domingo, 19 de abril de 2020

KUWA CHOMBO CHA HURUMA YA MUNGU



Kutafakari kuhusu Yoh 20,19-31



            Jumapili hii inaitwa “Jumapili ya huruma”. Tuko na mengi ya kujifunza kuhusu jambo hili lililo tabia ya msingi ya kitambulisho yetu ya Kikristo. Yesu mwenyewe anatuhakikishia: “Heri walio na huruma, maana watahurumiwa” (Mt 5:7). Kulingana na Baba Mtakatifu Francisco, “Yesu Kristo ni uso wa huruma ya Baba. Fumbo la imani ya Kikristo linaonekana kukuta awali yake katika neno hili (...) Tunahitaji kutafakari fumbo la huruma. Hiyo ndiyo chemchemi ya furaha, utulivu na amani.”

Somo la kwanza linaongea kuhusu njia ya Wakristo wa kwanza ya kuishi kilicho kipimo cha utambulisho wa jumuiya za Kikristo za nyakati zote. Wakristo wa zamani walipata mafanikio katika safari yao kwa sababu ya vipimo vinne, yaani “mafundisho ya mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.” Njia ya kuishi kama wamoja iliwavutia wengine wengi ambao walitambua katika matendo yao ya ajabu tendo la Bwana aliye Mfufuka. Hivyo,  kwa ushuhuda wao watu wengi walikutana na huruma ya Mungu.

Akiongea na watu wa Jumuiya za Kikristo ambazo zilikabiliana na migogoro mingi, Petro aliwahamasisha kwa maneno ya kutia moyo akiwaalika kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake kubwa. Kwa ufufuko wa Kristo yeye Mungu alitufanyisha kuzaliwa tena kwa tumaini hai ambayo haikatishi tamaa. Ingawa tukabiliane changamoto na mateso mengi tunaalikwa kuishi imani yetu kwa furaha na kwa ahadi mpaka tupate lengo la imani hii, yaani wokovu.

Baada ya kuona ukatili kwa Bwana wao, wanafunzi wa Yesu waliishi katika mazingira ya hofu. Hawakutaka kuwa na mwisho sawasawa wa mwalimu wao, lakini waliendelea wanakutana hata kwa siri. Mambo mengi ambayo walijifunza kutoka kwa Yesu yalikuwa maana ya utambulisho wao. Basi, ingawa walikuwa na hofu hawakuwa wasio na tumaini kwa sababu yule aliyewaita kumfuata hangewaacha peke yao. Kweli aliwataka kama mashahidi wake.

Akijua kwamba walihitaji msaada, Yesu aliwajia akiingia bila kufungua milango na kusimama katikati yao kwa sababu alitaka kuwa rejeo maishani mwao. Bwana Mfufuka ndiye mwenye uhuru na kupanga kufanyisha wenye uhuru wale ambao wanamfuata. Wanafunzi hawa walikuwa watumwa bado, yaani watumwa wa hofu zao, wa mashaka yao, wa mawazo yao ya Masihi yaliyokatisha tamaa na moyo wao wa kijiwe. Yeye alikuja kuwasaidia kushinda yote hayo katika safari yao ambayo yaliwazuia kumshuhudia kwa kweli.

Matokeo ya kwanza ya uwepo wa Bwana Mfufuka kwa wanafunzi ni furaha, yakithibitisha kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni kuwa mwenye furaha. Furaha inaifungua milango ya moyo kwa kuzipokea zawadi zingine. Bwana Yesu anawapa amani kama utambulisho naye aliye “Nabii asiye na ukatili”. Hivyo walikuwa vyombo vya amani. Pumzi ya Roho Mtakatifu ni ishara ya maisha mapya kwa ubinadamu uliofanyika upya kabisa kwa msalaba na ufufuko wa Kristo. Watu wapya hawa wakiishi kwa ushirika na Yesu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu walitumwa kwa wajumbe wa huruma ya Mungu kwa kupitia msamaha na upatanisho. 

Thomas hakuwepo katika mkutano wakati Bwana Mfufuka alijionyesha akitoa zawadi zake. Hakika Thomas alipendelea uzoefu tofauti, yaani uzoefu wa “nje ya jumuiya.” Kutokuwepo huko kunamaanisha vipengele viwili:  Kwanza, Thomas ni mfano wa wale ambao wana ugumu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Kutokuwepo huko ni hatari kwa uzoefu wao wenyewe na kunaweza kuweka vikwazo kwa imani ya wengine.

Kwa upande mwingine, tunaweza kusema kwamba mfano wa Thomas unafanya jumuiya kushuhudia imani yake kwa kweli na kuaminika.  Haitoshi kusema “tumemwona Bwana!”. Bali ni lazima kumtambua na kumtangaza bila hofu kama “Bwana wangu na Mungu wangu!”. Kwa sababu ya Thomas, Yesu anatangaza maneno haya ya ajabu, yaani “Heri walioamini bila kuona.”

Kupitia mitume yake kama msingi Yesu ametupa zawadi ya imani na kutuomba tuishi imani hii pamoja na wengine, kwa kupendana na kusaidiana kama matokeo ya maisha mapya kutokana na ufufuko wa Bwana wetu. Mtu ana ugumu wa kuamini ikiwa anaamini peke yake. Imani yetu ni matokeo ya uzoefu wa kikanisa, kwa sababu imani ya Kanisa inaitangulia, inaizaa na kuiimarisha imani yetu. Bila ushiriki kwa hamu katika Jumuiya ya kikanisa, tuko na ugumu wa kutambua ishara za uwepo wa Bwana Mfufuka miongoni mwetu na imani yetu inakuwa haba na tena ndiyo hatari kwa imani ya wengine.

Andiko hili linatusaidia kutambua umuhimu wa kushiriki pamoja katika jumuiya. Bwana Mfufuka alitaka kujifunua kwetu kupitia msaada wa wengine. Tunapaswa kuwa macho kwa mwelekeo wa ubinafsi katika jamii ambao umeshawishi mahusiano yetu ya wanafunzi wa Kristo na kuuvuruga undugu wetu. Kwa njia ya ubinafsi maovu mengi yanatujia. Ni lazima kumchukua Yesu kama kipimo cha uzoefu wetu wa jumuiya nayo jumuiya inapaswa kuwa na nafasi muhimu katika maisha yetu ili tuweze kushinda hofu na kutokuwa na imani ili ushuhuda wetu uwe ufanisi katika hali iliyo kandokando yetu.

Fr Ndega

Nenhum comentário: