terça-feira, 18 de dezembro de 2018

MWONGOZO KWA AJILI YA USOMAJI WA WARAKA WA SINODI YA MAASKOFU JUU YA VIJANA



“Vijana, imani na utambuzi wa wito”



UTANGULIZI
      Mwongozo huu unalenga kutuimarisha ili kusoma na kujifunza Waraka wa kimwisho wa Sinodi ya Maaskofu juu ya vijana ambayo yalifanyika katika Roma kati ya siku ya 3 na ya 28 ya Oktoba. Mbele ya utajiri wa maudhui haya, tunaweza kusema kwamba tuna mikononi mwetu kitu cha thamani kubwa, “kwanza kwetu”, kulingana na Papa Francisco. Waraka huu imegawanywa katika sehemu 3, sura 12, aya 167 na kurasa 60. Jambo ambalo linaongoza waraka mzima ndilo tukio la Wanafunzi wa Emau.

SEHEMU I - «ALITEMBEA PAMOJA NAO»

I. KANISA LINALOSIKILIZA
     Kusikiliza na kuona kwa huruma: Sinodi inasisitiza thamani ya kusikiliza. Mambo yote huanza kutoka kusikiliza kwa huruma: vijana wanataka kusikilizwa, kutambuliwa na kusindikizwa na wachungaji na walei wataalamu kwa upatikanaji na uvumilivu.

    Utofauti wa mazingira na tamaduni: inaita makini yetu kuhusu ulimwengu wingi na mabadiliko yake. Huu, kwa upande mmoja inawezesha maisha, lakini kwa upande mwingine inazalisha kutengwa na kubaguliwa. Ni muhimu kurejea nguvu ya imani. 

      Mtazamo mmoja kuhusu Kanisa leo: sehemu hii inazungumza kuhusu hamu ya elimu ya Kanisa ambalo linakusudia malezi kamili ya vijana. Shule na vyuo vikuu vina jukumu lao, lakini parokia lazima pia kufikiri kwa njia mpya kazi yake ya kiuchungaji ili iwe na kuvutia zaidi kwa vijana.

II. VIUNGO MUHIMU TATU
       Upya wa mazingira tarakimu: hii ni hali ambayo imejienea, ndiyo wavu wa fursa, lakini pia huleta pamoja nayo upande wa giza. Ni lazima tuingie katika hali hii kukabili kwa ujasiri uhusiano kati ya imani na changamoto za wakati huu wa sasa.

     Wahamiaji kama dhana ya wakati wetu: hilo ndilo jambo ambalo linaonyeshwa kwa njia wingi. Wahamiaji wengi ni vijana wenye kasoro, waathirika wa kila aina ya vurugu. Jukumu la kinabii la Kanisa limeelezwa na Papa Francisco kwa kutumia vitenzi nne: “kukaribisha, kulinda, kukuza na kuunganisha”.

      Kutambua na kujibu dhidi ya kila aina ya matukano: kuchukua kwa umakini ahadi na ukweli na kuomba msamaha. Kukabiliana na hali hii mbaya kwa maamuzi ya ukali. Sinodi ilionyesha pia shukrani na kutia moyo kwa wale ambao walikuwa na ujasiri wa kulaani hali hii.

III. UTAMBULISHO NA MAHUSIANO
     Familia na mahusiano kati ya vizazi: inaongea juu ya familia kama rejeo la kipendeleo, kwa kusisitiza jukumu la wazazi na uhusiano kati ya vizazi. Lengo hapa ni kushirikiana imani na kusaidiana katika ushuhuda.

    Mwili na Affectivity: kipindi hiki kinatukumbusha mabadiliko punde ambayo yaleta uhuru fulani juu ya mambo haya. Maadili wa kimwili wa Kanisa inafikiriwa na watu wengi kama hukumu. Ni lazima kupendekeza kwa vijana anthropolojia ya affectivity na sexuality ambayo iweze kutoa thamani kamili kwa usafi wa moyo kwa ajili ya ukuaji wa mtu katika hatua zote za maisha. Kuhusu ushoga, ni muhimu kuwasaidia vijana kuunganisha sehemu ya sexuality katika nafsi zao wenyewe, kwa kuongezeka mahusiano mazuri na wengine kwa ajili ya kujitolea.

     Aina za kuwa na kasoro: hali hii inatokea mbele ya kosa la kazi - ambalo linapunguza uwezo wa vijana wa kuota – mbele ya vurugu na mateso, yanayosababisha kubaguliwa. Sinodi inapendekeza mabadiliko ya moyo na mshikamano.

IV. KUWA KIJANA LEO
     Vipengele vya utamaduni wa kijana punde: Inatuomba kuthamini shughuli za michezo za vijana, ambazo zinaleta zenyewe uwezekano wa kielimu, wa kimalezi na wa jumuisho. Hasa muziki inachukuliwa kama chombo cha nguvu ya kuinjilisha na rasilimali kubwa ya kiuchungaji, kwa sababu inatoa vijana fursa ya kuonyesha vipaji vyao.

      Maisha ya kiroho na ucha Mungu: vijana wanaja kutoka miktadha ya kidini ya wingi na hii inadhihirisha utafiti mkubwa ya kidini. Wangependa kukutana na Yesu Kristo, hasa kwa njia ya liturjia hai na kweli, ambayo uzuri wa ishara, huduma ya kuhubiri na ushiriki wa jumuiya wasema kweli ya Mungu na hayo yote yapendezwa nao sana.

     Ushiriki na Protagonism: vijana wanataka kuwa wahusika wakuu; wanaomba waweze kuwa waamilifu katika uinjilishaji wa wenzao. Wanataka jumuiya za kikanisa ziwe za kindugu na kweli zaidi ambapo wajihisi kuunganishwa, waweze kuchukua majukumu na kuthaminiwa.

SEHEMU II - «MACHO YAO YALIFUNGULIWA»

       Pentekoste mpya: Roho Mtakatifu anafanya upya Kanisa na maisha ya kila mwamini.

I. KARAMA YA UJANA
    Yesu kijana miongoni mwa vijana: inaongea kuhusu ujana wa Yesu kwa kuwaalika wote kuangalia yeye. inafikiria kwamba kutoka kuangalia kwake tu inawezekana uzoefu kweli wa Mungu. Kutotulia kuzuri kwa vijana ni zawadi kubwa. Hao ni “mahali pa kitheolojia”, yaani, mahali ambapo Mungu yupo na kutoka huko anaongelea Kanisa na ulimwengu.

     Kuwa mtu mzima: inasisitiza umri wa ujana kama umri wa maamuzi. Ni jukumu letu kuwasaidia vijana kuishi kuwepo yao iliongozwa na ishara ya misheni kwa kutumia mafunzo ambayo yaweza kutoa changamoto na kuvutia. Tunapaswa kuwapa maana ya kweli ya mamlaka na kuwasaidia kuanzisha mahusiano ya kifamilia kwa njia ya kiinjili.

      kuitwa kwa uhuru: injili ambayo Kanisa linatangaza ni injili ya uhuru. Kristo hafuti uhuru lakini anaikomboa, yaani, yeye anatoa uhuru wa kweli na wa kijukumu, ambayo haiwezi kuishiwa bila undugu na mshikamano, hasa kwa ajili ya walio wa mwisho wa jamii.

II. FUMBO LA WITO
      Utafiti wa wito: dhana ya wito inahusiana na ile ya misheni. Kila maisha ni wito nao unamhusu Mungu. Wito sio jambo binafsi ambalo mtu linasimamia kwa uwezo wake peke yake. Kila wito wa kibatizo ni mwito wa utakatifu. Ni muhimu kusaidia mazingira kwa ajili ya kuendeleza utamaduni wa kweli wa wito katika jumuiya zote za Kikristo.

       Wito wa kumfuata Yesu: maisha ya Yesu bado yaendelea kuwa msukumo na kuvutia siku hizi. Ndiyo rejeo ambalo linapendekeza changamoto kwa vijana wote. Akidhihirisha fumbo la Baba na upendo wake, Yesu alifunua kikamilifu mtu kwa nafsi yake mwenyewe na kuonyesha wito wake mkubwa sana. Katika maana hii, Bikira Maria, mwanamke kijana, anatolewa kama mfano kwa sababu ya uwezo wake wa kukaribisha mwito wa Mungu na kumsaidia kwa ajili ya mipango yake. 

      Wito na miito: wito na utume wa Kanisa ni kusaidia ushirika na Mungu na miongoni mwa watu wote. Kwa ajili ya hali hii, yeye hutegemea namna nyingi za karama zinazo maonyesho ya utambulisho wake na zawadi za neema ambazo Roho hufufua daima Kanisani kwa ajili ya kulifanya upya. Kutoka ubatizo, sisi sote tumeitwa kwa utakatifu kwa mantiki ya imani na kujitolea unaoonyeshwa katika kila uamuzi wa maisha mtu anaofanya: ndoa, utawa, daraja, “single”, nk.

III. UTUME WA KUANDAMANA
     Kanisa linaloandamana: likifanya kazi yake ya mama, Kanisa huitwa kuwa karibu, kusaidia na kuandamana na safari ya vijana kuelekea maamuzi ya kweli. Kuandamana ni kuumega mkate pamoja na mahali pa kwanza pa mwendo huu ndiyo jumuiya yenyewe ambapo “wavu” wa mahusiano unaweza kumsaidia mtu katika safari yake na kutoa njia ya mwongozo. Kwa ajili ya utumishi huu, wanaitwa watu wote walio muhimu katika hali mbalimbali ya maisha ya vijana. Hii inajumuisha pia kuingizwa katika jamii.

       Kuandamana kwa kijumuiya, kwa kikundi na kwa kibinafsi: kuandamana ni Misheni ya kufanyika sio kwa kibinafsi tu lakini pia kwa kikundi. Katika kuandamana kwa njia ya kiroho, mtu anajifunza kutambua, kutafsiri na kuchagua katika mtazamo wa imani, kusikiliza kile Roho analopendekeza ndani ya maisha ya kila siku. Mwendo huu unaimarisha kutafuta sakramenti ya Upatanisho, kwa kuchukua jukumu na kuukaribisha utofauti kama fursa ya ushirika wa kidugu na ukuaji wa kubadilishana.

     Walioandamana wa ubora: shemasi Filipo anatolewa hapa kama mfano wa kuigwa: yeye anapatikana kwa Roho, anapata njia ya kuingia kwa uhusiano, anafanya maswali ambayo yasababisha uamuzi na kutoka nje ya tukio kwa unyenyekevu. Hivyo, yule anayeandamana anapaswa kuwa mtu uwiano, anayesikiliza, anayeamini na kusali; anajiona mtu wa udhaifu. Kwa sababu hii, anajua jinsi ya kukaribisha na kusahihisha kwa njia ya kindugu, bila tabia ya  kuwamiliki wala kuwadanganywa watu. Ni muhimu kutafuta malezi maalum kwa ajili ya utumishi huu.

IV. SANAA YA KUTAMBUA
      Kanisa, mazingira kwa ajili ya kutambua: kutambua ni mwendo wa kiroho ambao mtu, kikundi au jumuiya hutafuta kutambua na kukubali mapenzi ya Mungu katika halisi ya hali yake mwenyewe. Katika historia ya Kanisa, mwendo huu umekuwa na maana mbalimbali lakini mambo mengi ni sawa kati yao. Utambuzi hauwezi kupunguzwa kuwa mwelekeo binafsi peke yake bali ni jambo ambalo linajumuisha jumuiya nzima ambayo kwa nuru ya Neno yasikiliza lile Roho analopendekeza kupitia uzoefu wa kiroho wa wanashiriki wake.

     Dhamiri  katika mwendo wa utambuzi: dhamiri ni mahali maalum pa uhusiano na Mungu, ambamo sauti yake ndimo. Hii haimaanishi “kujitambua”, lakini inathibitisha uwepo wa kimungu. Malezi ya dhamiri ni kazi ya maisha yote na kuhitaji utunzaji wa ndani: ukimya, sala, sherehe ya sakramenti, mafundisho ya Kanisa na matendo mema.

      Mazoezi ya utambuzi: utambuzi unafahamika kama kazi ya dhamiri na njia ya kweli ya sala. Kwa kila mtu ambaye anaanza mwendo huu inahitajika uhusiano wa ndani na Bwana, mkutano mara kwa mara na mtu wa uongozi wa kiroho, sherehe ya sakramenti, tamaa ya moyo ya kusikiliza sauti ya Roho na nia ya kuweka utaratibu katika maisha yake mwenyewe. Jukumu la uamuzi huu huthibitishwa na uzoefu wa kindugu na utumishi kwa maskini.

SEHEMU III - «AKAONDOKA BILA KUCHELEWA»

      Kanisa kijana: picha ya Kanisa kijana tunaloota ndiye Maria Magdalena, ambaye akiishi upendo maalum kwa ajili ya Bwana, alienda kukutana na wanafunzi wengine na kusababisha harakati yao kwenye Yesu. Hivyo, Kanisa anataka kufikia vijana wote, kutembea pamoja nao na kupitia yao, kusikiliza sauti ya Bwana anayetuomba mabadiliko ya moyo na kufanya upya miundo. Vijana wote, bila kuacha hata mmoja, ndimo moyoni mwa Mungu na tena moyoni mwa Kanisa.

I. “SYNODALITY” YA KIMISIONARI YA KANISA
   Mabadiliko daima: vijana wanaomba wote watembee pamoja katika mwendo wa “kisinodi” daima. Kutoka Mkutano Mkuu huu na kutoka Waraka wa tukio hili, Mabaraza ya Maaskofu na Majimbo ya Kanisa yaalikwa kuendelea mwendo wa utambuzi kwa njia ya kishiriki na ya jukumu la kindugu kwa ajili ya kufafanua suluhu maalum za kiuchungaji.

    Njia kwa ajili ya utume: “sinodi” ni njia kwa ajili ya misheni ambayo inaomba tupite kutoka “mimi” kwa “sisi”, kwa kuzingatia nyuso mbalimbali, hisia, asili na tamaduni. Inahitajika kuthamini karama nyingi mbalimbali ambazo Roho huwapa wote kwa kuepuka clericalism na kuishi mamlaka kama utumishi. Ni lazima iwe njia ya “sinodi” pia mazungumzo ya kiekumeni na ya kidini: kuwa na parresia kwa kuongea na unyenyekevu kwa kusikiliza.

II. KUTEMBEA PAMOJA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU     
      Kutoka miundo kwa mahusiano: haja ya kutembea pamoja inahusu sio tu Kanisa kwa ujumla, lakini juu ya yote kila jumuiya moja. Hii inamaanisha kupita kutoka mantiki ya kumngoja mtu fulani afanye kitu kwa kufanya pamoja. Tunapaswa kufikiri upya kazi ya kiuchungaji ya parokia na miundo yake ambamo yatokee mahusiano ya kweli kwa ajili ya kusaidia uzoefu maalum maishani mwa vijana.

     Maisha ya jumuiya: jumuiya zetu zinaonyesha alama ya utofauti, mozaiki ya nyuso nyingi. Hii inaruhusu vijana waingizi katika maisha ya kijamii, kwa kuleta furaha ya injili. Katika tangazo na katekesi ni muhimu kufanya upya ahadi kwa ajili ya lugha na mbinu, lakini bila kusahau muhimu sana: mkutano na Bwana, kupitia uzoefu wa kiliturujia ambayo vijana wanakua katika hisia ya Diakonia, kwa kutafuta kujitolea na utumishi njia ya kukutana na Bwana.

      Kazi kwa ajili ya Vijana inayolenga wito: Kanisa linaitwa kuwa nyumba kwa ajili ya vijana, ambapo mtu anaishi hali ya familia kupitia imani na amini. Kama wito ni kiini ambapo mambo yote ya mtu ni yajumuisha, ndio kupitia hali ya wito ambapo uchungaji wote unapata msingi wa muunganisho. Kwa sababu hii kazi ya kiuchungaji nzima ya Kanisa ifanyike kwa kulenga wito, hasa ile ya vijana.

III. MSUKUMO MPYA WA KIMISIONARI
    Changamoto kuchukuliwa: mazingira ya kitarakimu – kujaza na injili tamaduni na mienendo yake; wahamiaji – kuwakaribisha, kuwalinda, kuwasaidia na kuwaunganisha; wanawake katika Kanisa – mabadiliko ya kijasiri ya mawazo ya kitamaduni na mabadiliko katika kazi ya kiuchungaji; sexuality – kupendekeza kwa vijana anthropolojia ambayo itoe thamani kamili kwa usafi wa moyo kwa kuwasaidia kuunganisha hali ya sexuality katika nafsi zao wenyewe; kuhusu uchumi, siasa, kazi – kusaidia na kuandamana ushirikiano wa vijana katika dunia hii ya kazi; Miktadha kati ya tamaduni, tena kati ya dini mbalimbali na mazungumzo ya kiekumeni - vijana Wakristo wanaitwa kuwa wamoja, kwa kujifungua pia kwa vijana wa mila nyingine na kushika nao mazungumzo ya kweli ambayo yalenge kuheshimiana na kuponya kutoka chuki na ubaguzi.

IV. ELIMU KAMILI
      Katika ulimwengu ambapo kila kitu ni kushikamana, inahitajika njia mpya ya mtazamo wa malezi ambao unaweza kuziunganisha hali tofauti za mtu. Uwepo wetu katika shule na vyuo vikuu unapaswa kuwa na maana kwa kulenga mtazamo wa malezi kamili ya vijana. Ni muhimu kuthamini uzoefu wa kimisheni wa vijana kwa kuwekeza kwa ukarimu hamu ya kielimu, wakati wa muda mrefu na pia rasilimali za kiuchumi. Mwishowe, Sinodi iliandaliwa mapendekezo matatu ili kuusukuma upya: kufanya nyakati ya malezi ya walei, watawa na mapadre pamoja; kujumuisha katika maandalizi ya upadre ama maisha ya Utawa maandalizi maalum kuhusu kazi ya kiuchungaji kwa ajili ya vijana; ndani ya mwendo wa utambuzi kuwa safari ya kimalezi kupitia uzoefu wa kijumuiya.

HITIMISHO
     Sinodi inatukumbusha kwamba sisi wote tumeitwa kuwa watakatifu na kupitia wito huu mmoja tu inawezekana kuendeleza aina tofauti za maisha. Vijana wanahitaji watakatifu wanaozalisha watakatifu wengine, hivyo inaonyeshwa kwamba “utakatifu ni uso mzuri sana wa Kanisa.” Hata vijana wanaweza kutufundisha mengi kuhusu huu. Kupitia utakatifu wa vijana, Kanisa linaweza kufanya upya hamu yake ya kiroho na nguvu yake ya kitume. Vijana wanatufanya kurudi kwa upendo wetu wa kwanza.

Fr Ndega

Nenhum comentário: