Kutafakari toka Luka - aya 4, sura 16-30
Yesu anashiriki na marafiki mji zake mpango wake wa maisha. Alichagua kufanya hivyo
wakati wa kiliturujia ili kutangaza kipaumbele cha kazi yake. Yeye akiongozwa na Roho Mtakatifu, alitangaza habari njema kwa maskini na ukombozi
kwa wanaoonewa, anayafufua matumaini yake na kuwarudishia furaha ya maisha yao.
Yesu
anaishi kwa furaha na
shauku utambulisho wake kama aliyechaguliwa kutangaza mpango wa upendo
na wokovu wa Baba yake. Mungu
anapenda kila mtu na kutaka kufikia kila mtu kwa upendo wake. Hata hivyo, ana mahangaiko makubwa kwa baadhi ya watu ambao wanahitaji huduma maalum, kwa sababu wanakataliwa na jamii.
Yesu kama wokovu wa Mungu,
yeye ni utimizaji wa Maandiko, lakini katika jumuiya yake alikataliwa kwa wale walijiona waliojua Maandiko. Labda walizoea
kukubali tu kile ambacho ni kulingana na mawazo yao, akirekebisha Neno la Mungu kwa njia yao ya maisha, bila tabia
nzuri ya kuishi mapendekezo yanayotokana na Neno hili.
Kama watu kutoka Nazareti, mara nyingi sisi pia tumelipinga Neno la Yesu linalouliza maswali kuhusu njia yetu ya kuishi na kudai ahadi kubwa kuhusu hali ya wengine,
hasa maskini. Hatuwezi kufikiri kwamba habari tumepokea kuhusu Yesu inatosha
kwa safari yetu ya wito. Ni muhimu kuruhusu kwamba yeye mwenyewe aweze kujidhihirisha
kwetu kwa nguvu yote ya upendo
wake. Tukaribishe ufunuo huu
wa Yesu leo kama mwaliko ili tufikiri
vizuri kuhusu vipambele vyetu vya thamani
na kuchukua ahadi ya mshikamano kwa ajili ya wengine.
Fr. Ndega
Nenhum comentário:
Postar um comentário