Kutafakari
kutoka Mt 1, 1-17
Kutokana na siku hii ya leo tunalianza juma maalum katika maandalizi yetu ya
Krismasi. Kwa hivyo injili inatuletea ukoo wa Yesu. Majina haya mengi
yaliyojulishwa na Mathayo yanatusaidia kufahamu mwelekeo wa binadamu wa Mwana
wa Mungu. Ni ushahidi kwamba Yesu hakuonekana ghafla wala ni mgeni katika
historia ya binadamu, bali tukio lake lilitokea polepole, hatua kwa hatua na
kwa muda mrefu. Mungu aliwaandaa watu wake kwa uvumilivu kupitia Mwana wake ili
historia hii ilikuwe na uwezo wa kumpokea katika wakati muafaka. Yesu Kristo
anakamilisha ahadi aliyoitoa Mungu katika Agano la Kale. Kwa sababu hii, Yesu
anatambulishwa kuwa ni mwana wa Mfalme Daudi na pia mzao wa Abrahamu. Mathayo
anatumia mifano mingi kutoka katika unabii uliotolewa na manabii wa Agano la
Kale, kueleza maisha ya Yesu ambaye alikuja kuwa Mwokozi wa Wayahudi (huu ni
ufahamu wa kwanza kuhusu utume wake). Lakini mpango na lengo la Maandiko
Matakatifu ni kuwasaidia watu kufahamu ufundishaji wa Mungu mwenyewe ambaye anatumia
watu fulani kwa kufikia wote. Kama hii Mwanao hakutumiwa ili awe mali ya
Wayahudi, bali Mwokozi
wa ulimwengu wote.
Kwa nini yeye ni Mwokozi wa ulimwengu wote? Ni muhimu sana kujipatia nia ya
Mungu kuhusu ubinadamu tangu uumbaji. Kwanza kabisa ulikuwa uamuzi wa Mungu kumwumba
binadamu kushiriki naye uzima wake mwenyewe. Upinzani asili kupitia dhambi haukumzuia
Mungu kuendelea mpango wake. Na, halafu aliamua kumwokoa binadamu mpotevu.
Mungu mwenyewe aliwaandaa watu wake kwa muda mrefu akiifanya historia yao kuwa
historia ya wokovu. Kwa sababu ya nia na matendo ya Mungu hatuwezi kuongelea
historia mbili, bali historia ya Mungu na binadamu, yaani Historia ya wokovu.
Mungu anamtafuta binadamu kumpa uzima wa milele ambao ni uhai wake mwenyewe.
Historia hii inatokea polepole kati ya mwanga na vivuli. Kizazi cha Daudi
kinaitwa kizazi cha mwanga kwa sababu ya mwelekeo wake kuelekea kwa Yesu.
Kizazi cha utumwa wa Babeli kinafikiriwa kizazi cha vivuli kwa sababu upinzani
wa watu dhidi ya mwongozo wa Mungu uliwazuia kuishi kama Watu wa Mungu.
Tunaweza kuongelea njia maalum ya kuingia katika historia ya binadamu. Mungu
anaingia katika maisha ya watu kwa wakati halisi. Yeye aliongea kwa namna
mbalimbali kupitia manabii na mababu zetu ya zamani na siku hizi anaongea
kupitia Mwanae mwenyewe. Yeye huongea kila wakati, lakini haongei hewani bali hupitia katika matukio
mazuri au mabaya katika historia ya
watu. Mungu alijifanya
mmoja wetu na bado yuko nasi kwa namna mbali mbali. Kwa kivyo hakuna tukio
lolote la historia lisilokuwa na maana. Angeweza kufanya kila kitu peke yake
bali hakutaka. Alichagua Maria, Yosefu, Yohane na viongozi wengi kama
washirika, akiingia katika historia kwa namna ya pekee na inabidi watu
watayarishwe kumkaribisha Masiya wake kwa wakati wote. Sisi ni sehemu ya mwendo
huu na kualikwa kumsaidia Mungu kwa mafanikio ya mipango yake kwa ubinadamu
wote. Tumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu katika historia yetu na kwa wito
wetu kama washirika wake.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário