domingo, 27 de setembro de 2015

KUTENDA MEMA KWA JINA LA YESU


Kutafakari kutoka Hes 11:25-29; Mk 9:38-43, 45, 47-48

Mungu hawabagui watu kwa maana anapenda na katika upendo hakuna ubaguzi. Maatarajio yake ni kwamba watu wake wote wangekuwa manabii, wanasikiliza neno lake na kuongea katika jina lake. Kupitia Roho wake Mtakatifu, anawahamasisha watu ili watende mema kulingana na mapenzi yake, akidhibitisha kwamba tendo lake halina mpaka. Mbele ya Mungu hakuna mtu wa heshima zaidi kuliko mwingine. Yeye hakubali umaarufu au ubaguzi, bali anatarajia ahadi kwa njia yake ya kufikiri na kutenda. Maana kwa njia hii ni upendo wake wa bure kwa wote.

Wanafunzi wa kwanza walijaribu kumkataza mtu fulani kufanya mwujiza kwa jina la Yesu kwa sababu hakuwa mmoja wao. Wlifanya hivyo kwa mamlaka gani? Yesu hakubaliani na tabia hii na akawaambia kwamba mtu ambaye anatenda mema kwa jina lake (Yesu) hawezi kumnenea mabaya. Kisha akiendelea kwa mafundisho yake, alisema kwamba watu wanaosaidia wafuasi wake watapokea tuzo kwa sababu ya utambulisho wake na wale waliotumiwa katika jina lake. Yesu anawakumbusha pia kwamba juhudi yote ya wale wanaomfuata lazima kuwa hamasa kwa wale ambao wanaanza kumwamini Kristo au wana ugumu kumwamini. Kashfa ni jambo mahututi sana na ni lazima kuepukwa kwa sababu huivuruga imani.

Tumetafakari kuhusu ugumu wa wanafunzi wa Yesu kuelewa na kuyapokea mafundisho yake. Wanaelewa nusunusu, hasa ile sehemu rahisi, wanaipokea na kuacha yaliyo magumu. Ni hatari mno kuelewa nusu ya ukweli kwa sababu kama hii tunaweza kuleta uzushi. Kujaribu kumkataza mtu fulani ambaye alifanya mema kwa jina la Yesu ni ishara ya ugumu ya kumfahamu Yesu na mapendekezo yake. Maana ya kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu si maneno tu, bali ni matendo mema hata kama mtu huyu hayumo kwenye kundi. Badala ya kuwakataa wengine ambao wanatenda mema kwa jina la Yesu, wanafunzi wake wanapaswa kujikataa wenyewe. Kuwa mwanafunzi wa Yesu inamaanisha imani iliyoonyeshwa kwa matendo. Kwani wao wanaokiri na kutenda kama kadiri ya neno” ndiyo mama na ndugu zake na wanafunzi wake. Ikiwa huyo mtu alitenda mema kwa jina la Yesu, tayari alikuwa mwanafunzi wake. Mtazamo wa wanafunzi una upungufu na ubaguzi, lakini mtazamo wa Yesu ni mpana na ni kwa wote wenye mapenzi mema.

Kitu muhimu katika dini au imani ni matendo na siyo maneno. Matendo husema zaidi ya maneno. Mifano halisi ni wakristo wa kwanza, waliweza kuwavuta wengine si kwa maneno, bali njia yao ya maisha. Kuhusu wao watu walisema: “Mwone kama wanavyopendana”! hali hii iliwezekana kwa sababu ya upendo wao ulionyeshwa kupitia ridhaa wao kwa wao, kushiriki pamoja, uvumilivu katika maombi pamoja na unyenyekevu wa moyo. Kuhusu hayo Sinodi ya Afrika imesema: “Sharti muhimu la kuhubiri ni ushuhuda wa maisha”. Mwanafunzi wa kweli wa Yesu hawezi kuwa na ubaguzi na kuamini kuwa watu wa kundi lake pekee, au chama chake cha utume, au kanisa lake ndiyo wanafunzi pekee wa Yesu na wameokolewa. Hatuwezi kufikiri kwamba Yesu ni mali yetu. Ikiwa tunahisi karibu na Yesu, hatuwezi kuishi mbali sana na ndugu zetu, kufungwa kabisa kwa hali kandokando yetu na hata kufikiri kwamba tunakuwa na mamlaka ya kuwazuia wengine watende kwa jina la Yesu. Tuko mbele ya kosa kubwa. Sisi lazima kuwa makini sana kuhusu baadhi ya uzoefu ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine na kutambua mema ambayo wanaweza kufanya imani yetu ni utenganisha. Basi, ili Mungu atufundishe kutambua mwendelezo wa kazi zake mbele ya matendo mema ya wakristo na kusaidiana kwa wema wa wote.

Fr Ndega

Mapitio: Sara

Nenhum comentário: