapo alikaribishwa sana. Aliweza kufanya kazi yake peke yake, bali hakutaka. Kwa hivyo aliwaita Mitume kumi na wawili kama washirika. Kabla ya kuwatuma kwa ujumbe, aliwapendekezea uzoefu wa ndani wa uzima; akawafundisha kwa uwezo aliopokea kutoka kwa Baba; akashirika nao unyeti wake kuhusu hali ya huzuni na mateso ya watu; kabla yao alitenda kwa mamlaka dhidi ya nguvu za maovu ambayo yaliwapooza watu, yakiwazuia kushiriki kikamilifu katika jamii. Hatimaye aliwapa maelekezo, hasa kuhusu mahitaji ya njia ya unyenyekevu wa maisha na akawatuma wawiliwawili.    

     Ari ya mwito inatoka kwa Yesu. Hakutafuta wenye nguvu au wenye adhiri katika jamii. Aliwachgua watu wanyenyekevu, wafanyakazi na walio makini sana kwa upya wa Mungu uliodhihirisha na Mwana wake. Yaliyomo ya maelekezo yaliyopewa na Yesu yanaufuata mwelekeo tofauti kabisa wa mawazo ya binadamu. Ili kuwa na mafanikio katika ujumbe, mitume walikuwa lazima kushinda baadhi ya tabia za binadamu ambazo zipo sana maishani mwetu: dhidi ya tabia ya kutenda ya mmoja mmoja, tunaalikwa kutenda pamoja na kusaidiana katika jumuiya na kwa wema wa jumuiya; dhidi ya tabia ya kutawala, Yesu anatupendekezea uwezo wake ili tutumikie watu; dhidi ya tabia ya kuwa na mali, Yesu anatupendekezea kujinyima, unyenyekevu na bure; dhidi ya tabia ya kulazimisha, tangazo letu ni pendekezo, pendekezo la toba, la ukombozi, la mabadiliko ya maisha. Kama Yesu sisi lazima kuheshimu uhuru wa wengine.   


     Ujumbe ulioshirikiwa na Yesu na wanafunzi wake ulichukuliwa kwa sisi sote ambao ni wafuasi wake wapya. Ni muhimu sana uwazi kwa msukumo wa Mungu ili tuwe na hamasa kuchukua njia ya unyenyekevu wa maisha yanayopendekezwa na Yesu, kwa ujasiri na hakika kama Amosi hata tutapokuta upinzani dhidi ya ari zetu. Matarajio ya Yesu ni kwamba pendekezo la toba ambalo tunawatangazia wengine liwe maonyesho ya mabadiliko ambayo tumehisi kupitia mkutano na huruma yake. Ili ukarimu na bure iwe tabia daima katika ujumbe wetu ili kupitia kwetu Mungu apatie maisha mengi kwa wote.    

Fr Ndega

Nenhum comentário: