domingo, 26 de julho de 2015

HURUMA NA KUSHIRIKIANA KAMA NG’AMBO YA UANAFUNZI


Kutafakari kutoka Jo 6, 1-15

     Mara nyingi injili zinasimulia kwamba Yesu anavuka ziwa. Ikiwa haikuwa na maana maalum  hata kigezo, wainjilisti hawangekiongea sana. Mwendo huu unatafsiri njia sahihi ya Yesu na wale ambao wako pamoja naye wanaalikwa kufanya vivyo hivyo. Kwa hivyo kwa kawaida husemwa kwamba kuwa pamoja na Yesu ni kuwa dhidi ya mawazo ya jamii. Kutafakari huku kunataka kuimarisha changamoto ya ungano huu na mshangao inayokutwa katika ng’ambo hii.

      Kwanza kabisa, katika ng’ambo hii Yesu anaukabili umati wa watu, walio maskini, ambao wamekuisha pitia huruma yake kwa ajili ya wagonjwa wao na walitambua katika yeye tabia sahihi ya binadamu ambayo inaweza kutoka kwa Mungu peke yake. Yesu anachagua kuwako katika ng’ambo au katika upande mwingine kwa sababu pale wako maskini, wagonjwa, wanaoteseka na walio na njaa. Yesu hatoroki kutoka kwao, bali anawaendea, kuwezesha pia mwendo wa watu hawa kwa yeye. Yesu anapanda mlima pamoja na wanafunzi wake. Mlima katika Biblia mara nyingi una uhusiano na uzoefu wa ufunuo wa Mungu. Hali hii inatukumbusha Musa alipopanda mlima ili kuongea na Mungu. Milima iliyojulikana zaidi katika Biblia ni Horebu, iliyoalikwa pia “Mlima wa Mungu”; Sinai, ambapo Mungu alianzisha Agano na watu wake; na Tabor, ambapo Yesu alijibadilisha mbele ya wanafunzi wake. Ili kudhihirisha mpango wa upendo na ukombozi wa Baba, Yesu alitafuta daima ushirika naye. Kutokana na mlima na mkutano na Mungu, Yesu anaona vizuri mahitaji ya watu kandokando na mbele yake. Watu wana njaa and hali hii inauvutia uangalifu na huruma ya Yesu. Haiweki hali hii kwa yeye mwenyewe tu, bali anashiriki na wanafunzi wake, ikiwamo katika mwendo wa malezi kwa uanafunzi. Kila kitu ambacho anatenda kwa ajili ya watu ni sehemu ya kujifunza kwa wanafunzi.

     Katika “shule” ya Yesu, tunakuta aina mbalimbali ya watu na njia tofauti ya kumfuata Mwalimu. Kuna wanafunzi ambao kama Filipo wanafikiri kwamba ni lazima kwanza kuwa na pesa nyingi ili baadye kumsaidia mtu anayehitaji. Kuna wanafunzi kama Andrea ambao wanaamini kwamba ishara au ari ndogo zinakaribishwa, lakini hazina nguvu kuyatoa maisha mapya kwa wale wanaopoteza tumaini la kuishi. Kuna pia wanafunzi ambao kumfuata Mwalimu kwa uaminifu wanawaambia watu kuketi kama wenye uhuru na wanaostahili maisha ya kustahiki, ishara ya uzima wa milele. Aina hii ya mwanafunzi alijifunza kutumikia kwa kweli na anasaidia kwa kito kinachothamini sana kwa njia nyingine ya jamii.

     Katika mwendo huu wote kushirikiana kunaonekana kigezo kikuu, kwa sababu watu wote walishiba, wakiepa mkusanyiko/ukusanyaji na ubadhirifu. Kunatangaza ukweli mkubwa, ni kwamba, zawadi za uumbaji ni ukarimu wa Mungu, zilifanyika kwa wote na zinapaswa kupatikana kwa wote. Ikiwa kuna watu bila chakula ni kwa sababu kuna wengine wanaokusanya kwa wao wenyewe. Sisi sote tuna ushiriki katika mateso ya maskini na wenye njaa. Uamuzi/ufumbuzi kwa mgogoro wa kiuchumi katika mahali pengi pa ulimwengu si kununua au kuuza zaidi au chini ya zaidi, bali ni katika kugawanya/kusambaza zaidi. Baadhi ya vielelezo miongoni mwetu vinaonyesha kwamba inawezekana kupitia hali nzuri wakati kila mtu anatoa kutokana na umaskini wake. Hati za Kanisa katoliki, zikiuita uangalifu wetu kuhusu uovu wa miundo jeuri zinashutumu aina ya kuendeleza iliyochukuliwa katika nchi maskini “imetajirisha baadhi ya watu milele kwa muda imesababisha umaskini milele kwa wengine (Puebla n. 30).”


      Katika mazingira haya, kama jumuiya ya kikristu, tuna ahadi ya ushahidi halisi zaidi ili uwe kulingana na chaguzi za Yesu. Katika maneno mengine, ushahidi wetu lazima kuwa ufunuzi wa unabii, unaodhihirisha hali inayofichwa na yenye barakoa. Hofu ya kupoteza urafiki na upendeleo, mara nyingi, inaifunga mikono yetu na inanyamazisha sauti yetu. Ikiwa hatupati kuwa sauti ya wale wasio na sauti na wasio na nafasi, maisha yetu ya kikristu yanamaanisha nini? Watu wengi hawana chakula. Ikiwa hali hii haisababishi huruma na hasira kwetu, ujumbe wetu una maana gani? Umuhimu wa maisha yetu ni Ekaristi takatifu kupitia hii tunampokea Yesu, Mkate wa uzima. Kupitia Ekaristi tumeshiba njaa yetu ya Mungu na tunachukua ahadi ya njaa ya watu. Swali kuu kutoka hali hi ni, ekaristi inashirikiwa kanisani inamaanisha nini ikiwa hatupati kushiriki kile tunacho na mtu anayehitaji? Wakati mmoja tu awe bila chakula mpango wa Ekaristi hautakamilika. Siku hizi zaidi kuliko zamani ni lazima kupita kwa upande mwingine ikiwa tunataka kuandamana na Yesu ili kufanya utofauti maishani mwa watu.

Fr Ndega
Mapitio: Sara

Nenhum comentário: