sábado, 27 de outubro de 2018

IMANI YETU INATUFANYA (INATUZUIA) KUONA NINI?


Kutafakari kutoka Yer 31,1-7; Wab 5,1-6; Mk 10, 46-52


     Kifungu cha Yeremia ni mwaliko wa furaha kwa sababu Bwana anapanga kutenda mambo ya ajabu katika maisha ya watu wake: hakika, kazi hii imekwisha anza. Yeye ndiye Baba amejaa upendo kwa ajili ya watu wake, hasa kwa ajili ya wadogo na wasio na nguvu miongoni mwetu. Yeye huvutia kwake kila anayeishi ili kufanya uzoefu wa wokovu wake kwa sababu “upole wake unafikia kila kiumbe.” Anatuambia leo: “Wewe ambaye husikiliza, wewe unayeteseka, wewe unayependa nawe unayesali, wewe ni mwanangu mpendwa, binti yangu mpendwa!” Mbele ya Mungu ambaye anatenda hivyo kwa ajili yetu, tabia yetu lazima kuwa ya amini kabisa, tukiacha nafasi kwa tendo la neema yake katika maisha yetu, yaani, kuruhusu Mungu awe Mungu ndani yetu.

       Kifungu cha waraka kwa Wayahudi kinaleta mfano wa kuhani ambaye amechaguliwa miongoni mwa watu na kufanya wakfu kwa manufaa yao. Yeye amevaa udhaifu na kwa hivyo anaweza kuhisi huruma kamili kwa ajili ya wanaokosa. Ukweli huu inamzungumzia Yesu Kristo, Kuhani wa kweli, ambaye “anakusanya katika nafsi yake udhaifu wa mtu na nguvu ya kufanya upya wa Aliye juu.” Yeye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” bali ndiye Baba aliyemtukuza. Sisi pia tangu ubatizo wetu katika Kristo, tuko na heshima ya kikuhani iliyo huduma ya wokovu. Kwanza ya yote hii ni zawadi ya Mungu nasi mbele ya hali hii tunapaswa kujibu kwa uaminifu na furaha. Tunasaidiwa na neema yake na jumuiya ya imani ili tuweze kuishi wito wetu kama zawadi kwa ajili ya wengine.

        Kifungu cha injili anaongelea kuponywa kwa Bartimayo na, basi, ufunuo wa Yesu kama mwanga ambaye anatupa mtazamo mpya. Muujiza huu ulitokea wakati Yesu alikuwa anaondoka mji wa Yeriko, yaani, katika pembezoni. Yeriko ni mmoja miongoni mwa miji ya zamani ulimwenguni. Mji huu ni eneo la baadhi ya matukio makuu ya biblia; hata katika muda wa Musa iliongelewa kuhusu mji huu. Tukumbuke “kuzingirwa na kuchukuliwa kwa Yeriko” na Waisraeli katika wakati wa Yoshua (Yoshua 6, 1-27). Tukumbuke pia Zakayo; mabadiliko ya maisha yake yalitokea katika Yeriko. Mji huu ni karibu na mto Yordano na Yesu alipita mahali huko mara nyingi. Andiko la siku ya leo linaongea kuhusu mkutano wa Yesu na kipofu Bartimayo, aliyeketi kando ya barabara ya mji. Hakika alikwisha amesikia kuhusu Yesu na alitaka sana nafasi ya kukutana naye. Lakini hakujua kwamba Yesu pia alitaka kukutana naye ili kumwongozea njia mpya ya kuishi. Kisha, nafasi imefika! Shauku ya kipofu ilikuwa kubwa sana hata hakuna mtu aweze  kumnyamazisha.

        Kilio cha kipofu ni kilio cha kila binadamu ambaye anajua udhaifu wake mwenyewe na kuhusu mahitaji ya huruma ya Mungu. Kipofu ni ishara ya kivuo dhahiri cha ndugu zetu wengi walio waathirika wa udhalimu na kosa la usawa wa kijamii. Ni nafasi ya kutambua kwamba watu wengi wanaanguka au wameachwa barabarani ama katika mahusiano yetu. Wanapaza sauti kwa huruma na kwa nafasi kwa sababu wanaamini kwamba wale ambao wanajiona kuwa wafuasi wa Yesu wanaweza kusikiliza sauti yao na kuwatendea mema. Yesu alisikia si kilio cha kipofu tu, bali pia kilio cha wale ambao walimwambia kipofu “anyamaze”!, wakionyesha kutojali. Yesu analaumu kutojali kwa sababu kunaharibu undugu na kukana utambulisho wa mwanafunzi wa kweli.  

     Hakika jibu la Yesu linaonyesha mchanganyiko wa huruma na hasira, kwa sababu alikuwa akishughulika kwa upofu wa aina mbili tofauti, yaani, upofu wa Bartimayo na upofu wa umati wa watu ambao walikuwa wakimfuata Yesu bila ushirika na hisia zake. Je, ni nani ana upofu zaidi, yule aliye kipofu asili au wale ambao hawapati kuona walio na mahitaji kandokando yao? Hata hivyo kuna tumaini, kwa sababu miongoni mwa wale ambao walimwambia kipofu “nyamaze!” walikuwapo wengine ambao walimwambia “jipe moyo, anakuita! Yeye hajakusahau wala hawaachi wale ambao wanamwamini”. Sauti hizi ni za watu ambao wanachukua ujumbe wa kinabii na kupata kuwahamasisha waliokata tamaa. Ni ishara pia ya walio vyombo vya Mungu katika maisha ya yeyote anayetaka kugundua wito wake ili aweze kumjibu Mungu kulingana na matarajio yake.

     Yesu ambaye tunamfuata ni mwenye hisia sana. Ana macho na masikio yalio makini sana kwa hali halisi ya watu. Anatualika kuwa na hisia sawa naye. Mara nyingi sisi tu kama kipofu huyo, yaani, tunahitaji na kutarajia mkutano wa mabadiliko ya maisha ili kuona vizuri kile kinachotokea kandokando yetu na kumfuata Yesu ambaye analeta maana mpya kwa maisha yetu. Tena mara nyingi sisi ni kama wengine karibu na Yesu, lakini mbali sana na ndugu, waliofungwa kwa hali iliyo kandokando yetu na hata tunafikiri kwamba tuna mamlaka ya kuwaambia wengine: “mnyamaze”. Hapo tuko na kosa kubwa. Tunapaswa kuwa macho kwa baadhi ya uzoefu wa sala ambao unatufungua kwa Mungu lakini unatufunga kwa wengine. Ikiwa imani yetu haituongozi kukutana na wengine wala haitufanyi wenye huruma, mbele ya mateso na mahitaji yao, imani ni kipofu, ni udanganyifu na kuhitaji kupona. Mungu atupatie neema ya imani ya kweli na halisi.

Fr Ndega

Nenhum comentário: