Kutafakari kuhusu Luka 2, 1-14
Kulingana na liturujia ya siku hii takatifu, ujumbe kuhusu kuzaliwa kwa Yesu ni ujumbe wa furaha
kubwa kwa wote, kwa sababu Mwokozi amezaliwa kwa
wote. Tufurahi kwa sababu Mungu
anatupenda, yeye yupo kati yetu
na analeta wokovu kwetu. Wokovu ni kazi
ya Mungu, lakini unatendeka duniani
na ushiriki wa binadamu. Basi tuchukue Mariamu na Yusufu kama mifano. Katika tukio
hilo la ajabu na unyenyekevu wa watu waliohusishwa,
Mungu alidhihirisha njia yake yenyewe ya kutenda. Hali hii inathibitisha msemo wa Afrika ambao husema, “watu wanyenyekevu,
kufanya vitu rahisi na katika mahali rahisi wana
uwezo wa kubadilisha ulimwengu.” Mabadiliko
makubwa ambayo jamii yetu
inahitaji lazima kutokea ndani ya
mwanadamu. Jamii mpya itatokea wakati kila mtu atatambua mahitaji ya kujibadilisha
mwenyewe zaidi kuliko ajaribu
kubadilisha wengine. Kulingana na
Baba Mtakatifu Francisco, “Dunia itabadilika
ikiwa tuanze kubadilisha matendo yetu kupitia tabia zetu na chaguzi zetu.” Kwa hiyo, Krismasi ni wakati wa kubadilisha tabia na chaguzi zetu.
Katika Yesu, Mungu amekuwa mmoja wetu, kuchukua hali halisi yetu ya binadamu na kulitoa pendekezo mpya
la maisha. Kwa hivyo haitoshi
kukiri katika Yesu
wokovu wa Mungu; ni muhimu
turuhusu kuongozwa na ujumbe wake wa
amani na upendo. Kuzaliwa kwa Yesu
kuliwabadilisha binadamu wote katika familia kwa njia ya kipekee,
kujaza mioyo ya watu kwa furaha na
matumaini. Kwa kweli, Mungu anajifunua
kama jirani, maskini
na anayekataliwa, kualika tutambue
thamani ya ishara ndogo na miradi
midogo. Bila shaka chaguo hili
la Mungu linatuaibisha, kutualika
kufikiri na kutenda tofauti. Kupitia udogo Mungu hufanya makuu. Hivyo,
Krismasi ni wakati wa kubadilisha mawazo wetu.
Kipengele kingine cha kutafakari kwetu katika usiku huu
ni kuhusu wachungaji,
waliokuwa watu wa kawaida wadharauliwa katika jamii. Wachungaji walikuwa watu waangalifu ambao walichunga wanyama wao
karibu na Bethlehem wakati wa usiku.
Walikuwa kweli waangalifu
kwa sababu ndani yao hisia kuhusu Mungu na
ukaribu wake ulikuwa hai sana. Wachungaji walikuwa
watu wa kwanza kuupokea ujumbe mkubwa
wa furaha kwa sababu mioyo yao ilikuwa macho. Yeyote tu aliye na moyo
makini ana uwezo wa kuamini katika
habari njema na kutarajia hali nzuri katika kila alfajiri
mpya. Mtu tu aliye na moyo makini
ana ujasiri wa kuanza safari kwa kukutana na Mungu katika
mahali pasipotarajiwa, yaani katika hali ya mtoto mdogo na mahali
maskini sana. Hivyo, Krismasi ni wakati wa kuangalia tofauti ili kuona zaidi
na kufanya tofauti katika maisha ya watu wengi.
Mungu Mwenyezi anakubali hali
ya mtoto mdogo, katika utegemezi
kabisa na utunzaji na upendo wa binadamu. Imani inatuongoza kumtambua mtoto huyu mdogo wa Bethlehemu katika
kila mtoto ambaye sisi hukutana katika safari yetu ya kila siku. Kila mtoto anaomba upendo wetu. Tufikiri
leo, kwa njia maalum, kuhusu baadhi
ya watoto ambao hawana uzoefu wa upendo
wa wazazi wao; kuhusu pia watoto wa mitaani ambao hawana mahali pa kuishi; kuhusu watoto ambao wanatumika kama askari, wanaobadilishwa katika vyombo vya vurugu,
badala ya kuwa vyombo ya upatanisho na amani; tena kuhusu watoto ambao ni waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, na kuhusu watoto
maskini waliolazimishwa kuziacha ndoto
zao kwa sababu ya hali mbaya ya
kiuchumi. Mtoto mdogo
wa Bethlehemu ni mapitio mapya ili
tuweze kujitoa ili dhiki ya watoto
hawa ikomeshwe. Mwanga wa Bethlehemu
uguse mioyo yetu, kuifanya yenye unyeti kwa hali hii. Hivyo, Krismasi ni wakati wa utunzaji na upendo
kwa walio na mahitaji mengi.
Ingawa sisi
huishi katika jamii ya ulaji ambayo
inatuzuia kushughulika kwa thamani muhimu
sana, tunapaswa kuwa macho. Krismasi
si ulaji. Ni sikukuu
ya ufunuo wa Fumbo la upendo wa Mungu unaobadilisha moyo wa binadamu
na kuufanya wenye unyeti kwa mapitio ya
Mungu. Mungu anatupenda bure na kwa
ukarimu, bila astahili kwa
upande wetu. Uzoefu huu lazima kutuongoza tufanye
vile vile anavyofanya. Kama hii,
Krismasi itakuwa zaidi kuliko kipindi kimoja
kwa mwaka. Itakuwa Krismasi daima ikiwa tujifunze
kupenda kweli na kuweka juhudi zaidi kwa kujenga jamii ya ndugu
na haki kwa wema
wa wote.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário