sexta-feira, 26 de setembro de 2014

NINI HATUWEZE KUFICHA?



Kutafakari kutoka Luka 8,16-18

Wafuasi wa Yesu ni nuru duniani. Nuru ilifanywa kuangaza na inatimiza mwisho wake unapotoa uwazi na maisha kwa wote. Ilikuwa hivi mwanzoni: wakati Mungu alisema “Na iwe nuru” na uhai ukatokea. Yeye ambaye anajiruhusu Kuongozwa na mwanga ana uwezo mzuri wa kuona ili kufikia malengo yake. Ushuhuda wa wafuasi wa Kristu unaelimisha maana ya watu ambao wanatafuta sababu ya kweli na upeo kwa maisha yao.
Kama wafuasi wa Yesu, tumechukua jukumu kuwa mwanga. Tunaelimishwa kwa Neno lake kila siku ili kuelimika kupitia mwanga wa nuru hii. Kulingana na Yesu mazoea haya ya kuelimishwa hayaweze yakafichwa. Kuficha mwanga inaueza maanisha unyenyekevu, lakini inaueza kuwa udanganivu pia au kukosa la uhalisi. Katika jinsi hii mwanga hautimize muisho wake. Wakati matendo yetu yanafanika kwa Mungu hatuna sababu kuyaficha. Kama tunahitaji kuficha baadhi ya matendo ni kwa sababu ya kukosa nuru ya kweli, nuru ya ukweli. Siku moja tutapoteza vifuniko vya macho na itadhihirishwa watu ambao sisi ni kweli.  
Neno la Mungu ni taa kwa hatua zetu na mwanga katika njia yetu ". Ufunuo wake unatokea kwa wingi lakini mapokezi yetu si katika kipimo sawa. Kama kuna baadhi ya kikomo, haikuji kutoka kwa Mungu, lakini inatokana na uwezo wetu mdogo wa mapokezi ya siri yake. Hapa ni muhimu ufunguzi: zaidi ya kufunguliwa kwetu ni rahisi kuelewa nini Mungu anatarajia kutoka kwetu. Kwa maana hiyo ni lazima kuangalia jinsi tumesikiliza Neno la Mungu. Kama tunalisikiliza na upatikanaji wa wakati na ukarimu wa moyo wetu, tutapata matokeo mazuri kwa maisha yetu. 

Hivyo, Yesu anatualika kuyakaribisha maneno yake kama mwanga na kuangazia kutoka kwa mwanga huu. Msukumo ambao tunapata kutoka kwa Neno lake haliwezi kufichwa. Vinginevyo, hilo huwa bila maana kwa ajili yetu na kwa wengine.    

Fr. Ndega
Mapitio: Rose Mong’are na Mwalimu Patrick

Nenhum comentário: