Mimi ni Josuel dos
Santos Boaventura, lakini ninapenda zaidi kuitwa Ndega kwamba inaazimu “Mtu mwema”.
Nilizaliwa tarehe ishirini na sita mwezi wa saba mwaka wa elfu moja mia tisa
sabini na tatu. Nimetoka Brazil. Jimbo langu ni Bahia na Jina la mji
nilipozaliwa ni “Cachoeira”, lakini niliishi daima katika “Conceição da Feira”,
kwamba unaitwa pia “Cidade Ternura”, ni kwamba, “Mji wa Huruma”. Niliishi Utoto
wangu wote Mjini huo mpaka kwenda seminarini katika mji mwingine, unaoitwa
“Feira de Santana”. Shule yangu ya msingi iliitwa “Grupo Escolar Hermilo
Cardoso” na Centro Educacional Yeda Barradas Carneiro. Shule yangu ya sekondari
iliitwa “Colegio Estadual”. Nilianza kuenda shuleni kuandamana na binamu yangu.
Baada ya wakati huo, nikaweza kuenda peke yangu. Nilisoma na nilifanya kazi
ngumu sana. Hata hivyo nilipata muda pia kujifunza na kucheza mchezo wa
“capoeira”.
Nina familia kubwa
kwamba inaitwa “familia ya kasisi”. Baba yangu anaitwa Martins Santos
Boaventura. Kazi yake ni kuviweka tayari vyuma kwa kujenga nyumba kubwa. Yeye
anapenda kucheza “capoeira” na anacheza ala za muziki vizuri sana. Mama yangu
anaitwa Clementina dos Santos Boaventura na anapenda kushona na kutumikia
kanisani. Wazazi wangu wangaliendelea wenye nguvu na wananiangalia na upendo
muhimu. Nina dada mmoja na kaka sita. Dada yangu anaitwa Joelma na anafanya
kazi mkahawani. Kaka yangu mkubwa anaitwa Jose Roque na anafanya kazi kama
bawabu wa benki. Kaka yangu Josemir ni polisi. Kaka yangu Josafaa ni mwalimu wa
mchezo wa “capoeira” na mchezo wa ndondi. Kaka yangu Josival anafanya kazi
katika kiwanda cha
karatasi. Kaka yangu Juvandro anafanya kazi katika jiko la watawala wa mji wetu. Mzaliwa wa mwisho Josias ni bawabu wa Kampuni
inayochukua pesa.
Katika familia yangu nilikuwa
daima mtu maarufu katika sanaa, hasa sanaa ya muziki na kusoma. Kaka zangu na
dada yangu walisoma mpaka shule ya sekondari. Nilitaka kuendelea kusoma zaidi
ya kaka na dada zangu kwa sababu tangu mtoto mdogo wito wangu ukawa kuwa
kasisi, na ili kuwa kasisi ni lazima kusoma sana. Jumapili nikapenda kuenda
kanisani kwa misa na kutumikia kama mvulana wa madhabahu. Kama hii, niligundua
wito wangu. Wakati mkuu wa maisha yangu ulikuwa nilipoingia seminarini. Kabla
ya kuingia seminarini, Nilikuwa nimesitawi tayari vipaji vingi vya muziki kama
kuimba na kupiga ngoma. Katika seminari nilipata nafasi kujifunza ujuzi
mwingine ambao umenisaidia katika kazi yangu halisi.
Mimi ni kasisi wa
Shirika “Poor Servants of Divine Providence”. Nilikuwa kasisi katika terehe ishirini
na sita mwezi wa kwanza mwaka wa elfu mbili na mbili. Niliondoka kutoka kwa familia
yangu katika Brazil na ninaishi katika Ongata Rongai tangu terehe kumi na nane mwezi wa kuanza
mwaka wa elfu mbili kumi na tatu. Nilikuja hapa kwa kufanya kazi katika nyumba
ya malezi. Jiukumu hilo
linanihitajia busara
na uangalivu daima.
Zaidi ya jukumu hilo, ninapenda muziki na “capoeira” kwa sababu inafaa kwa
afya, mizani na fikira.
Fr. Ndega
Mapitio: Mwalimu Patrick
Nenhum comentário:
Postar um comentário