Wis 2:12.17; Jas 3: 16-4:3; Mk
9,30-37
Kifungu hiki
kutokana na kitabu cha Hekima ya Sulemani kinaongea kuhusu ushuhuda muhimu wa mtu
mwenye haki na upinzani wa wale ambao hawaukubali ushuhuda wake na wanamtendea
vibaya, kupanga mauti yake. Hali hii inatokea kwa sababu ya njia ya maisha yake
kulingana na mapenzi ya Mungu. Njia hii inawasikitisha wale wanaopendelea
kuishi vibaya, mbali na Mungu. Hata hivyo, mtu huyo mwenye haki ni mwana wa
Mungu, na Mungu mwenyewe atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui zake. Hii
ni ishara ya Kristo, aliye Mwana wa Mungu kwa namna ya pekee kabisa. Yeye,
katika uaminifu wake kwa mpango wa Mungu, alipata wokovu hata kwa wale
waliwakandamiza wengine. Somo la pili linasema kuwa hekima ambayo inasababisha
kujua kamili inatoka kwa juu kwa sababu ni Mungu mwenyewe chanzo cha hekima ya
kweli. Mtu anayeongozwa na hekima hii anaweza kuwa mwenye moyo safi, tena ni
mtu wa amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu na kutenda mema kwa
ajili yao.
Injili ni
mwendelezo wa tangazo la Petro kuhusu utambulisho wa Yesu na mwaliko wa Yesu
mwenyewe kwa wafuasi wake wamfuate katika kujisalimisha kwake ili wapate uzima.
Yesu alitambua kwamba wakahitaji kujua zaidi kuhusu maana ya umasiha wake na
kuyafahamu vizuri mapendekezo yake. Kwa hivyo alitumia kipindi maalum kuwafundisha
peke yao kuhusu maana kamili ya umasiha aliochagua na uanafunzi. Hakutaka watu
wafahamu alipo. Yesu alijaribu tena kuongea na wanafunzi kuhusu mateso, kifo na
ufufuko wake, lakini walionekana mbali sana na mwalimu. Hawakuelewa tena kwa
sababu walishughulika sana kwa mawazo na nia tofauti. Hata hivyo Yesu anatumia
mifano ili waweze kufahamu ufunuo wake. Vipengele vya msingi vya ufunuo huu ni,
maana ya kuwa wa kwanza katika ufalme wa Mungu, jinsi ya kumpokea na hatimaye
kuwa watumishi katika ufalme wake.
Yesu
anadhihirisha utambulisho wake kama Mwana wa Adamu (mtu). Katika Agano la Kale
tunakuta maneno haya katika kitabu cha nabii Danieli na Ezekieli. Kulingana na
Daniel Mwana huyu ni hali ya utukufu wa yule ambaye atakuja siku ya mwisho (Dan
7:13). Kulingana na toleo la Ezekieli maneno Mwana wa Mtu yanatumika kueleza
ubinadamu na kifu chake (Ezk 2:1,3:1, 25, 17:2). Hii ni maana iliyotumiwa na
Yesu ili kuongea kuhusu utambulisho wake kwa uhusiano na hali ya binadamu na
fumbo la mateso, kifo na ufufuko wake kwa ajili ya wenye dhambi. Kulingana na injili
ya Marko Yesu ni mwenye unyeti mbele ya hali ya ujinga na udhaifu wa wanafunzi
wa kwanza; aliwafundisha polepole na kwa uvumilivu, akitumia mifano kadiri ya
mazingira na akili zao na kufungua ufahamu wao ili waelewe mpango wa Mungu.
Mtoto alijulishwa na Yesu ni tena sehemu ya ufundishaji na tabia yake ya ajabu.
Watoto
wadogo wana mahali maalum moyoni mwa Yesu. Alisema kwamba Ufalme wa Mungu ni wa
watoto na mtu ambaye anataka kuingia katika Ufalme huu anapaswa kuwa kama wao.
Siku hizi Yesu anatuongelea kwamba ni lazima mabadiliko ya mawazo na tabia ili
tuweze kumfuata kwa kweli. Tena rejea kwa njia hii ni watoto wadogo ambao wana
tabia kamili katika uhusiano wao na Mungu na wengine. Wanatusaidia kutafuta
muhimu zaidi ya maisha yaani ukweli, unyenyekevu wa moyo, ufukara na imani kama
mtoto mchanga kwa uhusiano na wazazi wake. Kama wanafunzi wa kwanza sisi pia
hatupati kufahamu kila kitu kumhusu Yesu na mapendekezo yake, lakini ikiwa
turuhusu, yeye anaweza kufungua akili zetu na kubadilisha mioyo yetu ilingane
na matarajio yake. Ili mfano wa watoto wadogo utusaidie kufahamu nia za Yesu
kuhusu maisha yetu na kukubali mapendekezo yake ili tupate uzima.
Fr Ndega
Mapitio: Sara
Nenhum comentário:
Postar um comentário