Kutafakari kutoka kwa Mathayo 1,18-23
Yesu ni habari njema kwa Mungu, alitangazwa na manabii kwa muda mrefu.
Kuzaliwa kwake kulifanyika katika hali halisi ya binadamu, kuonyesha dhamira ya Mungu
na hali hiyo. Katika aya, kabla ya andiko la leo, Mathayo anaonyesha orodha ya mababu
wa Yesu, anathibitisha uwiano wa
Yesu na hali binadamu kama mwana wa familia ya Daudi. Ingawa andiko hili
linaongea kuhusu hali ya ubinadamu
wa Yesu, linashahidi pia asili yake na umungu
wake. Yeye ni Immanueli,
ambayo ina maana, "Mungu yu pamoja nasi". Jina lake linamaanisha ujumbe
wake: Yesu-Mungu ni mkombozi. Hivyo, yeye
alikuja kudhihirisha mpango wa wokovu
wa Mungu kwa wanadamu
wote.
Siri ya Neno la Mungu, aliyefanyika mwili, inafuata
nguvu ambayo ni kinyume
na matarajio ya binadamu, ni
kwamba, mahali rahisi (Nazareth, Bethlehem), watu wanyenyekevu (Mariamu na Yusufu),
hakuna kuanzishwa, lakini mwaliko. Andiko linatuelekeza kwa Mariamu na Yusufu kama washirika
muhimu kwa Mungu
katika utambuzi wa mpango wa wokovu wake. Mariamu, kwa
jibu lake la ukarimu (ndiyo), anatoa kwa
Mungu upatikanaji wake na akawa mtumishi mwaminifu wake. Yusufu, kwa kutii kwa kimya
yake, anashinda tabia ya ubinadamu kutenda juu ya msukumo na, kama hii, anaruhusu kwamba Mungu adhihirishe mipango
yake. Yusufu anathamini zaidi mapenzi ya Mungu kuliko
yake mwenyewe.
Kama Mariamu na Yusufu, sisi pia tulioitwa na Mungu ili tushirikiana pamoja naye katika
utekelezaji wa mipango yake. Katika jibu lake, Mariamu alitufikiri na alitufungulia mtindo bora ili yanahusiana
kwa ushauri wa Bwana. Ni vizuri kufuata mtazamo
wake wa upatikanaji na ukarimu. Wakati Mungu anataka mtu fulani kwa utumishi ya watu wake, yeye husalimu
amri, lakini anaheshimu uhuru wa
kila mtu. Yeye anajua kuhusu mpungufu wetu, mbele ukuu wa mipango yake, lakini hata hivyo
anataka ushiriki yetu. Kile tunafikiria
si muhimu sana kwetu si sawa kwa Mungu, kwa sababu Yeye ana uwezo wa kutambua kisicho wezekana na katika Ufalme wake, ndogo ni kubwa zaidi. Kwa maana hiyo hatuwezi kuweka upinzani au kizuizi dhidi ya hatua yake. Kinyume chake, hebu tujiachilie
mikononi mwake kama Mariamu na
Yusufu, kwa kuamini kwamba Yeye anajua anachofanya.
Fr. Ndega
Mapitio: Rose
Mong’are na Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário